Mandonga apigwe stop kupanda ulingoni

Mandonga apigwe stop kupanda ulingoni

Watamuua, nakubaliana na mleta Uzi. Ngumi Ni mchezo usiohitaji mzaa
 
Huwezi kupigana mapambano matatu ndani ya mwezi mmoja hata kama ni ya kirafiki ngumi sio kama soka au riadha.. jamaa anatafuta umaarufu sana kuna siku itaokotwa maiti ulingoni
Anacheza na nyota. Atasahaulika karibuni sasa inabidi atumie umaarufu wake kwa ipasavyo kabla haujaisha.Nadhani by Dec 2022 atakuwa amefutika katika ramani kama Dr Shika
 
Nafikiri sasa ni muda muafaka cha chama kinachosimamia mchezo wa ngumi kumzuia Mandonga kupanda ulingoni.

Kwanza huyu jamaa anahatarisha usalama wake, ngumi sio mchezo wa kupanda panda ulingoni kila mwezi.

Pili anaudhalilisha huu mchezo, inaonekana ni kama anafanya comedy.

Tunajua anatafuta ugali wa familia, lakini miiko ya mchezo husika lazima izingatiwe.
Nadhani anachokitafuta atakipata
 
Back
Top Bottom