Siku moja pale Ubungo mataa (kabla ya kujengwa ile interchange) nilishuhudia timbwili la mwenye gari lake aliyekuwa mbele yetu, tukitokea Mwenge. Basi wakati tukisubiri taa za kijani zituruhusu kuendelea na safari,alitokea kijana na ndoo yake ndogo na vifaa vyake, ile anataka kuanza kuchafua kioo cha jamaa, akaambiwa kwa ishara asithubutu kufanya huo upuuzi.
Kijana akapuuzia akaendelea kumwaga povu kwenye kioo. Jamaa alishuka kwa kasi na hasira kali. Kijana akakunjwa shati, akapokonywa vifaa vyake na kutupwa kule, ndoo ya maji ikamwagwa chini na kukanyagwa na buti/kiatu kwa nguvu hadi kupasuka. Kijana alipopata upenyo alitimua mbio ili kujinusuru.