Manara amepotosha, Bandari ya Dar ilikuwepo siku zote, Mreno na Muarabu wameikuta

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Kuna upotoshaji mkubwa umefanywa na Manara ukishabikiwa na madalali wa kugawa bandari zetu kwa muarabu.

Kuweka kumbukumbu za kihistoria sawa hapa JF nitaweka ufafanuzi kumjibu Manara.

1. Bandari ya Dar imekuwepo karne nyingi sana kabla ya wavamizi wageni kutoka sehemu mbali mbali duniani kuja ukanda wa Afrika mashariki. Wageni wa mwanzo mwanzo kabisa walikuwa ni wareno ambao kihistoria walikuwa ni wajuzi wakubwa wa safari za masafa ya baharini, walitua na kuweka nanga ya meli zao kwenye ukanda wote wa pwani ya bahari ya hindi barani Afrika ikiwemo Dar na Mombasa, nao pia walikuta kuna bandari.

2. Wageni wote walikuja na kuikuta bandari ya Dar ikiwa pale na kuitumia au kuboresha ili kukidhi shughuli zao mbalimbali zikiwemo za kipepelezi, kivita, kidini na kibiashara.

3. Muarabu hakujenga bandari, bali aliirasimisha bandari ya Dar kuwa sehemu ya kufanyia biashara zake za kubebea watumwa, kutoroshea pembe za ndovu, vipusa na tunu mbalimbali za wazawa.


Bandari ya Dar haikuletwa na mtu yoyote na haikuanzishwa wala kujengwa na mvamizi yoyote bali iliporwa na wavamizi mbalimbali na kutumiwa kwa maslahi yao.
 
Manara ni chawa anaishi na waarabu pale kwenye jengo la GSM unafikiri atasema nini zaidi ya uchawa!
 
Huu mtindo wako kila comments zako ni "hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa" unafirahisha Sana..
 
Manara ni popo, si myama wala si ndege
Nakumbuka akiwa mdogo kabisa aliletwa kwa babu yake pale Mtaa wa Twiga ikidaiwa katoka Australia na baba yake😂😂

Tena Walikuwa Wawili sijui mwenzake aliishia wapi!!
 
Watu wasio na uonowala akili za kuwatosha kama Manara kuingia mjadala wa Bandari, eti ni ya waarabu, basi ujue tumwkwisha.
 
Eti bandari ilikuepo kabla ya wareno na waarabu, hao babu zako walikuwa wanajua nii Bandari? PUMBA TUPU.
 
Mohamed aliwahi kua boss wake Haji, sasa baada ya Haji kufukuzwa Simba na akaanza kumuita Mohamed eti mudi  na mwamedi hapo ndipo nilipo gundua kwamba Haji hana akili timamu...🤣
 
Ni Tanzania tu utakakutana na ujinga kama huu. Angalia timu za malumbano
Timu A: 1. Profesa Shivji. 2. Profesa Tibaijuka 3. Tundu Lissu 4. Dr Padre Kitima. 5. Dr Slaa. 6. Balozi Warioba 7. Chama cha wanasheria Tanzania
Timu B: 1. Haji Manara 2. Maulidi Kitenge 3. Zembwela 4. Musukuma Kasheku 5. Sheikh Mwaipopo
6. Kasim Majaliwa 3. Chama cha wasanii Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…