Manabii wa "Mchongo" - Njia rahisi ya kuwatambua na kujiepusha nao

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Nyakati hizi kuna watu wengi wanaoitwa manabii. Nabii ni mtu anayepokea ufunuo au maono kutoka kwa Mungu na kuyatangaza kwa watu. Kwa maneno mengine Nabii ni mtu anayeongea kwa niaba ya Mungu. Je, kila anayejiita Nabii ni nabii wa kweli? Biblia inatufundisha kwamba siku za mwisho, manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya watu wengi, yamkini hata walio wateule(Mt 24:24).

Hebu leo tuchunguze kwa makini tabia na mwenendo wa "manabii wa mchongo," yaani manabii feki au wa uongo, ili tujihadhari tusije tukadanganywa na kuiacha imani ya kweli, au tukaliwa pesa zetu bure.

Jinsi ya Kuwatambua Manabii wa Uongo.
1. Wanatangaza ufunuo au maono yao wenyewe, yaani yasiyotoka kwa Mungu.
Yeremia 14:14
"...Hao manabii wanatoa unabii wa uongo kwa jina langu. Mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, uaguzi usio na maana yoyote, uongo wanaojitungia wenyewe."

2. Ni watu wanaotafuta faida binafsi – Wanahubiri kwa lengo la kupata pesa na heshima kutoka kwa watu badala ya kutangaza kweli ya Mungu (Mika 3:11).

3. Hufanya miujiza ya uongo (2 Wathesalonike 2:9). Wanafanya miujiza feki ili kuwavuta watu. Wengine hukodi watu wa kushuhudia uongo kwamba wamepona au kupata miujiza fulani.

4. Hupotosha mafundisho ya Biblia – Wanachanganya ukweli na uongo na kuwavuruga watu wa Mungu (2 Petro 2:1-3).

5. Wanaishi maisha ya dhambi – Kwa haraka haraka wanaweza kuonekana kuwa watu wa Mungu, lakini ukichunguza kwa makini maisha yao utagundua yako kinyume na Neno la Mungu (Mathayo 7:15-20).

6. Hawana ushuhuda wa unabii uliotimia – Nabii wa kweli anathibitishwa pale unabii aliotoa unapotimia (Kumbukumbu 18:22). Manabii wa uongo, wakitoa unabii unaotimia huwa wanasema mambo ambayo hata kwa akili tu za kawaida unaweza kujua yatatokea. Kwa mfano kusema: "mwaka huu utakuwa mwaka wa baraka." "Fulani atashinda uchaguzi."

7. Hupenda kujikweza kwa kujiita majina mazito mazito kama vile: Nabii wa Kimataifa, "Master Prophet" nk. Katika Biblia hakuna nabii aliyejiita Nabii mkubwa. Wanazuoni tu ndio wanawaita hivyo manabii wale ambao vitabu vyao ni virefu.

8. Kuna wengine hawatabiri chochote lakini kwakuwa wanajiita manabii, hutumia jina hilo kufundisha mafundisho potofu. Mfano mzuri ni Shemaya. Huyu alijifanya kuwa ana mamlaka ya kinabii na akawachochea watu kupinga kweli ya Mungu. Katika Yer 29:24-32 tunasoma kwamba alituma barua kwa makuhani wa Yerusalemu akiwataka wamwondoe Yeremia kwa sababu ya ujumbe wake kuhusu uhamisho wa Babeli. Alidai kuwa Yeremia sio nabii wa kweli, akajaribu kuwashawishi watu wasimsikilize Yeremia.

