The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Wakuu habari za jumapili.
Naomba kuuliza.
Juzi ijumaa nilikua mjini kati Dar es salaam, nikakutana na jamaa yangu mmoja mwenye asili ya kiarabu niliesoma nae elimu ya sekondari ya juu ambae miaka mingi hatujaonana, tukazungumza kidogo na kwa kua ilikua muda wa chakula tukaona tupate chakula, akanipeleka kwenye mgahawa mmoja wa wasomali.
Hapo akaagiza chakula inaitwa mandi kama sijakosea. Ikaja hiyo mandi akaniambia ni kama biriani.
Mimi hizo vyakula sio mzoefu kabisa, nimezoea ugali na nyama, samaki, wali nyama au samaki au ndizi nyama.
Chakula kilipokuja ni kitam kweli kweli ila wakati tunakula nikawa najiuliza huu mchele uliotumika kupika ni mbegu za wapi maana punje ya mchele ni ndefu kuliko punje nilizozizoea miaka nenda rudi, huu wali wa rangi rangi unaonekana ni wa tofauti. Sasa ili nisionekane mshamba sana sikuuliza pale mgahawani. Nimekuja kwenu wadau kuuliza, ule mchele ni mbegu za wapi?
Maana ukubwa wa zile punje sio wa kawaida. Ni aina nyingine ya mchele? Kama tulivyo na kuku wa kisasa na kienyeji, je ule ni mchele wa kisasa?
Ahsanteni na mtanisamehe kwa ushamba wangu.