SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
Wataalamu wa lugha husema kwamba lugha ni kitu hai; hukua na kufa. Lugha kadhaa hapa duniani zilikua kisha zikafa mazima, kama kilatini, sanskrit n.k. Sijui jinsi lugha zinavyokufa mazima ila najua jinsi maneno ya lugha fulani yanavyobadili maana.
Pengine huku kubadili maana ndio kukua kwenyewe. Kama ni hivyo, huenda maneno haya ya Kiingereza hapa Tanzania ni ishara kwamba Kiingereza kinapanuliwa hapa nchini.
Maneno ya Kiingereza yanayotumika kwa maana tofauti kabisa hapa nchini ni matatu: local, booking na personality. Tuanze kuyatezama moja moja, maana halisi na jinsi maana ilivyobadilishwa hapa nchini.
1. Local
Neno hili ni kivumishi (adjective) kuelezea kitu cha mahali fulani chenye asili yake hapohapo. Kwa hiyo unapata misemo kama local food = chakula cha eneo hilo, local drinks = vinywaji vya eneo fulani nk.
Local inavyotumika Tanzania
Neno local hutumiwa na watanzania wengi kumaanisha kitu cha ovyoovyo cha kudharaulika. Utasikia wakisema: "Mambo yake ni ya kilocal sana =Mambo yake ya ovyo sana. Kama mtu hajavaa vizuri utasikia: Kavaa kilocal sana huyo!
2. Booking
Hili ni neno linalotumika sana kwenye usafiri likiwa na maana ya kununua tiketi ya usafiri siku kadhaa kabla ya kuanza safari ili kujihakikishia usafiri. Kwa wenzetu kuna ofisi maalumu ya kuuza tikiti kwa wale wanaotaka kusafiri siku za mbeleni. Ofisi hiyo huitwa booking office.
Booking office inavyotumika Tanzania
Niligundua maana ya kitanzania ya booking office nilipofika stendi ya bus na mzigo wa ndizi. "Mzee," waliniambia vijana. "Kwa kuwa gari yako itaondoka mchana, weka huu mzigo booking office." Nikajua kumbe sehemu ya kuhifadhi mzigo kibongobongo huitwa booking.
3. Personality.
Hili ni neno linalotumiwa sana na wanasaikolojia kuzungumzia hali na tabia za watu katika mazingira tofauti.Mathlan, mwanaume akinywa pombe kisha akatokea msichana mrembo mbele yake huyo mwanaume atabadilika? Kubadilika kwa huyo mwanaume na tabia atakayoonesha ndiyo personality yake.
Personality inavyotumika kibongobongo
Mwanaume mrefu mnene aliyevalia suti na kupendeza eti huyo ndiye husemwa ana personality. Utasikia sana: Aisee Mkurugenzi wa ..........ana personality huyo! Kibongobongo msukuma mkokoteni hana personality ni wakubwa tu!