Maneno gani ya dharua uliambiwa yakakuumiza sana

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
21,952
Reaction score
43,265
Mimi aliniomba 100K aongeze kwenye kodi wakati me mwenyewe kodi jau enzi za chuo hizo nikamwambia asubiri nipate boom. Akasema mwanaume wa kutegemea boom nae mwanaume sasa[emoji24][emoji24][emoji24]

Kitu gani cha dharau alichowahi kukwambia babe wako alipokuomba hela ukasema huna?
 
kuna mzee mmoja alikua hataki nisitembee na binti yake.Sasa cku moja alinifata kijiweni mbele ya washkaji ngoja ni mnukuu "ctaki ufala wako kwangu unataka mwanangu aje azae mtoto ana mashavu kama mtungi" nilijickia vibaya sana kwa kudhalilishwa kule mbele ya watu nikajiondokea kwenda gheto kujiangalia kwenye kioo hayo mashavu kama mtungi lakin cku yaona.

Ila mapenz ndo kama aliyachochea binti alidata kupita maelezo.
 
Kulikuwa na shida ya maji mkoa mzima.so maji yakiwa ya kununua dumu mia tano hapo zamani.visima vikiwa adimu
My sister alikua sekondari sasa akirudi inabidi akatafute maji japo ndoo kubwa moja kwa kufulia uniform na anabakisha ndoo ndogo moja ya kuosha asubuhi .siku hiyo akakosa hata maji ya kisima.kuna ndugu mmoja alinunua maji sababu alikua na ajira.alipopata maji ya kuoga akataka kuyamwaga yaliyobaki.Dada akamuwahi "kaka flani usimwage hayo maji kama huyataki nayaomba"

Yule kaka akamwangalia kwa dharau akamjibu "haya maji si bora niyamwage au nimpe mbwa kuliko wewe"
Halafu Ilikua mbele ya member wengine wa familia mchanganyiko..


Sasa hivi huyo aliejibu kwa dharau anapuyanga huko vijijini mlevi hafai.huyo mdada yuko mjini na maisha yake kayapata.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kama nauona mtungi wa Bibi yangu kule Moshi,jameni so mliishia wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…