Labda nikuzindue tu kwamba kumiliki dimba la kati ni namna tu, siyo mwisho, wa kuhakikisha ushindi. Ni namna ya kuharakisha ushindi kwa anayelimiliki wakati huohuo akichelewesha ushindi kwa adui. Ulichokuwa hukunifahamu ni kwamba si sahihi kusema Mkude amemdhibiti Tshishimbi kwa sababu tu hakuendelea kusumbua viungo wa Simba kama awali lakini kiwango na hatari ya Simba kushambuliwa ikabaki palepale. Hata alipoingia Mkude Simba bado haikusogea sana golini kwa Yanga ilhali Yanga iliendeleza mishitukizo ya mashambulizi ya hatari golini kwa Simba. Inaweza kuwa Tshishimbi hakuonekana sana baada ya Mkude kuingia (ingawa siyo kweli). Lakini imesaidia nini kama kasi ya Mashambulizi ya Yanga haikupungua? Nadhani mnaohisi hivyo mlikuwa mkiangalia zaidi Tshishimbi akiwa na mpira. Lakini mchezaji hodari huangaliwa zaidi asipokuwa na mpira. Wapi anakaa, nini anafanya, anawasaidiaje wenzake wenye mpira bila ya yeye kuucheza, anazibaje njia hatari za timu yake kufungwa, anafunguaje njia za timu yake kufunga, n.k. My take: hata baada ya Mkude kuingia Tshishimbi alin’gara zaidi kwa sababu aliendelea kuifanya timu yake iendelee kushambulia hata kama akiwa hana mpira. Na ndio maana ni Simba ndio walikuwa wanaomba mpira uishe licha ya Mkude kuwemo. Ndio maana mpira kwa dakika kumi za mwisho ulimalizikia kwa kona na kosakosa upande wa Simba. Ulivunjwa wakati Yanga wakijiandaa kurusha mpira kwenye robo ya timu ya Simba.