Maneno matatu ya Kiingereza yaliyobadilishwa maana yake hapa Tanzania

Maneno matatu ya Kiingereza yaliyobadilishwa maana yake hapa Tanzania

Kwenye language inaitwa 'meaning shift' haina shida hata english yenyewe kuna maneno yamebadilika maana baada ya kipindi flan, pia hao wanatumia katika kiswahili na sio kiingereza
 
1. Local

Neno hili ni kivumishi (adjective) kuelezea kitu cha mahali fulani chenye asili yake hapohapo. Kwa hiyo unapata misemo kama local food = chakula cha eneo hilo, local drinks = vinywaji vya eneo fulani nk.
Neno local hata wenyewe wanalitumia hivyo hivyo though hawamaanishi ovyo ovyo bali huwa linabeba less value ya kitu unachozungumzia
 
Kwenye booking mzee hakukosea kwani alikueleza kuwa ukauweke sehemu ya booking than gari ikija utaondoka, nadhani hakukuwa na goods shade.
 
Democracy
Is the government of the people by the people and for the people themselves.

Democracy inavyotumika tanzania sasa.
Tanzania wanataka demokrasia ya kila mtu kufanya anachotaka tu bila kujali kuna sheria
 
Bora sie kuliko hao wanaigeria,maana wao wana maneno ambayo wanayatumia kama maneno ya kiingereza ila ajabu hayo maneno hayapo kwenye kiingereza.
 
Nilizinguana na jamaa wa wrong parking enforcement mwisho wa siku akaniambia, "Take your time".

Baada ya kuniambia hivyo mimi ndio nikazima gari moto. Kumbe yeye alimaanisha nisepe!
 
Wataalamu wa lugha husema kwamba lugha ni kitu hai; hukua na kufa. Lugha kadhaa hapa duniani zilikua kisha zikafa mazima, kama kilatini, sanskrit n.k. Sijui jinsi lugha zinavyokufa mazima ila najua jinsi maneno ya lugha fulani yanavyobadili maana.!


Lugha ndiyo zilivyo. Neno moja linapewa maana hii huku kule lina maana nyingine. Kwa mfano matumizi ya neno "tafadhali" hapa bara na kule Unguja ni tofauti. Neno "bibi" linavyotumika Kenya tofauti na hapa Tanzania. Ndiyo maana kuna Kiingereza cha Kifaransa, Kireno cha Brazil na Kiswahili cha Kenya. Matumizi ya lugha tajwa kama inavyoongelewa na kutumiwa katika nchi fulani ama eneo fulani. Ndio maana kipo Kiingereza cha Marekani na kile cha Uingereza. Na tufahamu kuwa hayo maneno hayawezi kutumika kwa maana za kibongo mtu akiyatumia anapoongea kiingereza. Yatatumika tu katika maudhui ya Kiswahili, yakibeba maana za Kiswahili si kiingereza tena. Yame-Swahilishwa isivyo rasmi.
 
Locally .... Ni ya kienyeji. Personality ni yenye hadhi,,, na booking OFFICE... Ni SEHEMU ya kukatia ticketi mbona wapo sahihi tu...
 
Local government. Serikali ya hovyo kabisa
Ndiyo nilitaka kuulizia hilo pamoja na local market!! Itakuwa soko la hovyo hovyo? Ninavyojua neno local ni kinyume cha neno foreign /a /kigeni!! Hilo la hovyo hovyo sijui
 
Ninavyojua

Local = Kienyeji

Umevaa kilocal, una mambo local = umevaa kienyeji, una mambo ya kienyeji n.k.

Kampuni nyingi za magari, eneo lao la kukatia tiketi hua ni hilo hilo wanahifadhi mizigo. Ulipoambiwa peleka mizigo booking office kwa mazingira yetu walikua sahihi.
Uko sahihi Nina wasiwasi na mtoa maada ndio kilaza mfano hapo kwenye maelekezo ya kupeleka mzigo "booking office" mbona ilikuwa sahihi na hata hapo kwenye "LOCAL" ni sahihi. Mfano huu mtu wa Tanzania akivaa nguo za kusitiri mwili wake vizuri kulingana na maadili yetu yuko LOCALLY
 
Hiyo namba moja mimi sioni kama wamebadili. Mimi nadhani ni kasumba tu ya kuona vitu vizuri vinatoka kwa wenzetu hasa wazungu. Huwa husikii mtu akiwa anasifia kitu akitaka kuweka msisitizo anasema 'kama mbele'? Kwa maana hiyo watu tunaamini mambo yetu sisi ni hovyo-hovyo kwa hiyo mtu akiwa wa hovyohovyo anakuwa anakuwa anawakilisha utanzania haswaa
 
Ninavyojua

Local = Kienyeji

Umevaa kilocal, una mambo local = umevaa kienyeji, una mambo ya kienyeji n.k.

Kampuni nyingi za magari, eneo lao la kukatia tiketi hua ni hilo hilo wanahifadhi mizigo. Ulipoambiwa peleka mizigo booking office kwa mazingira yetu walikua sahihi.
Aisee kwa hiyo mambo ya kienyeji yote ni ya ovyoovyo na ya kudharaulika
 
Back
Top Bottom