Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kuna upotoshaji mkubwa umefanywa na Manara ukishabikiwa na madalali wa kugawa bandari zetu kwa muarabu.
Kuweka kumbukumbu za kihistoria sawa hapa JF nitaweka ufafanuzi kumjibu Manara.
1. Bandari ya Dar imekuwepo karne nyingi sana kabla ya wavamizi wageni kutoka sehemu mbali mbali duniani kuja ukanda wa Afrika mashariki. Wageni wa mwanzo mwanzo kabisa walikuwa ni wareno ambao kihistoria walikuwa ni wajuzi wakubwa wa safari za masafa ya baharini, walitua na kuweka nanga ya meli zao kwenye ukanda wote wa pwani ya bahari ya hindi barani Afrika ikiwemo Dar na Mombasa, nao pia walikuta kuna bandari.
2. Wageni wote walikuja na kuikuta bandari ya Dar ikiwa pale na kuitumia au kuboresha ili kukidhi shughuli zao mbalimbali zikiwemo za kipepelezi, kivita, kidini na kibiashara.
3. Muarabu hakujenga bandari, bali aliirasimisha bandari ya Dar kuwa sehemu ya kufanyia biashara zake za kubebea watumwa, kutoroshea pembe za ndovu, vipusa na tunu mbalimbali za wazawa.
Bandari ya Dar haikuletwa na mtu yoyote na haikuanzishwa wala kujengwa na mvamizi yoyote bali iliporwa na wavamizi mbalimbali na kutumiwa kwa maslahi yao.