Pana tofauti za wazi baina ya wana Chadema almaarufu makamanda na wale wa ule upande mwingine wakiwamo CCM.
Habari ya mjini, masikioni mwa watanzania kwa sasa ni chanjo ya Corona. Safari inayotegemewa kufikishwa palipo pema takribani ndani ya kama wiki 2.
Habari ya mjini kwa makamanda ni:
1. Mwenyekiti wao aliyeko nyuma ya nondo kwa tuhuma zisizokubalika kwao.
2. Kuanzishwa kwa mchakato wa katiba mpya uliosimama.
Habari ya mjini kwa wale wa ule upande mwingine ni kupalilia utengamano wowote ndani ya mahasimu wao, kwa namna yoyote.
Hawa kama wale wengine wa walioibuka majuzi kati Dar, wanaongea lugha moja na wale wa ule upande mwingine.
Je, huu ni mwanzo wa mbingu mpya ambapo sasa kuna kukaribiana zaidi miongoni mwa baadhi ya makundi haya? Jambo la kheri maana umoja ni nguvu.
Au labda ni mwendelezo ule ule wa kuunga mkono juhudi uliozoeleka kama au ule wa wale wabunge 19, kina Lijualikali na wenzao? Almaarufu chini ya mwamvuli wa kuunga mkono juhudi?
Kwa kukaribiana huku, bila shaka makundi mapya haya yatakuwa yanakubaliana na kilichotokea Mwanza na yote yatokanayo, zikiwamo tuhuma zinazomkabili mwenyekiti wao.
Hata hivyo kinachotia shaka, wanaoyafanya haya mbele ya camera za TV hawatoi uthibitisho wowote kuonyesha kuwa wao kweli ni makamanda.
Kwa vile haupo mlango uliofungwa ndani ya Chadema ukiwamo ule wa kutokea, haiingii akilini ni vipi basi hawajapenda kuunga mkono juhudi.
Iwapo kwa kuunga mkono tu wengi wamepata ubunge, uwaziri, u RC, uDC nk ni vipi makamanda hawa kuendelea kudai wao ni Chadema damu na kuzikosa fursa zote mbele zao?
Kwa nini kuendelea kukomaa kwao wasionekane kuwa ni mamluki tu ndani ya magwanda?