Maneno (sentence) ya kutia hasira uloambiwa na bosi/mkuu wako

busy bees

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Posts
2,249
Reaction score
1,340
Salaam wana JF

Katika maeneo ya kazi hasa hasa taasisi binafsi huwa zatolewa kauli sijui niziite CHAFU ambazo si tu kuwa hukera, huumiza hasa KISAIKOLOJIA bali pia kukatisha tamaa na kuhafifisha malengo pia kushusha ufanisi .....

Tushirikishane na itakuwa vyema ukatujuza pia namna ulivyokabiliana na hiyo changamoto ili maisha yako yaendelee ..... UZOEFU huo waweza kuwa msaada kwa mtu fulani ....
 
Nilipoandika barua kwa bosi nikiomba gari ili nipelekwe hospital, nilijibiwa ...... "Kwani barua yako ya mkataba wa ajira uliambiwa utapewa gari ..... acha ujinga tumia mshahara wako kodisha pikipiki. .."
 
Boss wangu kwenye kikao hapendagi maswali siku hiyo nikajikuta nauliza swali, daah badala ya kupewa jibu ni vitisho, eti nina uwezo wa kukuondoa na ukahamishiwa popote, sikuogopi na kama unanirekodi rekodi.
Siku ilikuwa ndefu
 
Enzi hizo ninakimkataba cha mwaka mmoja ndio nimebakiza mwezi ni renew nikatibuana na deputy manager akaniuliza "when are you going to renew your contract? " nikamjibu bado kama mwezi hivi!... akaniambia "your days are numbered"

Roho iliniuma! Ila sikumjibu week tatu mbele zilikuwa ngumu sana......Kibaya siku sita kabla sija sign mkataba wangu akatimuliwa yeye... karma achana nayo.
 
Boss wangu kwenye kikao hapendagi maswali siku hiyo nikajikuta nauliza swali, daah badala ya kupewa jibu ni vitisho, eti nina uwezo wa kukuondoa na ukahamishiwa popote, sikuogopi na kama unanirekodi rekodi.
Siku ilikuwa ndefu
"siku ilikuwa ndefu .... " masaa 12 ya mchana kutwa yakawa 24
 
"your days are numbered .... " afu uambiwe kipindi kama hiki ajira imekuwa "rubby" waweza changanyikiwa ukajikuta wasahau hata jina lako asee
 
Siku moja boss aliniambia " wewe ni hope less " iliniuma sana nikajirekebisha baada ya miezi kadhaa akaniita ofisini kunipongeza kwa kubadiri tabia.
mkuu sorry ulikuwa hopeless kweli ama bosi alivuka mstari mwekundu
 
Sijawai kutukanwa mi ndo natukana...na Leo kuna dogo kaja kachelewa nmemwambia sense nyumbani akalale akichoka arudi kazini..
 
Nilipoandika barua kwa bosi nikiomba gari ili nipelekwe hospital, nilijibiwa ...... "Kwani barua yako ya mkataba wa ajira uliambiwa utapewa gari ..... acha ujinga tumia mshahara wako kodisha pikipiki. .."
Japo nilikuwa naumwa taaban ... nilikuwa mpole nkafanya maandalizi ya pikipiki (mshikaki) ili nipate support/balance .... but at last nikapata msaada wa gari ya halmashaur (afya) walokuwa wakirejea mjini baada ya kufanya- delivery ya dawa na vifaa tiba kwenye kituo cha afya pia kutoa chanjo ya minyoo kwa wanafunzi toka vijiji vilivyozunguka mradi wetu .... na hiyo ilikuwa ni baada ya mwendo kama wa nusu kilometa tangu tuanze safari yeye km zaidi ya 45
 
Sijawai kutukanwa mi ndo natukana...na Leo kuna dogo kaja kachelewa nmemwambia sense nyumbani akalale akichoka arudi kazini..
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
We acha tu, nilitamani kesho yake pasiwepo na kaziii ili tu nisikutane nae
Ulikabilianaje na hayo mazingira mkuu .... je wajibu wako wa kila siku ulikukutanisha na huyo bosi?
 
Pole, ni changamoto za maisha tuu ndugu
 
Sipendi mtu aninyanyase sababu ya nafasi niliyopo, vivyo hivyo sipendi kumnyanyasa mtu mwingine.

Kama ningekuwa na Boss basi angetakiwa awe na utu, lasivyo ni lazima angenifukuza.
 
Sipendi mtu aninyanyase sababu ya nafasi niliyopo, vivyo hivyo sipendi kumnyanyasa mtu mwingine.

Kama ningekuwa na Boss basi angetakiwa awe na utu, lasivyo ni lazima angenifukuza.
ndo ukutane na bosi mchina na nasikia wana kiburi na jeuri balaa c ndo utarusha na ngumi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…