Bila kuwa na katiba itayodhibiti wizi na utoroshaji wa mali za umma. Tunakwenda kuumia. Maana hii miaka mitatu mpaka uchaguzi mkuu ufanyike tutaibiwa sana.
Mandamano yaitishwe nchi nzima bila kujali itikadi zetu.
Tupate katiba ambayo hata Rais au waziri akifanya ufisadi anafikishwa mahakamani bila kinga.
Ikiwezekana anyongwe hadharani.
Suala la wizi na Ufisadi ni Hulka na sifa za mt ,haitokani na uwepo wa katiba Mpya kamwe.
Kinachoonesha ni kwamba watanzania wengi wanasilka ya WIZI, na kwa muktadha huu Taifa hili litandelea kudidimia.
Hata kama tutaweka Katiba Mpya ,bado Mwanya ukipatikana ,wizi utaendelea.
Enzi za Miaka ile ya 60's na 70's ,viongozi wetu wengi walikuwa wazalendo na hawakua wizi. Kwa sababu hawakuwa na silka hizo, na kiukweli walikuwa masikini sana kuliko sisi leo.
Nakumbuka Wabunge walikuwa wanapanda Basi la KAMATA kwenda DODOMA Bungeni, wakifika wanapeleka ticket zao nakurudushiwa nauli.
Leo Kila Mbunge ana Pajero na Milioni 12, za mshahara mbali 10 za jimbo..
Mimi nadhani
Tutumieni sheria ya Kiislamu kuwadhibiti WEZI na
Mafisadi.
MWIZI AKATWE MKONO, MZINIFU APIGWE MAWE, MBAKAJI ATUPWE KWENYE GEMA LA MLIMA NK.
Walevi wachapwe bakora.
Kiukweli uzinzi na Ulevi ndivyo vinachangia wizi.