Maneno haya ya Kikwete kwa Rais Samia yana ujumbe mzito mno

Maneno haya ya Kikwete kwa Rais Samia yana ujumbe mzito mno

Katika hotuba yake kwenye mazishi ya JPM, Jakaya alisema:

"Mimi na wenzangu tuko na wewe. Tutume tutaitika. Usipotutuma tutaendelea na mambo yetu"- JK

My Take: wenzake kina nani? Mambo yao yepi?
Na wastaafu wenzake
 
Wenzake wastafu, kama akina Malechela, Pinda na wengine wastafu wenzie. Wataendelea na mambo yao wanayoyafanya sasa hivi, kama kulima mananasi, mahindi. Au unawafanyia wewe mambo yao?. Mbona simple tu...! Nyie ndio mnaoifanya dunia iwe ngumu kukalika nyie, kila neno la mtu unaanza kulitafutia tafsiri yako. Utachelewa
 
Waswahili wanajuana kwa vilemba hao, hamna jipya JK atamfumba ama kumpatia shida Mama yetu. Time is about to tell it.
 
Sijajua kwann TZ bongo movie haifanyi vizuri. Watunzi ni wengi sana.
Mtu anaweza kupaliwa tu na maji ikatungwa movie kuwa yale maji si ya kawaida, pale freemason walituma secret agency wao wamuondoe bla bla bla.
 
Wenzake ni Viongozi Wakuu wa staafu: Marais, Makamu Rais, Waziri Wakuu, Maspika, Majaji Wakuu etc ambao hata Magufuli alikuwa anawatumia wakati mwingine wamwakilishe katika baadhi ya matukio na si jambo jipya.

Kuhusu kuendelea na mambo yao ni kama vile alivyosema wakati Samia anatangaza kifo cha JPM yeye alikuwa anapiga soga na wazee wenzake wa kijijini. Hilo ni miongoni mwa mambo yake, pamoja na kilimo na ufugaji mdogo anaofanya.
 
Mjanja wa mjini anataka amuingize kenge Mama Samia. Magu alikuwa amewabana mbavu, ingawa hawasemi lakini inawezekana timu JK imefurahi kwa kuondoka MAGU.
Kuna kipindi watu walijaribu kuwashwa washwa wakapigwa spana, sasa ruksaa kuwashwa washwa.
giphy.gif
 
Mjanja wa mjini anataka amuingize kenge Mama Samia. Magu alikuwa amewabana mbavu, ingawa hawasemi lakini inawezekana timu JK imefurahi kwa kuondoka MAGU.
Waliobanwa mbavu ni wastaafu mafao yao, watumishi wa umma ambao hawajawahi kupandishiwa mishahara, wakulima wa korosho, wafanyabiashara wadogo waliolazimishwa vitambulisho vya elfu 20, wafanyabishara wakubwa ma wadogo waliofunga biashara kwa kodi za makadirio makubwa, waliookotwa kwenye viroba n.k kwa uchache tu hawa ndio waliobanwa mbavu
 
Wenzake ni Viongozi Wakuu wa staafu: Marais, Makamu Rais, Waziri Wakuu, Maspika, Majaji Wakuu etc ambao hata Magufuli alikuwa anawatumia wakati mwingine wamwakilishe katika baadhi ya matukio na si jambo jipya.

Kuhusu kuendelea na mambo yao ni kama vile alivyosema wakati Samia anatangaza kifo cha JPM yeye alikuwa anapiga soga na wazee wenzake wa kijijini. Hilo ni miongoni mwa mambo yake, pamoja na kilimo na ufugaji mdogo anaofanya.
Vema
 
JK hatuwezi kuacha kupata ushauri kwake kabisa maana amtumikia nchi hii kwa miaka 10 mfululizo hivyo kuna mambo anayafahamu na ushauri wake waweza kufaa sana.

Uzuri ni kuwa kwa wastani hata matatizo!
 
Katika hotuba yake kwenye mazishi ya JPM, Jakaya alisema:

"Mimi na wenzangu tuko na wewe. Tutume tutaitika. Usipotutuma tutaendelea na mambo yetu"- JK

My Take: wenzake kina nani? Mambo yao yepi?
Sio kazi yako kujua.
 
Back
Top Bottom