Manara anawaloga wachezaji wa Simba

Manara anawaloga wachezaji wa Simba

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Anawajengea hofu wachezaji kuwa waamuzi wanawaonea. Madhara yake atayaona hivi punde. Wachezaji wa Simba wana hofu nyingi zinazosumbua akili zao kama vile hofu ya kushindwa kuipokonya Yanga kombe, hofu ya kushindwa kubakia kileleni, hofu ya kufungwa na timu ndogo, hofu ya kuweza kukidhi matakwa ya usajiri wa mbwembwe na gharama, hofu ya kelele za Manara, kocha, viongozi, mdhamini na mashabiki, hofu ya kukamiwa na kuumizwa na sasa wameongezewa hofu ya kuonewa na marefa. Watachanganyikiwa. Hawahitaji kuwa na boss mwenye mambo ya vijiweni na mwenye kisebusebu cha kushinda kwa njia za mkato (vitisho, kulalamika, FIFA) kama Manara.

Manara sio taahila, katika level yake anapaswa kufahamu kuwa swala la marefa ni la dunia nzima, hata Ulaya na FIFA wanahangaika hadi leo kutaka kuboresha sekta ya maamuzi uwanjani bila mafanikio. Na hii inasababishwa na factors nyingi zikiwemo za human errors, kama binadamu refa pia ana timu zake anazozishabikia toka utotoni kabla hajakuwa kuwa refa, ana wachezaji anaowashabikia na uwepo wa vishawishi kutoka makampuni makubwa ya kubeti, n.k.
 
Aendelee hivyo hivyo ili Yanga ipete.
Kichaka chao Malinzi yupo Keko. Sasa watapata wapi justification ya kuonewa na waamuzi wakati Karia na Wambura wote ni Simba damu?
Ama kweli njia ya muongo ni fupi sana!
 
Mimi ni simba damu lakini huyu jamaa anakera sana. Nilifikiri baada ya Jerry Muro kuondolewa Yanga walau angetulia na kufanya mambo kwa weledi badala yake amekuwa anafanya mambo yale yale yasiyo na faida kwa Simba. Sidhani kupiga kelele sana ndio unakuwa mzalendo kwa Simba. Kwa mtu yeyote aliyewahi kucheza mpira anajua wazi kabisa ukianza kubishana na marefa hutaweza kucheza mpira wako kwa sababu unakuwa unacheza na timu mbili kwenye mechi moja. Moja inakuwa ni timu mnayopmbana nayo na ya pili unakuwa unaangalia marefa watakosea wapi ili uwatoe kasoro. Matokeo yake unapoteza umakini uwanjani. Timu ikiwa ipo vizuri hata refa akatae magoli nane nyie fungeni kumi mtatoka uwanjani na magoli mawili. Hata refa na mshika kibendera wakiwa wanaonyesha off side kila saa nyie mpangeni Ndemla atafunga kwa mashuti kutokea katikati ya uwanja halafu tuone refa kama atakataa. Viongozi wasipokuwa makini wakamfunga gavana huyu jamaa atawagharimu hao viongozi na simba yenyewe kwa ujumla.

Shida kubwa ya simba sasa hivi ni makosa madogo madogo katika kusajili. Wachezaji kama Juma luizio, Mavugona Gyan hawana hadhi kabisa ya kuchezea Simba. Lakini pia Omog naye ameshindwa kabisa katika kupanga wachezaji, sub pia zinamshinda na hata kubadili mbinu timu inapobanwa hawezi.

Na kama kuna kosa viongozi wa simba wamelifanya na hawajui ni kosa ni kumtimua Mayanja badala ya Omog. Mayanja ni bonge la mtaalam. Aliiwezesha simba kucheza mpira unaoeleweka na kupata ushindi akiwa na wachezaji wa kawaida kabisa sembuse leo tuna Okwi na Kichuya.
 
Unless hatujui, lakini Mayanja hakufukuzwa bali aliomba kuondoka. Mchango wa Mayanja bado ungefanya kazi unless Omog ana tatizo la kutokuelewana na msaidizi wake, sababu, superfiacially mayanja alikuwa na uhuru mkubwa wa kuendesha mambo kwenye kikosi.

Swali la pembeni. Kama tuko serious na tathmini ya coaches wa Tanzania, tunaionaje timu ya taifa:Taifa Stars yenye wachezaji hawa wa ligi kuu: Kichuya, Ajibu, Mzamiru, Yondani, Gadiel Michael, Nyoni etc. na wale wa nje: Samatta, Msuva n.k. tunamlinganisha vipi coach MAYANGA na hawa wa ligi kuu: Omog, Mayanja, Lwandamina, Pluijm etc. Whatever the result of comparison, Je, tuko fair tunavyo watathmini akina Omog? Kwa mfano, Mayanja anaweza kupewa nafasi Taifa Stars? Kiufundi tu nazungumzia. Kama YES Taifa Stars inaweza piga hatua nzuri zaidi? Kama ndiyo, then sifa zake ni za kweli, kama hapana, then tatizo la mpira Tanzania ni kubwa kuliko hawa makocha tulionao, pamoja na MAYANGA.
 
Back
Top Bottom