Man of the match: Papy Kabamba Tshishimbi

Fundi Papy Kabamba Tshitshimbi a.k.a Ngolo Kante a.k.a Kiboko ya mikia fc.
Siku ya tatu leo kipa wa mikia fc, Aishi Manula usiku halali analalamika mikono inamuuma na usiku anaweweseka anataja kila mara Tshishimbi Tshishimbi kisa mashuti makali ya Papy Kabamba Tshishimbi.
Mkuu nimecheka kwa sauti nadhani majirani wameshtuka. Hahaaa Yanga raha sana
 
Huyo Dogo naona na yeye anatafuta Jezi..kama yule aliyeandika Donald Ngoma hahha

Papy Kabamba Tshishimbi habari ya mjini
 
Nyie wagonjwa kwer kamsoko naye pind anafika sifa kibao soka la bongo bana fainali ni may 2018
 
Kabamba kama Sergio Busquet pale Barca huezi sikia akizungumza ila shughuli yake muulize Kotei.
Huyu fundi wa mpira halafu pacha wake hakuwepo Kamusoko

Wanasema Ulipo mpira na Papy yupo

Kaletewa Mkude,Ndemla ila bado mutu ya Kongo kawafunika.
Alipoingia MKUDE tu katikati akachukua dimba kama kawaida yake.
 
Fundi Papy Kabamba Tshitshimbi a.k.a Ngolo Kante a.k.a Kiboko ya mikia fc.
Siku ya tatu leo kipa wa mikia fc, Aishi Manula usiku halali analalamika mikono inamuuma na usiku anaweweseka anataja kila mara Tshishimbi Tshishimbi kisa mashuti makali ya Papy Kabamba Tshishimbi.
Nilifikiri magoli kumbe mashuti, mpira Tanzania bado sana. Yaani unamlenga kipa halafu unasifiwa eti unajua mpira???
 
Alipoingia Mkude katikati Simba wakapamiliki na ndio maana official ball possession ya Simba ilikuwa juu ya ile ya Yanga.
Na ndio maana mpira ukamalizikia kwa kona na kosakosa nyingi golini kwa Simba nini?
 
Nazungumzia stats za ball possession ambazo Simba ni 58% na Yanga ni 42%. Achana na zile long balls toka golini kwa Yanga kwenda Simba ambazo obviously zilikuwa na madhara kwa Simba kwa sababu walikuwa focused kwenda mbele zaidi kuliko kudefend.
 
Ya

YA MTIBWA TULISHANGILIA KWASABABU TULIFANYA MAKOSA MENGI NA HATUKUCHEZA VIZURI KWAHIYO MTIBWA WALICHEZA VIZURI SASA NYIE ETI MNA MAN OF THE MATCH LEO WA JANGWANI HE HE AU KWASABABU MMEZOEA MARA NYINGI KIPINDI CHA PILI HUWA TUNACHEZA SABA SASA LEO MKAONA HUU MZIKI WA KUMI NA MOJA KWA KUMI NA MOJA MTAUWEZA KWELI.PENATI MBILI MMESAMEHEWA!
Penati mbili mmeshinda zote...so simba 3-yanga 1 maana manara anataka kukata rufaa
 
Nazungumzia stats za ball possession ambazo Simba ni 58% na Yanga ni 42%. Achana na zile long balls toka golini kwa Yanga kwenda Simba ambazo obviously zilikuwa na madhara kwa Simba kwa sababu walikuwa focused kwenda mbele zaidi kuliko kudefend.
Naona umepoteza kumbukumbu mkuu. Unazungumzia kuingia kwa Mkude na jinsi alivyomiliki dimba la kati kiasi kwamba umiliki wa mpira (ball possession) kwa Simba ukawa uko juu . Ingawa hata kabla ya kuingia yeye umiliki wa mpira ulizidi ule wa Yanga, nilikuunga mkono. Kwa sababu mpira ulimalizikia golini kwa Simba baada ya kona na mashambulizi kadhaa. Nadhani ni kwa sababu Mkude hakuwapo eneo la golini kwao, alikuwa akiendelea kumiliki dimba la kati ili kuimarisha umiliki wa mpira. Au siyo?
 
