Maneno ya chuki hayaumizi hisia pekee, huharibu maisha na taaluma

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Anastazia alikuwa mwenye ndoto ya kuwa mwanasiasa mkubwa. Alizaliwa akiwa na kasoro ya kimwili kwenye uso wake, lakini hakuwahi kuruhusu hali hiyo imzuie kutimiza ndoto yake na kushiriki shughuli za kijamii.

Baada ya picha zake kuanza kusambaa mitandaoni, baadhi ya watu walianza kumkejeli na kumkashifu kutokana na maumbile yake. Wengine walimtengenezea majina ya dhihaka, wakamcheka na kumdhalilisha hadharani kwenye mitandao ya kijamii.

Kadri maneno ya chuki yalivyozidi, Anastazia alianza kupoteza kujiamini. Alijitenga na marafiki, akakosa usingizi na kupoteza focus kwenye career yake. Msongo wa mawazo uliongezeka na baadaye akaingia kwenye hali ya sonona (depression).

Licha ya kuwa na uwezo mkubwa kujieleza jukwaani, alishindwa kuendelea kufuatilia ndoto yake ya kuwa mwanasiasa. Aliamua kuacha baadhi ya shughuli kwa sababu ya hofu ya kuendelea kudhalilishwa.
 
Ni kweli kabisa kuwa maneno ya chuki yana madhara makubwa na ya kudumu yanayovuka mipaka ya maumivu ya hisia za kawaida.

Katika ngazi ya mtu binafsi, chuki ya maneno husababisha msongo mkubwa wa mawazo, wasiwasi uliopitiliza, na sonona, hatua zinazoweza kubomoa kabisa afya ya akili ya mwathirika na kumfanya ajitenge na jamii inayomzunguka.Kijamii na kitaaluma, athari zake ni kubwa sawa na uharibifu wa mali.

Maneno ya chuki yanaposambazwa, hasa mtandaoni, huharibu sifa na taswira ambayo mtu ameijenga kwa miaka mingi, hali inayopelekea kupoteza uaminifu mbele ya waajiri, wafanyakazi wenzake, au wateja. Hali hii isipodhibitiwa, husababisha wafanyakazi kufukuzwa kazi, biashara kufungwa, na fursa mpya za maendeleo ya kimaisha kufungwa kabisa, jambo linalothibitisha kuwa chuki si maneno tu, bali ni silaha inayoharibu mustakabali wa maisha.

Ili kukabiliana na janga hili, ni muhimu kuchukua hatua za haraka kwa kuhifadhi ushahidi wa ujumbe huo kupitia picha za skrini na kuripoti mara moja kwenye mifumo ya mitandao husika.

Pale ambapo maneno hayo yanahusisha vitisho vya usalama au kashfa nzito, ushirikiano na mamlaka za kisheria na usalama wa mitandao ni hatua ya lazima ili kulinda haki na usalama wako. Pia, kutafuta msaada wa kisaikolojia kutoka kwa wataalamu au watu wa karibu husaidia kurejesha amani ya moyo na nguvu ya kusonga mbele kimaisha.
 
Umenena vyema kaka, ukatili wa namna hii unaondoa watu kwenye reli.
 
Online bullying ni mbaya sana. Mtu hamjuani anakupiga na maneno mazito na hajui atakuachaje. Bora mtu akufanyie bullying mnaonana unaweza m-handle ila hawa ghost bullers ni mbaya sana...
 
Back
Top Bottom