kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Anawajengea hofu wachezaji kuwa waamuzi wanawaonea. Madhara yake atayaona hivi punde. Wachezaji wa Simba wana hofu nyingi zinazosumbua akili zao kama vile hofu ya kushindwa kuipokonya Yanga kombe, hofu ya kushindwa kubakia kileleni, hofu ya kufungwa na timu ndogo, hofu ya kuweza kukidhi matakwa ya usajiri wa mbwembwe na gharama, hofu ya kelele za Manara, kocha, viongozi, mdhamini na mashabiki, hofu ya kukamiwa na kuumizwa na sasa wameongezewa hofu ya kuonewa na marefa. Watachanganyikiwa. Hawahitaji kuwa na boss mwenye mambo ya vijiweni na mwenye kisebusebu cha kushinda kwa njia za mkato (vitisho, kulalamika, FIFA) kama Manara.
Manara sio taahila, katika level yake anapaswa kufahamu kuwa swala la marefa ni la dunia nzima, hata Ulaya na FIFA wanahangaika hadi leo kutaka kuboresha sekta ya maamuzi uwanjani bila mafanikio. Na hii inasababishwa na factors nyingi zikiwemo za human errors, kama binadamu refa pia ana timu zake anazozishabikia toka utotoni kabla hajakuwa kuwa refa, ana wachezaji anaowashabikia na uwepo wa vishawishi kutoka makampuni makubwa ya kubeti, n.k.