Heci
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 3,591
- 6,114
Kwenye geti la chuo kikuu cha Cape Town nchini Afrika kusini kuna maandishi yasemayo "Ukitaka kuangamiza taifa lolote duniani huhitaji kutumia silaha za nyuklia wala mabomu ya atomic. Njia nzuri ya kuangamiza taifa ni kuharibu mfumo wa elimu. Ruhusu "mbumbumbu" waonekane wamefaulu na wasonge mbele.
Matokeo yake yatajionesha baada ya muda, "mbumbumbu" hao wakishahitimu. Wagonjwa watafia mikononi mwa madaktari, majengo yataanguka mikononi mwa wahandisi, pesa zitapotelea mikononi mwa wachumi, utu utapotea mikononi mwa viongozi wa dini, na haki itapotelea mikononi mwa mahakimu. Kuchezea elimu ni kuangamiza taifa!