POTOSHI Manara alisema hakuna jipya wanalofanya Yanga ambalo Simba haijafanya

POTOSHI Manara alisema hakuna jipya wanalofanya Yanga ambalo Simba haijafanya

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Nimekutana na hii Video inasambaa huko Instagram ikimhusu aliyekuwa Msemaji wa Yanga, Haji Sunday Manara ikiwa na maneno kuwa Yanga haifanyi lolote jipya ambalo halikuwahi kufanywa na Simba!

Imenishangaza hii kauli kama ni kweli Manara aliongea hivyo au imechezewa?

1731404901036.png



 
Tunachokijua
Aliyewahi kuwa Msemaji wa vilabu yva soka vya Simba na Yanga kwa nyakati tofauti Haji Manara na Mkurugenzi wa Manara Tv Mnamo Tarehe 9 2024 alifanya mahojiano na Millard Ayo ambapo alizungumzia mambo kadhaa ikiwemo Nafasi yake ya kiungozi ndani ya klabu ya Yanga pamoja na mahusiano yake ya sasa kati yake na Viongozi wa timu hiyo.

Kumeibuka taarifa yenye madai kuwa Haji Manara kwenye mahojiano hayo amesema kuwa hakuna kitu kipya ambacho Yanga inafanya na Simba haikuwahi kufanya huko nyuma, Kwa rejea tazama hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa na hapa

Je, Uhalisia wa Madai haya ni upi?
JamiiCheck imefuatilia mahojiano hayo na kubaini kuwa taarifa hiyo inapotosha kwani Manara hakusema hakuna kitu ambacho Yanga inafanya na hakikuwahi kufanywa na Simba huko Nyuma.

Kwenye mahojiano ambayo Haji Manara alifanya Tarehe 9 2024 na Millard Ayo alipokuwa akieleza kuhusu maendeleo ya Mpira wa Tanzania hasa Timu ya Taifa akibainisha changamoto zinazopelekea Timu ya Taifa kutokuwa na mwendelezo wa kufanya vizuri ambapo alisema moja ya Changamoto ni kutokuwepo kwa ukuzaji na uendeleza wa vipaji kutoka kwa watoto ambapo alieleza kuwa kwa sasa wachezaji wengi umri wao siyo halisi kama wanavyodai.

Katika kuchanganua hoja yake alisema Anaamini kunawezekana kufanyika kukuza vipaji vya watoto na kueleza kuwa Zamani mbona waliweza, kulikuwa na kizazi cha kina Pondamali na wenzake ambao walicheza mpira kwa muda mrefu kwa kuwa walianza wakiwa wadogo.

Aidha alieleza kuwa mafanikio yanayofanywa na vilabu vya mipira sasa hivi siyo mapya kwani yalishafanyika huko nyuma miaka ya 60 na 70 ila kwa sasa wachezaji wanaosajiliwa kwa ajili ya kupata mafanikio ya muda mfupi tu sasa na si uwekezaji wa muda mrefu.

"Viongozi wale wa Simba wale kina Mangara Tabu wameacha Legacy majengo yale miaka hiyo ya 70 watu wana majengo kama yale.

Yanga wamefika mpaka kuacha uwanja kwa miaka ile ule ulikuwa ni uwanja proper, hostel iko pale wachezaji wanakaa pale.

Sisi tuna nini? Tunajivunia nini, tunaacha legacy gani? Sisi kizazi chetu tuna nini Yanga, Simba tuna nini? Afadhali Azam timu ya mtu yaani sisi tunaacha legacy gani, Kufika Robo fanaili? Champions leage hata huko miaka ya 60 walifika.

69 Yanga imekwenda Semi final, robo fainal 72, imekwenda robo final 98.

Simba amefika mpaka nusu Fainali 74, kwa hiyo hakuna kitu ambacho huko nyuma hakikufanyika, hakipo":- Alisema Haji Manara,Tazama hapa alichosema
Back
Top Bottom