Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Mchezo ambao utapigwa siku ya Jumanne tarehe 23 Februari 2021 umebeba kauli mbiu ya 'TOTAL WAR , POINT OF NO RETURN' .
Msemaji wa Klabu hiyo Haji manara amesema kuwa Simba ina historia nzuri ya kushinda inapokuatana na Al ahly katika Ardhi ya Tanzania.
Mara zote Al ahly ilipocheza na Simba ardhi ya Tanzania ilifungwa na mara ya mwisho ni mwaka 2019 katika hatua ya makundi ambapo ushindi wa 1-0 katika uwanja wa Mkapa uliivusha Simba kwenda hatua ya robo fainali katika michuano hiyo.
Manara amesisitiza kuwa wanao uwezo wa kuwafunga tena licha ya kukiri kuwa Al ahly ni timu kubwa kwa upande wa kikosi, vikombe na hata historia, ameongeza kuwa Simba hupenda mechi kubwa kama hizo.
Vilevile amesema kuwa tageti yao ya chini ni kufika nusu fainali ya michuano hiyo.
"Ni vita ya nje na ndani ya uwanja lazima tupate point 3. Wachezaji wanaenda kucheza kuwakilisha Simba, Tanzania na ukanda wote wa Afrika Mashariki" . Alisema Manara.