Maneno mengi kwa wanaojifanya wachambuzi, lengo ni kuivuruga Yanga

Maneno mengi kwa wanaojifanya wachambuzi, lengo ni kuivuruga Yanga

Nilisema hapa kulingana na mtiriko wa mechi na aina ya wapinzani waliokutana na Yanga mechi ngumu mfululizo, watu wangeanza kuhoji habari ya rotation baada ya mechi ya Yanga dhidi ya Mtibwa. La mwisho ni kwamba, japo Gamond ameingia katika kundi la wanaomchukia ila inaweza kuchukua muda mrefu kuiona Yanga yenye kasi kama Yanga hii ya Gamondi, Yanga yenye soka safi kama Yanga hii ya Gamondi. Kuna mapungufu madogo madogo ya matumizi ya nafasi ambalo bado limekuwa tatizo sugu kwa akina Mzize na wengineo.
 
Back
Top Bottom