Mpaka hapo naamini umetambua jinsi ya kuwatambua manabii wa mchongo au manabii wa uongo. Ufanyeje sasa ili kujiepusha nao? Zingatia njia hizi tatu kuu:

1. Pima Mafundisho yao kwa Neno la Mungu – Linganisha mafundisho yao kwa kusoma Biblia. Manabii wa kweli hufundisha kulingana na Biblia bila kupotosha Maandiko kwa faida zao binafsi. Kwa mfano, kama Nabii anakuambia "Biblia sio Neno la Mungu - ni maneno tu ya watu," soma mwenyewe Biblia utakuta Maandiko haya:

2 Timotheo 3:16 – “Kila Andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.”
Andiko hilo linaonyesha kuwa Biblia ni kitabu kilichoandikwa kwa Uongozi wa Roho Mtakatifu.

2 Petro 1:20-21 – “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”

Kwahiyo maneno aliyoyaandika Paulo, kwa mfano, sio yake; ni maneno aliyoyaandika kwa kuongozwa na Mungu. Mwanafunzi akinakili maneno yaliyoandikwa ubaoni na mwalimu, huyo mwanafunzi atasema ni yake?

2. Angalia Matunda ya Maisha Yao – Yesu alisema “Mtawatambua kwa matunda yao” (Mathayo 7:16). Manabii wa kweli huonyesha tabia ya utakatifu, unyenyekevu, na maisha yanayoakisi tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23).

3. Epuka Kufuata Miujiza tu – Manabii wa uongo mara nyingi hufanya ishara na miujiza ili kuwapotosha watu. Usivutwe tu na miujiza, bali hakikisha kuwa mafundisho yao yanakuhimiza kuwa mtakatifu mbele za Mungu. Pasipo utakatifu hakuna mtu atakayemuona Mungu(Ebr 12:14).

Mungu atusaidie tuwe waangalifu na kuhakikisha kuwa hatudanganywi na manabii wa uongo, wanaotumia jina la Mungu ili "kupiga pesa" na kuwatoa watu kwenye imani sahihi.

Katika post #2 ntaelezea sifa za manabii wa kweli.

May the LORD bless you and protect you from the wiles of the devil and all his agents. Amen
 
Sifa za Nabii wa Kweli
Ujumbe wake unatoka kwa Mungu – (Yeremia 1:9) Mungu mwenyewe ndiye anayeweka na kuwatuma manabii wake.

Nabii wa kweli unabii wake unatimia(Kumbukumbu 18:22). Unabii wa kweli hutokea kama Mungu alivyoahidi.

Anahubiri kuhusu toba, haki na utakatifu – Nabii wa kweli anapohubiri huwaita watu wamrudie Mungu na kuacha dhambi (Yeremia 23:22).

Haombi pesa wakati wa huduma – Huduma yake sio biashara (Mika 3:11).

Anaishi maisha matakatifu – Nabii wa kweli huishi kulingana na Neno la Mungu (Mathayo 7:16-20).
 
Hata Yesu alisema yupo midomoni mwetu Ila mioyo yetu ipo mbali nae,

Watu wengi wanataka miujiza na uponyaji mkuu,
 
Mifano ya Manabii wa Kweli Katika Biblia ambao unabii wao ulitimia:
Musa – Alitabiri ujio wa Yesu Kristo ukatimia (Kumbukumbu 18:15).
Isaya – Alitabiri kuzaliwa kwa Yesu ikatimia (Isaya 7:14).
Yeremia – Alitabiri uharibifu wa Yerusalemu ikatimia (Yeremia 25:11).
Ezekieli – Aliona maono ya kurejeshwa kwa Israeli, ikawa hivyo (Ezekieli 37:1-14).
Nabii wa kweli anadhihirika kwa jinsi unabii aliotoa ulivyotimia.
 