Kwa namna ulivyoandika nimeshindwa kukupata vizuri. Niseme tu kifupi kuwa mara zote dimba la kati anapocheza Mkude huwa anawamudu sana Yanga kuliko ilivyokuwa kwa Kotei.

Hakuna wakati ambapo Tshishimbi amecheza (akang'ara) wakati Mkude akiwa kati katika mechi zote mbili ambazo Yanga amecheza na Simba.

Siku ambapo Dimba litakuwa kati ya Tshishimbi na Mkude halafu Tshishimbi ang'are hapo nitaamini kuwa jamaa ni kifaa. Kwa sasa bado benchmark yangu haijawa tested.
 
Labda nikuzindue tu kwamba kumiliki dimba la kati ni namna tu, siyo mwisho, wa kuhakikisha ushindi. Ni namna ya kuharakisha ushindi kwa anayelimiliki wakati huohuo akichelewesha ushindi kwa adui. Ulichokuwa hukunifahamu ni kwamba si sahihi kusema Mkude amemdhibiti Tshishimbi kwa sababu tu hakuendelea kusumbua viungo wa Simba kama awali lakini kiwango na hatari ya Simba kushambuliwa ikabaki palepale. Hata alipoingia Mkude Simba bado haikusogea sana golini kwa Yanga ilhali Yanga iliendeleza mishitukizo ya mashambulizi ya hatari golini kwa Simba. Inaweza kuwa Tshishimbi hakuonekana sana baada ya Mkude kuingia (ingawa siyo kweli). Lakini imesaidia nini kama kasi ya Mashambulizi ya Yanga haikupungua? Nadhani mnaohisi hivyo mlikuwa mkiangalia zaidi Tshishimbi akiwa na mpira. Lakini mchezaji hodari huangaliwa zaidi asipokuwa na mpira. Wapi anakaa, nini anafanya, anawasaidiaje wenzake wenye mpira bila ya yeye kuucheza, anazibaje njia hatari za timu yake kufungwa, anafunguaje njia za timu yake kufunga, n.k. My take: hata baada ya Mkude kuingia Tshishimbi alin’gara zaidi kwa sababu aliendelea kuifanya timu yake iendelee kushambulia hata kama akiwa hana mpira. Na ndio maana ni Simba ndio walikuwa wanaomba mpira uishe licha ya Mkude kuwemo. Ndio maana mpira kwa dakika kumi za mwisho ulimalizikia kwa kona na kosakosa upande wa Simba. Ulivunjwa wakati Yanga wakijiandaa kurusha mpira kwenye robo ya timu ya Simba.
 
Kucheza mpira kwenye final third bila kupata ushindi kwenye football ni nothing kwa sababu .mpira unaweza kurudi upande mwingine na likawa goli. Stats zinaonesha kuwa Yanga wamepiga mashuti mengi on target kuliko Simba lakini with few shoots Simba wakapata goli.
Kwahiyo kushambulia is one thing na kupata ushindi is completely a different thing.
 
Kushambulia ndio njia pekee ya kupata ushindi. Kutumia nafasi vizuri ndio kinachobaki ili goli liingie. Kadri unavyoshambulia ndivyo unavyoelekea kupata goli. Na kadri unavyocheza zaidi kwenye ngwe ya mwisho ya adui ndivyo ushambuliaji unavyokuwa endelevu, hivyo kutengeneza nafasi nyingi za kufunga. Na kadri unavyotengeneza nafasi nyingi za kufunga ndivyo uwezekano wa kufunga unavyoongezeka. Ndio maana hakuna timu inayoruhusu kwa makusudi kuchezewa mpira ndani ya kumi na nane yao. Simba hawakuridhia kuchezewa hivyo, imewakuta tu; pamoja na kuwepo Mkude. Kwamba Simba ilitumia nafasi moja tu kushinda imetokana zaidi na makosa ya kipa kuliko utimilifu wa shambulizi lao. Kwamba Yanga haikutangulia kufunga ilitokana zaidi na uwezo wa kipa wa Simba kuliko ubutu wa mashambulizi yenyewe. Anyway, umenifanya nikufuate kwenye kutoka nje ya mjadala mama wa Mkude na Tshishimbi. Naamini umekubaliana nami, maana hatimaye hukuongea chochote kuhusu hilo.
 
