[emoji1241]Atumie nafasi hiyo vizuri kuji brand huko Kenya[emoji1139]
[emoji1241] Wasanii wengi wa Tanzania wametajirika kwa supporter ya wa Kenya kupenda vitu wavifanyavyo .
[emoji1139]Wakenya wengi wanafuatilia Sana na wanapenda Sanaa na vituko vya Tanzania na hii inasababisha na kuifahamu kuongea vizuri lugha ya kiswahili, Sasa inakuwa rahisi kuzitumia kama Sanaa,Kenya wao wamechanganya kiasi Fulani Kiingereza na kiasi Fulani lugha zao za asili hivyo wanakosa ule mkong'osio wa Lugha.
[emoji1241] Msanii anaweza kuwa amefulia kabisa huku Tanzania au mnamwona wa kawaida kabisa lakini kule Kenya akienda anapokelewa kama mfalme, mfano akina Mr. Nice, Roze Mhando, Amorapa nk.
Hata nyimbo zilizokwisha kupitwa na wakati huku Tanzania kule ndio kwanzaaa Zina hiti kwenye top 10. Hata nyimbo za dini kama gospel na za kikatoliki zilizovuma zamani bongo kwao ndio asubuhi.
Mandonga Mtu kazi, Atumie vizuri kipaji chake Cha kuongea kupiga mkwara mbuzi wapinzani wake, akijipanga vizuri Wakenya wanapenda Sana maneno ni burudani kwao na nadhani hata kumwalila wamefuatilia Tambo zake.
Akijipanga vyema atakuwa anapaya mikataba mingi Sana Kenya ya promotion na madoko. Kila la heri Mandonga mtu kazi, ndoige usiyechagua pa kuupigania au mpinzani wako