Maneno maarufu secondary za bweni

Maneno maarufu secondary za bweni

Kuvunja mifupa~ siku ya disco sketi ya shule inapigwa bonge la hemming iwe kimino. Afu itafumuliwa baadae maanke uniform lazm iwe chini ya goti. Kitendo cha kuifupisha kwa muda ndo kuivunjisha mifupa.
Cc Madame B, nahisi unahusika sana.

Mndele umenikumbusha mbali saaana.
Nakumbuka tuliwaalika Boys shuleni kwetu kwa ajili ya kuja kucheza na sisi Girls disco.
Mh!
Yaliyoendelea siri yetu.
 
Last edited by a moderator:
Njuka - Form one
Nyumbu wa kiangazi - form five
Madungulushi - vyakula kutoka home
Machale - akari polisi
Panya - spy wa walimu
Trees - nyama
Nyali - wali
madoa - wasichana wanaotoka shule jirani kuja disco
anasa - maandazi
Dah! Mbali sana, enzi hiyo akikatisha demu hapo skuli basi ni miluzi tupu na watu kutoroka madarasani hata kama kuna mwalimu.
 
Kayamba = Bakuli kubwa lenye kuchukua chakula kingi
Horizontal = Kusoma ukiwa umelala kitandani
Kuzamia = Kuingia kwenye sherehe pasipo mwaliko rasmi
Passport size = Kunawa nusu ya mwili ili kuepuka kuoga


watu8 um3n1kumbush4 mb4l1 s4n4....
 
Last edited by a moderator:
Boy = Mwanafunzi mnaetokea mkoa mmoja
Ng'ande = Kande
Kitei = Wali
Sumu = Uji wa dona
Vitufti/ Mapisi = Mjumuiko wa vitafunwa kama mandazi, bagia, half cakes....
Mtego = mwanamke mrembo, tv au filamu.
Chui = Ugali wa dona
Umenikumbusha mbali kugombania tuftiii......ha ha ha ha ha haaaaaaa
 
Back
Top Bottom