Manara: Ni vita ndani na nje ya uwanja lazima tupate point 3

Manara: Ni vita ndani na nje ya uwanja lazima tupate point 3

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105
20210219_171414.jpg
Kuelekea mchezo wa Klabu bingwa barani Afrika wa Simba dhidi ya Al ahly ya Misri, Simba imeitisha mkutano na waandishi wa habari kuelezea maandilizi kuelekea mchezo huo.

Mchezo ambao utapigwa siku ya Jumanne tarehe 23 Februari 2021 umebeba kauli mbiu ya 'TOTAL WAR , POINT OF NO RETURN' .

Msemaji wa Klabu hiyo Haji manara amesema kuwa Simba ina historia nzuri ya kushinda inapokuatana na Al ahly katika Ardhi ya Tanzania.

Mara zote Al ahly ilipocheza na Simba ardhi ya Tanzania ilifungwa na mara ya mwisho ni mwaka 2019 katika hatua ya makundi ambapo ushindi wa 1-0 katika uwanja wa Mkapa uliivusha Simba kwenda hatua ya robo fainali katika michuano hiyo.

Manara amesisitiza kuwa wanao uwezo wa kuwafunga tena licha ya kukiri kuwa Al ahly ni timu kubwa kwa upande wa kikosi, vikombe na hata historia, ameongeza kuwa Simba hupenda mechi kubwa kama hizo.

Vilevile amesema kuwa tageti yao ya chini ni kufika nusu fainali ya michuano hiyo.

"Ni vita ya nje na ndani ya uwanja lazima tupate point 3. Wachezaji wanaenda kucheza kuwakilisha Simba, Tanzania na ukanda wote wa Afrika Mashariki" . Alisema Manara.
 
Simba tujiandae kisaikolojia na matokeo ya mechi ijayo, iwe wazi kuwa mende hawezi kuangusha kabati.
 
Simba atasumbua sana kwenye hii game ila wasiwasi wangu upo kwenye finishing kule mbele basi.
 
Kwaiyo kesho Yanga wakifungwa watajitoa kwenye ligi?
 
Ndiyo maana Jerry Muro alimwambia Manara kuwa ni kihirizi cha simba maana wenzake wote aliokuwa nao wameondoka yeye kang,ang’na tu wala habanduki
 
Lesson 3: Numbers (1-10)
واحد wahed. one.
اثنين ethnein. two.
ثلاثة thalatha. three.
أربعة arba-a. four.
خمسة khamsa. five.
ستة sitta. six.
سبعة sab-a. seven.
ثمانية thamanya. eight.
Tutaanza kuhesabu leo vizuri saa kumi jion, karibu darasani
 
Back
Top Bottom