Mada ndefu sana hvy sijasoma mada ila sasa hao manabii wale wapi na wana familia, mtaani kuna pesa nyingi sana za wapuuzi ndo mana wachungaji na manabii wanatajirika kitu ambacho nakiunga mkono
 
Mifano ya manabii wa uongo waliotoa unabii au utabiri ambao haukutimia:

1. Hanania mwana wa Azuri
Yeremia 28
Hanania alitabiri kuwa nira ya Babeli itavunjika na Wayahudi walioko uhamishoni watarudi Yerusalemu ndani ya miaka miwili (Yeremia 28:2-4).
Yeremia alimkemea na kusema kuwa Hanania alikuwa amesema uongo. Mungu akasema Hanania atakufa kwa sababu ya unabii wake wa uongo, na kweli alikufa mwaka huo huo (Yeremia 28:15-17).

2. Manabii wa uongo wakati wa Mfalme Ahabu
1 Wafalme 22
Wakiongozwa na Sedekia mwana wa Kenaana, manabii 400 walitabiri kuwa Mfalme Ahabu atashinda vita dhidi ya Washamu (1 Wafalme 22:6, 11-12).
Nabii wa kweli Mika mwana wa Imla alitabiri kinyume, akasema Ahabu atauawa. Hatimaye, Ahabu aliuawa vitani kama Mika alivyotabiri (1 Wafalme 22:34-37).

3. Manabii wa uongo wa wakati wa Ezekieli
Ezekieli 13
Walisema kuwa Yerusalemu haitaanguka, wakati Mungu alikuwa amesema kuwa Babeli itashinda na kuharibu mji huo.
Yerusalemu ilianguka mwaka 586 KK, kuthibitisha kuwa hao walikuwa manabii wa uongo (Ezekieli 13:8-9).

5. Bar Yesu (Elima)
Matendo 13:6-12
Huyu alikuwa mchawi na nabii wa uongo aliyepinga Injili alipokutana na Paulo na Barnaba. Paulo alimkemea na kumwambia kwamba alikuwa anapotosha njia za Bwana, na mara moja akapigwa upofu kwa muda.
 
Mada ndefu sana hvy sijasoma mada
Hili ndio tatizo kubwa. Kama hiyo page moja tu unashindwa kusoma, Biblia yote ndo utaweza kuisoma mkuu? Na hapo nime-summarize! Manabii wa uongo wanatumia mwanya huo kuwapotosha watu. Kwa kuwa watu ni wavivu kusoma Biblia, basi Nabii anaweza kujitamkia chochote tu akijua watu watamwamini kwa kuwa hawasomi Biblia.
 
Nyakati hizi kuna watu wengi wanaoitwa manabii. Nabii ni mtu anayepokea ufunuo au maono kutoka kwa Mungu na kuyatangaza kwa watu. Kwa maneno mengine Nabii ni mtu anayeongea kwa niaba ya Mungu. Je, kila anayejiita Nabii ni nabii wa kweli? Biblia inatufundisha kwamba siku za mwisho, manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya watu wengi, yamkini hata walio wateule(Mt 24:24).

Hebu leo tuchunguze kwa makini tabia na mwenendo wa "manabii wa mchongo," yaani manabii feki au wa uongo, ili tujihadhari tusije tukadanganywa na kuiacha imani ya kweli, au tukaliwa pesa zetu bure.

Jinsi ya Kuwatambua Manabii wa Uongo.
1. Wanatangaza ufunuo au maono yao wenyewe, yaani yasiyotoka kwa Mungu.
Yeremia 14:14
"...Hao manabii wanatoa unabii wa uongo kwa jina langu. Mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, uaguzi usio na maana yoyote, uongo wanaojitungia wenyewe."

2. Ni watu wanaotafuta faida binafsi – Wanahubiri kwa lengo la kupata pesa na heshima kutoka kwa watu badala ya kutangaza kweli ya Mungu (Mika 3:11).

3. Hufanya miujiza ya uongo (2 Wathesalonike 2:9). Wanafanya miujiza feki ili kuwavuta watu. Wengine hukodi watu wa kushuhudia uongo kwamba wamepona au kupata miujiza fulani.

