Nakumbuka mwaka 2014 mwanzoni nilienda kufanya interview pale ukonga. Interview ilikua ni ya Jeshi la Zimamoto. Sasa sisi tulikua wengi sana hivyo ili zoezi liende kasi ilibidi wao mainterviewer wajigawe kwenye magroup matatu mule bwaloni.
Ilipofika zamu yangu niliingia na nikaangukia kwenye meza moja yenye wasaili watatu akiwepo mmama mmoja hivi mtu mzima na miwani yake.
Akaniambia nikae. Baada ya kuka akaamza kuniuliza jin langu nani, naishi wapi na shughuli yangu kwa wakati ule ilikua ni nini. Baada ya kumjibu hivyo, ilionekana kama namdanganya (nahisi alinifananisha na mtu mwingine) , na nilipojitetea zaidi akanambia kwa ukali, "shika vyeti vyako uondoke kwanza mdomo wako unanuka"
Kwakweli iliniuma sana hasa ukizingatia nilitokea mwanza kwa ajili ya hiyo interview.
Nilichojifunza baada ya miezi kadhaa ni kutolalamika sana kwani kila kitu kina sababu na Mungu mwenyewe ndie ajuae. Nadhani nilipo hapa ni pazuri zaidi kuliko nafasi niliyokua naitafuta Zimamoto.