Maneno ya dharau na kuudhi ya Juma Lokole kuhusu mtu mweusi yanaudhi na kushawishi unyonge kwa vijana wanaomsikiliza ambao ni weusi

Maneno ya dharau na kuudhi ya Juma Lokole kuhusu mtu mweusi yanaudhi na kushawishi unyonge kwa vijana wanaomsikiliza ambao ni weusi

alibaaliyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
623
Reaction score
576
Binadamu aliyeumbwa na Mungu ana haki ya kuheshimiwa. Ikiwemo kuheshimiwa rangi ya ngozi yake. Hii ni haki ya kikatiba katika nchi yetu ya Tanzania.

Mtanzania Juma Lokole akihojiwa mitandaoni amekuwa kuvunja haki hii. Amekuwa akikejeli rangi ya mtu mweusi anapohojiwa mitandaoni Rejea mahojiano kwenye tv ya mtandaoni "Maximum tv online". Anadhihaki rangi yetu sisi Waafrika weusi kwa maneno yafuatayo; weusi nuksi, rangi nyeusi ni rangi chafu, rangi nyeusi rangi ya matatizo. Anapoulizwa anasemaji kuhusu watu wanautukuza Uafrika yaani weusi wa uafrika anasema " ni kujifariji".

Maneno yake ya dharau na kuudhi kuhusu rangi ya mtu mweusi asilia yanaudhi lakini pia yanashawishi unyonge kwa vijana wanaomsikiliza ambao ni weusi. Mbaya zaidi maneno yake yanawafikia watu wengi. Hivi Wizara yetu pendwa ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo watu kama Juma Lokole mnawachukuliaje wanapoeneza kutojiamini na kutojikubali ndani ya jamii yetu.

Naamini kuwa KUJIAMINI kwa binadamu ndio chanzo cha maendeleo yake binafsi na jamii yake.
Juma Lokole anasambaza elimu ya mtu mweusi asilia ajiona myonge. Hana haki hii. Msanii Mpoki naye yuko kundi hili.

Mwafrika mweusi ametoka mbali katika kupigania haki yake ya kutambuliwa kama binadamu kamili ambayo ni kweli tupu. Tusiruhusu watu kama Juma Lokole, Mpoki kuturudisha nyuma.

OMBI: Wizara husika mchukue hatua.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yupo Sahihi sana.

MTU mweusi ndio Race yenye watu Wavivu, Wakatili, Wenye majungu na wasiopendana.

Pia tuna Imani za kijinga sana ambazo hazina maana.

Hatuna Ubunifu wala teknolojia ya kuweza kuwasaidia binadamu wengine duniani.

Ndio maana tulitawaliwa kikoloni na Waarabu na Wazungu kwa ukoloni wa zamani.

Hata leo watu weusi wengi wanatawaliwa na haohao na wameongezeka Wahindi pia kutawala mtu mweusi kikoloni kasoro tu ni mijeledi hatuioni.

Kama Mhindi anaajiri watanzania masikini wanafanya kazi ngumu katika mazingira magumu sana mfano kuchanganya rangi za nguo au kuchochea moto kiwandani usiku na mchana kisha analipwa elfu 80 kwa mwezi ndani ardhi yao, maji yao, serikali yao, huo sio ubepari na ukoloni?

Tunafanya kazi nyingi za kutumia nguvu kuliko akili na malipo ni kidogo sana.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye ana ka ji rangi kidogo ka kidhungu?
I mean ni kama akina Maria Sarungi?
 
We jamaa na wewe yani mtu anayebanduliwa na wanaume wenzake ndo anakuumiza kichwa namna hiyo? au umekosa thread za maana za kuanzisha mkuu?
 
Back
Top Bottom