4. Hupotosha mafundisho ya Biblia – Wanachanganya ukweli na uongo na kuwavuruga watu wa Mungu (2 Petro 2:1-3).

5. Wanaishi maisha ya dhambi – Kwa haraka haraka wanaweza kuonekana kuwa watu wa Mungu, lakini ukichunguza kwa makini maisha yao utagundua yako kinyume na Neno la Mungu (Mathayo 7:15-20).

6. Hawana ushuhuda wa unabii uliotimia – Nabii wa kweli anathibitishwa pale unabii aliotoa unapotimia (Kumbukumbu 18:22). Manabii wa uongo, wakitoa unabii unaotimia huwa wanasema mambo ambayo hata kwa akili tu za kawaida unaweza kujua yatatokea. Kwa mfano kusema: "mwaka huu utakuwa mwaka wa baraka." "Fulani atashinda uchaguzi."

7. Hupenda kujikweza kwa kujiita majina mazito mazito kama vile: Nabii wa Kimataifa, "Master Prophet" nk. Katika Biblia hakuna nabii aliyejiita Nabii mkubwa. Wanazuoni tu ndio wanawaita hivyo manabii wale ambao vitabu vyao ni virefu.

8. Kuna wengine hawatabiri chochote lakini kwakuwa wanajiita manabii, hutumia jina hilo kufundisha mafundisho potofu. Mfano mzuri ni Shemaya. Huyu alijifanya kuwa ana mamlaka ya kinabii na akawachochea watu kupinga kweli ya Mungu. Katika Yer 29:24-32 tunasoma kwamba alituma barua kwa makuhani wa Yerusalemu akiwataka wamwondoe Yeremia kwa sababu ya ujumbe wake kuhusu uhamisho wa Babeli. Alidai kuwa Yeremia sio nabii wa kweli, akajaribu kuwashawishi watu wasimsikilize Yeremia.

Mpaka hapo naamini umetambua jinsi ya kuwatambua manabii wa mchongo au manabii wa uongo. Ufanyeje sasa ili kujiepusha nao? Zingatia njia hizi tatu kuu:

1. Pima Mafundisho yao kwa Neno la Mungu – Linganisha mafundisho yao kwa kusoma Biblia. Manabii wa kweli hufundisha kulingana na Biblia bila kupotosha Maandiko kwa faida zao binafsi. Kwa mfano, kama Nabii anakuambia "Biblia sio Neno la Mungu - ni maneno tu ya watu," soma mwenyewe Biblia utakuta Maandiko haya:

2 Timotheo 3:16 – “Kila Andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.”
Andiko hilo linaonyesha kuwa Biblia ni kitabu kilichoandikwa kwa Uongozi wa Roho Mtakatifu.

2 Petro 1:20-21 – “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”

Kwahiyo maneno aliyoyaandika Paulo, kwa mfano, sio yake; ni maneno aliyoyaandika kwa kuongozwa na Mungu. Mwanafunzi akinakili maneno yaliyoandikwa ubaoni na mwalimu, huyo mwanafunzi atasema ni yake?

2. Angalia Matunda ya Maisha Yao – Yesu alisema “Mtawatambua kwa matunda yao” (Mathayo 7:16). Manabii wa kweli huonyesha tabia ya utakatifu, unyenyekevu, na maisha yanayoakisi tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23).

3. Epuka Kufuata Miujiza tu – Manabii wa uongo mara nyingi hufanya ishara na miujiza ili kuwapotosha watu. Usivutwe tu na miujiza, bali hakikisha kuwa mafundisho yao yanakuhimiza kuwa mtakatifu mbele za Mungu. Pasipo utakatifu hakuna mtu atakayemuona Mungu(Ebr 12:14).

Mungu atusaidie tuwe waangalifu na kuhakikisha kuwa hatudanganywi na manabii wa uongo, wanaotumia jina la Mungu ili "kupiga pesa" na kuwatoa watu kwenye imani sahihi.

Katika post #2 ntaelezea sifa za manabii wa kweli.

