Maneno yaliyoandikwa kwenye geti la kuingia Chuo Kikuu cha Cape Town, yana funzo kubwa!

Maneno yaliyoandikwa kwenye geti la kuingia Chuo Kikuu cha Cape Town, yana funzo kubwa!

Kwenye geti la chuo kikuu cha Cape Town nchini Afrika kusini kuna maandishi yasemayo "Ukitaka kuangamiza taifa lolote duniani huhitaji kutumia silaha za nyuklia wala mabomu ya atomic. Njia nzuri ya kuangamiza taifa ni kuharibu mfumo wa elimu. Ruhusu "mbumbumbu" waonekane wamefaulu na wasonge mbele.

Matokeo yake yatajionesha baada ya muda, "mbumbumbu" hao wakishahitimu. Wagonjwa watafia mikononi mwa madaktari, majengo yataanguka mikononi mwa wahandisi, pesa zitapotelea mikononi mwa wachumi, utu utapotea mikononi mwa viongozi wa dini, na haki itapotelea mikononi mwa mahakimu. Kuchezea elimu ni kuangamiza taifa
UCT wanaelewa. . Tz je?
 
Tatizo kwetu hatujui cha kuchagua japo nasikia tu kupanga ni kuchagua:
i. Quality hatutaki, watu wakitaka quality education utasikia wengine wanapiga kelele si waachiwe tu wote waendelee Mara kutafutwe namna F iwe C kwa kushusha kidogo "-" katikayi ili kuunda "[" ambayo sir tutaita "C" na hapa ndo tunasimama mbele ya kamera na kusema wamefaulu vizuri wakati F ndo imekuwa C.
ii. Quantity, wale wa quantity education wanapenda mamba kubwa hali watoto wao wako nje
 
Samahani mleta uzi, unaweza kuweka picha ya hilo BANGO hapa kwenye hii thread?
 
Mie ndo maana niliamua kujielimisha mwenyewe.ningetegemea elimu ya kumezeshwa darasani na hizi sylabus chovu nisingekuwa najua ninayoyajua hivi sasa.
 
Ikiwa viongozi wanaotawala waliopata elimu hii hii inamaanisha vichwani ni sifuri, na km wao wenyewe ni sifuri watapata wapi ujuzi wa kutambua kuboresha elimu!?
aiseeeee
 
kusahihisha mitihani kwa njia ya mashine kumepekekea wanafunzi kufanya mitihani ya hesabu kwa njia ya kuchagua maswali bomu hilo

usitoze michango ya walimu wa ajira za muda huku shule nzima walimu wa sayansi na hisabati ni wanne tu bomu hilo

tunapanda mbegu ya uharibifu sisi wenyewe
Neno kuntu
 
Shule yetu ya Kata hapa mjini imerundika watoto 3000 kwenye miundombinu ya watoto 400 sasa hivi wanasoma kwa shift, mwakani tunategemea "Zero" (isome kama kiswahili) 300. Hii ndiyo elimu bila malipo,, halafu mipumbavu inazuia shule za private zisikaririshe ng'ombe!
 
Nafikiri kwa upande wa elimu ya chuo. Tuache kutumia written examinations kama njia ya kupima uelewa na ufaulu wa wanafunzi. Tubase kwenye kupima competence, ya mwanafunzi kwa oral examinations na practicals.
 
Oral examinations na practicals ndio zilikua zinanifanya nisome wakati niko chuoni,.
Oral examination ya kwanza nilifanya nikiwa std 7 wakati nafanya mtihani wa kujiunga na Seminary.Ni mfumo mzuri sana wa kutahini
 
kusahihisha mitihani kwa njia ya mashine kumepekekea wanafunzi kufanya mitihani ya hesabu kwa njia ya kuchagua maswali bomu hilo

usitoze michango ya walimu wa ajira za muda huku shule nzima walimu wa sayansi na hisabati ni wanne tu bomu hilo

tunapanda mbegu ya uharibifu sisi wenyewe
mkuu una uhakika na hayo? wewe umesoma hesabu? kuchagua ni kubaya, mbona vyuo vikuu yapo na watu hawafaulu!
 
Back
Top Bottom