Manabii wa uongo

Manabii wa uongo

Hawa tunaweza kuwaita matapeli tu, hawana sifa za kuitwa manabii kwa mujibu wa maandiko ya biblia. Manabii gani wanakula bata pamoja na watawala?

Manabii gani wanaishi maisha ya anasa na ufahari? Manabii wana vitambi na shavu dodo! Wamenenepeana kuliko waumini wao kwa ukwasi walionao. Hawa ni wajanja fulani wenye kazi maalumu kwa jamii na sio unabii wa Mungu
Hivi yule aliesema dar inaangamizwa mwezi huu, mbona siku zinayoyoma au tayari?
 
Anatumia unabii kukuambia mbaya wako!! Hii ni ramli chonganishi, siku mtu akiamua kumkatakata mwenzake kwa panga ndio serikali itaingilia kati.
 
Anatumia unabii kukuambia mbaya wako!! Hii ni ramli chonganishi, siku mtu akiamua kumkatakata mwenzake kwa panga ndio serikali itaingilia kati.
Kweli kabisa Muombee mtu apone hahitaji kujua nani alimuharibia
 
Hata uwaambie vipi waumini wa hao manabii kamwe hawabanduki na wameshaaminishwa anayepinga au kuleta hoja pinzani basi ni mfuasi wa shetani au ibilisi
 
Back
Top Bottom