Kwanza nikupe heads up kwa kulifanya jukwaa hili kuwa lenye uchambuzi zaidi kuliko ushabiki. Nadhani ukiendelea kupitia jukwaa hili na kutoa uchambuzi wako utakuwa unatenda haki zaidi.

Nirudi kwenye topic, Mkude aliingia wakati almost mpira unakwisha zikiwa zimesalia dakika chache sana kipyenga cha mwisho kupulizwa, hata hivyo alionekana kung'ara zaidi kwa maana ya kuiunganisha timu toka defence kwenda forward kuliko mwanzoni.

Kwa stats hizi hapa chini sioni ni wapi Yanga walilishambulia sana lango la Simba. Yanga walipiga mipira michache zaidi kuelekea golini kwa Simba (On target + Off target) kulinganisha na Simba ambao jumla walipiga mipira mara 16 dhidi ya mara 12 ya Yanga.

Simba walipata kona nyingi zaidi ya Yanga na mwisho wa siku walimiliki zaidi mpira kuliko Yanga kwa kiwango kikubwa sana kama inavyooneshwa hapo chini.

Yet in my book, Simba wali underperform.

Stats Yanga Simba
Shots on Target 9 4
Shots off Target 3 12
Corners 5 6
Ball Possession 42% 58%
 
Shukran kwa maoni yako mema kuhusu mimi na jukwaa hili. Nami nakushukuru pia kwa mjadala uliojaa ustaarabu, hekima na busara. Natamani wana-Jamii Forum wote wangekuiga wewe jinsi ya kutetea hoja bila ya jazba wala mihemko na kuhoji bila ya kejeli wala kiburi.
Kinachotutofautisha mimi na wewe kwenye mjadala wetu ni kuzimwa kwa Tshishimbi baada ya kuingia Mkude. Sipingani hata chembe na takwimu ulioztoa. Ila naomba nikutanabahishe kupitia kwa usemi wa mwandishi maarufu, Mark Twain. Anasema takwimu ni kama bikini (suti ya kuogelea). Inachoonesha ni udhanifu, lakini inachoficha ndio muhimu (statistics are like a bikini. What they reveal is suggestive, what they conceal is vital). Na kwenye hizi takwimu ulizoainisha, what was vital ni rate of attacking success, yaani kima cha ufanisi wa mashambulizi. Kinapimwa kwanza kwa magoli yaliyofungwa, yakifuatiwa na mipira iliyolenga golini, yakifuatiwa na mipira isiyolenga golini, ikifuatiwa na kima cha umiliki wa mpira. Ilivyokuwa Yanga na Simba zimefunga magoli sawa, aliyecheza vizuri zaidi anapaswa kupimwa kwa aliyelenga mipira mingi zaidi golini. Laiti na idadi hiyo Ingekuwa sawa, angefuatia aliyetoa mipira mingi zaidi nje ya goli. Na kama hiyo ingekuwa sawa, angefuatia aliyemiliki zaidi mpira.
Aidha, kazi ya mchezaji wa kiungo ni kudhibiti mashambulizi ya adui na kusukuma mashambulizi ya timu yake. Si kazi ya mchezaji wa kiungo kumdhibiti mchezaji mwenzake - awe wa kiungo au mwenginewe. Kufanya hivyo ni njia mojawapo tu ya huko kudhibiti mashambulizi dhidi ya timu yake na kusaidia mashambulizi ya timu yake. Kwa hivyo ubora wa Tshishimbi na Mkude usipimwe kwa vipi mmoja alimdhibiti mwenzake, bali upimwe kwa alivyoisaidia timu yake kujihami na kushambulia. Na kwa hilo imani yangu ni kwamba Tshishimbi alikuwa zaidi.
 
Wachezaj wapo wa aina tatu.
1st.wachezaj wa big mechi kubwa
2nd.wachezaj wa mechi ndogo.
Apo ndo utaona tofaut ya okwi na manula, tshishimbi na okwi.
 
Back
Top Bottom