Binadamu aliyeumbwa na Mungu ana haki ya kuheshimiwa. Ikiwemo kuheshimiwa rangi ya ngozi yake. Hii ni haki ya kikatiba katika nchi yetu ya Tanzania.
Mtanzania Juma Lokole akihojiwa mitandaoni amekuwa kuvunja haki hii. Amekuwa akikejeli rangi ya mtu mweusi anapohojiwa mitandaoni Rejea mahojiano kwenye tv ya mtandaoni "Maximum tv online". Anadhihaki rangi yetu sisi Waafrika weusi kwa maneno yafuatayo; weusi nuksi, rangi nyeusi ni rangi chafu, rangi nyeusi rangi ya matatizo. Anapoulizwa anasemaji kuhusu watu wanautukuza Uafrika yaani weusi wa uafrika anasema " ni kujifariji".
Maneno yake ya dharau na kuudhi kuhusu rangi ya mtu mweusi asilia yanaudhi lakini pia yanashawishi unyonge kwa vijana wanaomsikiliza ambao ni weusi. Mbaya zaidi maneno yake yanawafikia watu wengi. Hivi Wizara yetu pendwa ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo watu kama Juma Lokole mnawachukuliaje wanapoeneza kutojiamini na kutojikubali ndani ya jamii yetu.
Naamini kuwa KUJIAMINI kwa binadamu ndio chanzo cha maendeleo yake binafsi na jamii yake.
Juma Lokole anasambaza elimu ya mtu mweusi asilia ajiona myonge. Hana haki hii. Msanii Mpoki naye yuko kundi hili.
Mwafrika mweusi ametoka mbali katika kupigania haki yake ya kutambuliwa kama binadamu kamili ambayo ni kweli tupu. Tusiruhusu watu kama Juma Lokole, Mpoki kuturudisha nyuma.
OMBI: Wizara husika mchukue hatua.
Sent using
Jamii Forums mobile app