3ZOV
JF-Expert Member
- Dec 28, 2020
- 6,259
- 7,015
Huyu manara alishawahi kuwa punda wa kuuza sembe huko South Africa. Huyu kijana ni tapeli,punda n.k
Kumbe mnamjua manara [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu manara alishawahi kuwa punda wa kuuza sembe huko South Africa. Huyu kijana ni tapeli,punda n.k
Kwa hii CV yake bado mnawalaumu Simba kumpumzisha kazi?
Shida ni kwamba tuliwaambia jamaa ni samjo ila wakawa awatuelewi
Umenunulia bei gani na Mudy?
Anaweza kuwa Kendazake Miaka 8 siyo Mchezo...Dah, last seen ya mleta mada ni 2013.
Hoja zake zijibiwe, wanaosema ni mwizi wa magari watoe taarifa polisi.KATIBU Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara, amejiuzulu wadhifa huo baada ya kuhusishwa na tuhuma za utapeli. Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kirumbe Ngenda, jana alilithibitishia gazeti hili kuwa wamekubali barua ya kujiuzulu kwa Manara iliyowasilishwa kwao juzi.
Manara aliyechaguliwa kushika wadhifa huo miaka miwili iliyopita, amekumbwa na kashfa ya kukodisha magari kwa watu mbalimbali yanayofikia 40, na kuyaweka rehani kwa watu mbalimbali Dar es Salaam na mikoa mingine nchini.
Anadaiwa kukodisha magari hayo kutoka katika kampuni tofauti za kukodisha magari nchini akitumia jina la CCM kwamba inayahitaji kwa kazi maalumu. Anadaiwa kuingia makubaliano ya kukodisha magari hayo kwa gharama ya Sh 60,000 kwa siku.
Tayari suala lake liko katika vyombo vya Dola baada ya wenye magari wanaotuhumiwa kutapeliwa na Katibu Mwenezi huyo kuwasilisha malalamiko yao kwa Polisi na sasa suala hilo linashughulikiwa na Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Lakini jana Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, alisema barua ya Manara ya kujiuzulu wadhifa wake imekubaliwa na suala lake linaachwa katika vyombo vya Dola vifanye kazi yake.
Ni kweli jana (juzi) Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, ilikutana na mbali na ajenda nyingine, ilikutana kupokea na kujadili barua ya Haji Manara ya kujiuzulu wadhifa wa Katibu Mwenezi.
Halmashauri Kuu ya Mkoa imekubali uamuzi wake wa kujiuzulu na haikutoa tamko lolote jingine, badala yake imeviachia vyombo vya Dola vifanye kazi yake kwa kuwa suala hilo limefikishwa huko, alisema Ngenda alipozungumza na gazeti hili kwa simu jana.
Alisema katika barua yake ya kujiuzulu, Manara amesisitiza kuwa hilo ni suala lake binafsi, na halina uhusiano na chama hicho, na atapata fursa ya kulielezea vizuri katika siku zijazo. Lakini kwa mujibu wa Ngenda, Manara amewaomba radhi wana-CCM wenzake, viongozi na wakereketwa wa chama hicho kutokana na namna suala hilo lilivyowasononesha, na kwamba amejiuzulu ili kukisafisha chama na kashfa hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa alisema kikao cha juzi chini ya Mwenyekiti wao, John Guninita hakikuwa na pingamizi na uamuzi wa Manara kwa sababu suala hilo linazungumzika. Kuhusu kama CCM ilikuwa na taarifa za utapeli unaodaiwa kufanywa na kiongozi wake, Ngenda alisema mmoja wa walalamikaji alifikisha suala hilo kwao na baada ya kuoneshwa nyaraka zilizokuwa na nembo za CCM, lakini zikagundulika ni za kughushi, walimshauri aende katika vyombo vya Dola.
Sisi ndio tuliomshauri aende katika vyombo vya Dola baada ya kumueleza kuwa CCM haihusiki na suala hilo na hata nembo zilizotumika, zimeonekana ni za kughushi.
Kwa hiyo, hatukuficha kitu na ndio maana tulimpa ushirikiano mhusika kwa sababu sisi sio chama cha kuficha madhambi, alisema.
Aidha, alisema kwa ujumla CCM ni chama cha binadamu, na akafananisha na familia inayoweza kuzaa watoto ambao miongoni mwao wakawemo mchungaji, shehe au mwizi; kwa hiyo, lililomkuta Manara linaangukia humo, ingawa alisisitiza, ni Mahakama pekee inayoweza kusema kada huyo ni mkosaji.
Haya yanatokea kwa sababu chama ni cha binadamu, sisi kama taasisi tuna watu wa aina mbalimbali, lakini la msingi ni kuzingatia maadili na miiko ya uongozi, na huo ndio mwito wetu kwa wana-CCM wengine.
Tuzingatie maadili ya uongozi, alisema Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam. Manara hakupatikana jana kuzungumzia hatima yake baada ya kujiuzulu, lakini kijana huyo machachari alieleza wiki iliyopita anapanga kulizungumzia atakapozungumza na wanahabari.
Hoja zake zijibiwe, wanaosema ni mwizi wa magari watoe taarifa polisi.
Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Kumbe bwana mdogo[emoji23][emoji23]Enzi hizo nipo darasa la 7
Sahiv ninandevu na sina kazi nipo home wale mabro niliowaona hawana ramani enzi hizo Sasa hiv na mimi nimekua Kama waoKumbe bwana mdogo[emoji23][emoji23]
Umekutaje humo ndani ya kaburi ?Tunafukua makaburi[emoji28][emoji28]
Zamani RTD kulikua na kipindi kinaitwa "Kutoka Magazetini"Umekutaje humo ndani ya kaburi ?
inaonesha huyu mwamba haozi humo
Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
"Mzungu" ana heka -heka sana!KATIBU Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara, amejiuzulu wadhifa huo baada ya kuhusishwa na tuhuma za utapeli. Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kirumbe Ngenda, jana alilithibitishia gazeti hili kuwa wamekubali barua ya kujiuzulu kwa Manara iliyowasilishwa kwao juzi.