Mandi/Biriani ni mchele wa wapi huu?

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Wakuu habari za jumapili.

Naomba kuuliza.

Juzi ijumaa nilikua mjini kati Dar es salaam, nikakutana na jamaa yangu mmoja mwenye asili ya kiarabu niliesoma nae elimu ya sekondari ya juu ambae miaka mingi hatujaonana, tukazungumza kidogo na kwa kua ilikua muda wa chakula tukaona tupate chakula, akanipeleka kwenye mgahawa mmoja wa wasomali.

Hapo akaagiza chakula inaitwa mandi kama sijakosea. Ikaja hiyo mandi akaniambia ni kama biriani.

Mimi hizo vyakula sio mzoefu kabisa, nimezoea ugali na nyama, samaki, wali nyama au samaki au ndizi nyama.

Chakula kilipokuja ni kitam kweli kweli ila wakati tunakula nikawa najiuliza huu mchele uliotumika kupika ni mbegu za wapi maana punje ya mchele ni ndefu kuliko punje nilizozizoea miaka nenda rudi, huu wali wa rangi rangi unaonekana ni wa tofauti. Sasa ili nisionekane mshamba sana sikuuliza pale mgahawani. Nimekuja kwenu wadau kuuliza, ule mchele ni mbegu za wapi?

Maana ukubwa wa zile punje sio wa kawaida. Ni aina nyingine ya mchele? Kama tulivyo na kuku wa kisasa na kienyeji, je ule ni mchele wa kisasa?

Ahsanteni na mtanisamehe kwa ushamba wangu.
 
Subir wajuviwaje ila zenji nimeukuta sana huu mchele nikiwa nakula pilau nyama ni hatari sana aisee
 
Subir wajuviwaje ila zenji nimeukuta sana huu mchele nikiwa nakula pilau nyama ni hatari sana aisee
Basmat ni michele ya pakistan malysia india.
Mandi ni kama kula wali kwa supu ila ile ni supu ya kondoo au mbuzi inatengenezwa mild yaani sio mchuzi wala sio supu yataka kufanana na mchuzi chukuchuku wetu ila sisi tume focus kwa ukali/uchachu wao wasomali kwa ladha flavor na texture ya mchuzi wenyewe yeah ni mtamu sana ule wali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee,sijakuelewa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa Mandi ilianza huko Hadhramaut Yemen na huko ndio asili ya dishi hili
Halafu ikasambaa mpaka Somalia, Saudia, na kuvuka kabisa mpaka india na Pakistan

Na mchele wanaotumia ni Basmati long grain
Ili kupata ladha ya Mandi upishi wake lazima utumie wanyama wadogo sio waliokomaa
Yaani baby lambs au wengine kama ni ngamia au ng'ombe basi wawe wadogo bado, ili unapomeza inatereza tu
Upishi wake pia kwa kuongeza utamu ni spices zinazotumika
Hapo ndio Utamu wa mandi unakamilika

Sent from my SM using Tapatalk
 
MANDI raha yake ipakuliwe kwenye SINIA kubwa.

Halafu muwe wengi mnalizunguka SINIA.

Ukimaliza shushia na MTINDI ule wenyewe, sio wa kuchakachua.

Nakuambia ni hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…