Maneno (sentence) ya kutia hasira uloambiwa na bosi/mkuu wako

[emoji6] [emoji6] [emoji6] [emoji6] [emoji6]
Hukumwambia chochote kumpongeza mkuu?
 
Da mi nilichelewa nikaambiwa 'hapa hatuji kucheza cheza kama huwezi kuwahi,bora ubaki nyumbani ulale', da mhindi huyo na traffc jam za dar mhii shidaa
 
Nakumbuka kuna siku jioni natuma report ya siku kwa Boss,ghafla akanijibu nafaa kufanya kazi bar alinikatisha tamaa sana,baada kama ya mwezi mmoja hivi akanipiga chini,baada ya siku tatu hivi nikapata boge la job,ofisi safi na dereva yupo standby kuniendesha kunipeleka popote pale ninapotaka,siku moja kama wiki moja hivi nikakutana na yule Boss wa zamani kwenye mgahawa flani hivi anashushwa na dereva wake kupata lunch na mimi nashushwa na dereva wangu kupata msosi aliona aibu sana aisee,duniani humu kuna mambo sana.
 
"mfeli au mfaulu mwisho wa mwezi mshahara wangu upo pale pale" kauli hizi since nipo primary mpaka namaliza secondary hazikuwahi kuisha masikioni kwangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…