Mandamano yaitishwe nchi nzima kushinikiza kupatikana katiba mpya ili kudhibiti mafisadi wa CCM. Vinginevyo tukisubiri baada 2025 tutaumia

Mandamano yaitishwe nchi nzima kushinikiza kupatikana katiba mpya ili kudhibiti mafisadi wa CCM. Vinginevyo tukisubiri baada 2025 tutaumia

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Bila kuwa na katiba itayodhibiti wizi na utoroshaji wa mali za umma. Tunakwenda kuumia. Maana hii miaka mitatu mpaka uchaguzi mkuu ufanyike tutaibiwa sana.

Mandamano yaitishwe nchi nzima bila kujali itikadi zetu.

Tupate katiba ambayo hata Rais au waziri akifanya ufisadi anafikishwa mahakamani bila kinga.

Ikiwezekana anyongwe hadharani.
 
Katiba mpya ni Sasa. Kwanini tusubiri? Katiba mpya itamnufaisha kila mmoja, hata hao wanaoipinga.
 
Kwanini katiba ya kudhibiti mifumo inakataliwa????. Wanaokataa wanataka wizi uendeleee? Kwani wao ni wezi???. Wanataka ushahidi gani kwamba mfumo/ katiba inachochea wizi na ukatili/ udikteta???. Mbona Nyerere alikiri kuwa mfumo unaruhusu hayo!!. Mbona ripoti za CAG zinaonesha hayo. Mbona Mkapa alikiri kwenye kitabu chake pia???. Mm sielewi kwa nini tukatae kuweka mfumo mpya wa kudhibiti uharifu!!!
 
Mtz hawezi kuandamana labda umlipe, hata ukimlipa hato andamana ni vigeu geu sana ss
 
kusanya familia yako nenda kaandamane mnawaza mambo ya kijinga mnaacha kufanya kazi familia zile mm ni MTanzania na Rais wangu ni Samia kaandamane na mwenyewe
 
Haimdhibiti Rais hata akifanya makosa hivyo wateule wa Rais wakiiba anao uwezo wa kuwalinda. Rais ana uwezo wa kumkata za DPP kuendelea na kesi.
Chadema Kuna wizi mkubwa, hasa fedha za michango ya wabunge na ruzuku
 
Nyie chadema sijui mna Akili gani...hivi Kenya SI Wana katiba mpya na nzuri kushinda yetu?mbona ufisadi ni mkubwa kushinda wetu?...katiba is just a piece of papers...na mwanadamu ndo anaiongoza hivyo lolote linaweza kutoka...
NB: ni wajinga tu ndo wanaamini KATIBA ndo suluhisho la matatizo yetu
 
Alipokuwepo magufuli mliwaachia chadema wapiganie katiba mpya, Leo mpendwa wenu hayupo ndio mnatambua hili??.
 
Bila kuwa na katiba itayodhibiti wizi na utoroshaji wa mali za umma. Tunakwenda kuumia. Maana hii miaka mitatu mpaka uchaguzi mkuu ufanyike tutaibiwa sana.

Mandamano yaitishwe nchi nzima bila kujali itikadi zetu.

Tupate katiba ambayo hata Rais au waziri akifanya ufisadi anafikishwa mahakamani bila kinga.

Ikiwezekana anyongwe hadharani.
Umeandika ujinga uliopuuzwa na wajinga wenzako. Naona kila mtu anapambania nafasi ya uchawa. Vijana mmekimbia shule na kujiunga na uwanaharakati msiofahamu faida na hasara zake huko vijijini kwenu.

images (68).jpeg
 
Suala la katiba mmeliweka kisiasa sana ndio maana halitafanikiwa. Huwezi kumwambia mtanzania wa kawaida aingie barabarabi kuadai katiba asiyojua itamsaidia nini. Mngeweka jitihada kuwaelekeza watanzania umuhimu wa katiba mpya washawishike akilini haswaaa, vinginevyo mtaidai kwenye mitandao hadi mtazeeka. Kila post mnayoweka mngekuwa mnataja udhaifu wa katiba ya sasa na kuweka maboresho yake kwenye katiba mpya
 
Nyie chadema sijui mna Akili gani...hivi Kenya SI Wana katiba mpya na nzuri kushinda yetu?mbona ufisadi ni mkubwa kushinda wetu?...katiba is just a piece of papers...na mwanadamu ndo anaiongoza hivyo lolote linaweza kutoka...
NB: ni wajinga tu ndo wanaamini KATIBA ndo suluhisho la matatizo yetu
Mleta mada kaamua kuwa chawa wa wale wanaotaka kupiga hela kupitia vikao hivyo vya katiba. Ndio maana wenye akili wameupuuza uzi wake.
 
Katiba mpya ilianzia chadema, baadae chadema wakauza hili wazo kwa mama, sasa hivi muda si mrefu katiba mpya itakuwa ajenda ya CCM.
 
Back
Top Bottom