Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Licha ya kuwa na msimu mbaya, Manchester United imekamilisha mchezo wake wa mwisho kwenye Uwanja wa Old Trafford msimu huu wa 2021/22 kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brentford.
Katika mchezo huo wa Premier League mabao yamefungwa na Bruno Fernandes ambaye amefunga bao lake la 50 tangu atue kikosini hapo, Cristiano Ronaldo na Raphael Varane aliyefunga bao lake la kwanza katika #EPL.
United sasa imesaliwa na michezo miwili ili kukamlisha ratiba ya msimu ambapo yote itakuwa ugenini.