Manchester United (Red Devils) | Special Thread
We acha tu, naona tumeamshwa!..loh,hawa Spurs mmh!

Mzima lakini BJ? naona mmeanza vibaya leo na SAF anatafuna Big G yake kama ugomvi ha ha ha ha lakini mpira ni dakika 90 na bado kuna dakika kibao. Chelsea wanaendelea na 100% perfect record yao baada ya Malouda kuziona nyavu za Stoke dakika za majeruhi (93rd minute)
 
wajameni marefa hawajaacha tu kuwapendelea Man U? Penalti kabisa pale jamaa kaachiwa apete tu!
 
Spurs wasiposhinda leo kesho mitaa hakukaliki kwa mashabiki wa Arsenal naomba mungu manu afungwe au matokeo yaendelee hivi hivi...
 
Mzima lakini BJ? naona mmeanza vibaya leo na SAF anatafuna Big G yake kama ugomvi ha ha ha ha lakini mpira ni dakika 90 na bado kuna dakika kibao. Chelsea wanaendelea na 100% perfect record yao baada ya Malouda kuziona nyavu za Stoke dakika za majeruhi (93rd minute)

Salama BAK,niaje wewe?!..we acha tu, angalau tupo droo mpaka sasa..huyo SAF kwa kutafuna ana rekodi mana hadi taya zimezoea..tusikilizie full-time itakuwaje!
Poleni kwa kipigo from Spurs, hao Chelsea naona hawataki utani..Ila kama kawaida Man U ndo vinara wenyewe, ha ha
 
Naona kijana Anderson leo kajipatia bao lake la kwanza hii ni mechi ya baraka sana kwa Man U. I hope dogo amefungulia sasa na ataanza kupiga mabao. Game tumelikamata lazima hawa madogo wapigwe 4 au 5.
 
siamini kwamba Man U wako kumi uwanjani...aisee

Hawa watoto tunavyowamiliki utadhani tuko 11, kweli bingwa bingwa tuu. Na msimu wa Spurs ndio umeisha leo officially.
 
Back
Top Bottom