May the LORD bless you and protect you from the wiles of the devil and all his agents. Amen
wataje na hawa wa kizazi hiki
naona unataja waisraeli tu
 
Hili ndio tatizo kubwa. Kama hiyo page moja tu unashindwa kusoma, Biblia yote ndo utaweza kuisoma mkuu? Na hapo nime-summarize! Manabii wa uongo wanatumia mwanya huo kuwapotosha watu. Kwa kuwa watu ni wavivu kusoma Biblia, basi Nabii anaweza kujitamkia chochote tu akijua watu watamwamini kwa kuwa hawasomi Biblia.
Inasikitisha sana mkuu 😎
 
Manabii wa uongo kazi yao ni

Kuwaambia watu wanunue chumvi
Kuwauzia watu fruto wakidai ni damu ya Yesu
Kuwauzia watu mafuta wakidai yana upako
Kuwakanyagisha Watanzania mafuta
Kuwauzia wananchi maji wakidai yana upako
Kuwauzia watu vitambaa wakidai vina upako
Kuwashikisha vazi au nguo walizovaa wakidai zina upako

Pia Ibada zao zina sadaka nyingi zisizo na maelezo

Na wamejazana miji yenye mizinguko ya pesa wapo Arusha,Dar na Mwanza huwezi wasikia wameenda Kilolo,ruvuma,simiyu,singida wote wapo mjini 😃🙆

Tuwakatae hawa Matapeli wa Imani, hawa hawakuombei bila kuwapa pesa au kukuuzia bidhaa zao za kichawi
 
Nyakati hizi kuna watu wengi wanaoitwa manabii. Nabii ni mtu anayepokea ufunuo au maono kutoka kwa Mungu na kuyatangaza kwa watu. Kwa maneno mengine Nabii ni mtu anayeongea kwa niaba ya Mungu. Je, kila anayejiita Nabii ni nabii wa kweli? Biblia inatufundisha kwamba siku za mwisho, manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya watu wengi, yamkini hata walio wateule(Mt 24:24).

Hebu leo tuchunguze kwa makini tabia na mwenendo wa "manabii wa mchongo," yaani manabii feki au wa uongo, ili tujihadhari tusije tukadanganywa na kuiacha imani ya kweli, au tukaliwa pesa zetu bure.

Jinsi ya Kuwatambua Manabii wa Uongo.
1. Wanatangaza ufunuo au maono yao wenyewe, yaani yasiyotoka kwa Mungu.
Yeremia 14:14
"...Hao manabii wanatoa unabii wa uongo kwa jina langu. Mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, uaguzi usio na maana yoyote, uongo wanaojitungia wenyewe."

2. Ni watu wanaotafuta faida binafsi – Wanahubiri kwa lengo la kupata pesa na heshima kutoka kwa watu badala ya kutangaza kweli ya Mungu (Mika 3:11).

3. Hufanya miujiza ya uongo (2 Wathesalonike 2:9). Wanafanya miujiza feki ili kuwavuta watu. Wengine hukodi watu wa kushuhudia uongo kwamba wamepona au kupata miujiza fulani.

4. Hupotosha mafundisho ya Biblia – Wanachanganya ukweli na uongo na kuwavuruga watu wa Mungu (2 Petro 2:1-3).

5. Wanaishi maisha ya dhambi – Kwa haraka haraka wanaweza kuonekana kuwa watu wa Mungu, lakini ukichunguza kwa makini maisha yao utagundua yako kinyume na Neno la Mungu (Mathayo 7:15-20).

6. Hawana ushuhuda wa unabii uliotimia – Nabii wa kweli anathibitishwa pale unabii aliotoa unapotimia (Kumbukumbu 18:22). Manabii wa uongo, wakitoa unabii unaotimia huwa wanasema mambo ambayo hata kwa akili tu za kawaida unaweza kujua yatatokea. Kwa mfano kusema: "mwaka huu utakuwa mwaka wa baraka." "Fulani atashinda uchaguzi."

7. Hupenda kujikweza kwa kujiita majina mazito mazito kama vile: Nabii wa Kimataifa, "Master Prophet" nk. Katika Biblia hakuna nabii aliyejiita Nabii mkubwa. Wanazuoni tu ndio wanawaita hivyo manabii wale ambao vitabu vyao ni virefu.

8. Kuna wengine hawatabiri chochote lakini kwakuwa wanajiita manabii, hutumia jina hilo kufundisha mafundisho potofu. Mfano mzuri ni Shemaya. Huyu alijifanya kuwa ana mamlaka ya kinabii na akawachochea watu kupinga kweli ya Mungu. Katika Yer 29:24-32 tunasoma kwamba alituma barua kwa makuhani wa Yerusalemu akiwataka wamwondoe Yeremia kwa sababu ya ujumbe wake kuhusu uhamisho wa Babeli. Alidai kuwa Yeremia sio nabii wa kweli, akajaribu kuwashawishi watu wasimsikilize Yeremia.

Mpaka hapo naamini umetambua jinsi ya kuwatambua manabii wa mchongo au manabii wa uongo. Ufanyeje sasa ili kujiepusha nao? Zingatia njia hizi tatu kuu:

1. Pima Mafundisho yao kwa Neno la Mungu – Linganisha mafundisho yao kwa kusoma Biblia. Manabii wa kweli hufundisha kulingana na Biblia bila kupotosha Maandiko kwa faida zao binafsi. Kwa mfano, kama Nabii anakuambia "Biblia sio Neno la Mungu - ni maneno tu ya watu," soma mwenyewe Biblia utakuta Maandiko haya:

2 Timotheo 3:16 – “Kila Andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.”
Andiko hilo linaonyesha kuwa Biblia ni kitabu kilichoandikwa kwa Uongozi wa Roho Mtakatifu.

2 Petro 1:20-21 – “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”

Kwahiyo maneno aliyoyaandika Paulo, kwa mfano, sio yake; ni maneno aliyoyaandika kwa kuongozwa na Mungu. Mwanafunzi akinakili maneno yaliyoandikwa ubaoni na mwalimu, huyo mwanafunzi atasema ni yake?

2. Angalia Matunda ya Maisha Yao – Yesu alisema “Mtawatambua kwa matunda yao” (Mathayo 7:16). Manabii wa kweli huonyesha tabia ya utakatifu, unyenyekevu, na maisha yanayoakisi tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23).

3. Epuka Kufuata Miujiza tu – Manabii wa uongo mara nyingi hufanya ishara na miujiza ili kuwapotosha watu. Usivutwe tu na miujiza, bali hakikisha kuwa mafundisho yao yanakuhimiza kuwa mtakatifu mbele za Mungu. Pasipo utakatifu hakuna mtu atakayemuona Mungu(Ebr 12:14).

Mungu atusaidie tuwe waangalifu na kuhakikisha kuwa hatudanganywi na manabii wa uongo, wanaotumia jina la Mungu ili "kupiga pesa" na kuwatoa watu kwenye imani sahihi.

Katika post #2 ntaelezea sifa za manabii wa kweli.

May the LORD bless you and protect you from the wiles of the devil and all his agents. Amen
Amina.
 
Na manabii wa uongo waumini wao uwaambii kitu kuhusu wao ,hata ngumu utapigwa ukimsema nabii wa mtu mbele yake haswaa kina dada na wa mama😄
 
Watu wengi wanataka miujiza na uponyaji mkuu,
Ni kweli, wanataka miujiza lakini ukiwaambia waache dhambi hawataki.
Ndivyo ilivyokuwa hata wakati wa Yesu
Yohana 6:26 NEN
Yesu akawajibu, “Amin, amin nawaambia, ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba."
 
Back
Top Bottom