Maneno yaliyoandikwa kwenye geti la kuingia Chuo Kikuu cha Cape Town, yana funzo kubwa!

Ikiwa viongozi wanaotawala waliopata elimu hii hii inamaanisha vichwani ni sifuri, na km wao wenyewe ni sifuri watapata wapi ujuzi wa kutambua kuboresha elimu!?
Hapo kitambo wakati wa Mwalimu mwenyewe tulikua sawa.

Sema kuna bwana mmoja aliibuka na mfumo huo sijui hata aliukota wapi...

Katuvuruga mpaka leo tumepoteana tunatafuta mchawi hatumuoni.

Mama Tanzania kapiga kelele wee kuhusu KKK hadi kaugua...
 
Sisi kazi yetu ni kukopi na kupaste. Hakuna utaratibu kila waziri analeta mawazo yake. Huyu sasa kakaa muda mrefu madudu yake yatafumuliwa akiondoka. Mara divisheni mara GPA, mara kubadili dividheni mara scantron.
Mara TCU inadahili mara vyuo vyenyewe, mara pivate schools hakuna kufukuza wanao fail mara hakuna kurusha madarasa, mara ada elekezi mara elimu bure, mara wazazi changieni chakula cha watoto wenu, mara paap kumekuchwa...ili mradi matamko kumridhisha mkuu.
Hii serikali wakitoka, utasikia huu mfumo mbovu hahaha.
 
Kwenye geti la chuo kikuu cha Cape Town nchini Afrika kusini kuna maandishi yasemayo "Ukitaka kuangamiza taifa lolote duniani huhitaji kutumia silaha za nyuklia wala mabomu ya atomic. Njia nzuri ya kuangamiza taifa ni kuharibu mfumo wa elimu. Ruhusu "mbumbumbu" waonekane wamefaulu na wasonge mbele.

Matokeo yake yatajionesha baada ya muda, "mbumbumbu" hao wakishahitimu. Wagonjwa watafia mikononi mwa madaktari, majengo yataanguka mikononi mwa wahandisi, pesa zitapotelea mikononi mwa wachumi, utu utapotea mikononi mwa viongozi wa dini, na haki itapotelea mikononi mwa mahakimu. Kuchezea elimu ni kuangamiza taifa

Hayo maneno na yenyewe pia yameandikwa hivi hivi kwa Kiswahili Mkuu au? Kama yameandikwa kwa Kiingereza basi tunakuomba utuandikie hapa mubashara / live ili na Sisi pia tuweze kuyatafsiri vizuri kwani katika Saikolojia kila Binadamu ana mtazamo wake juu ya jambo / kitu / taarifa fulani.
 
Wewe Google tu, utayaona pale kwenye lango la kuingilia chuo.
 
Na hii Serikali iko busy kununua wapinzani badala ya kusimamia mambo ya msingi kama Elimu.
 
Wewe Google tu, utayaona pale kwenye lango la kuingilia chuo.

Kwani hujayakariri Mkuu? Halafu samahani Wewe ndiye muanzisha uzi ambaye kimsingi ndiyo nilimuomba Yeye hayo maneno?
 
mkuu una uhakika na hayo? wewe umesoma hesabu? kuchagua ni kubaya, mbona vyuo vikuu yapo na watu hawafaulu!
unajua maana ya elimu ya msingi? unamjengea mwanao tabia ya kuchagua majibu ya hesabu?
solving vs choosing most suitable answer umeambiwa hiyo ni ufahamu?
 
Huku kwetu kuanzia Jana wazazi wamejazana ofisi ya kijiji wanadai pesa zao walizo zitoa kama michango ya kwenda kufyatulia tofali ili tujenge secondary ya pili,kisa cha kudai ni mkuu kasema ,haki vile tunaizika elimu yetu kiziko ambacho hakijapata kutokea naonea huruma sana Taifa langu nalia machozi yamasikitiko eehh Mungu tumekukosea wapi baba khaa
 
Kwenye geti la chuo kikuu cha Cape Town nchini Afrika kusini kuna maandishi yasemayo "Ukitaka kuangamiza taifa lolote duniani huhitaji kutumia silaha za nyuklia wala mabomu ya atomic. Njia nzuri ya kuangamiza taifa ni kuharibu mfumo wa elimu. Ruhusu "mbumbumbu" waonekane wamefaulu na wasonge mbele.

Matokeo yake yatajionesha baada ya muda, "mbumbumbu" hao wakishahitimu. Wagonjwa watafia mikononi mwa madaktari, majengo yataanguka mikononi mwa wahandisi, pesa zitapotelea mikononi mwa wachumi, utu utapotea mikononi mwa viongozi wa dini, na haki itapotelea mikononi mwa mahakimu. Kuchezea elimu ni kuangamiza taifa
Ujumbe mwanana
 
Huku kwetu kuanzia Jana wazazi wamejazana ofisi ya kijiji wanadai pesa zao walizo zitoa kama michango ya kwenda kufyatulia tofali ili tujenge secondary ya pili,kisa cha kudai ni mkuu kasema ,haki vile tunaizika elimu yetu kiziko ambacho hakijapata kutokea naonea huruma sana Taifa langu nalia machozi yamasikitiko eehh Mungu tumekukosea wapi baba khaa
yani kma nilikua sijanunuliza vifaa vya ujenzi ni hapohapo nawapangisha foleni unasaini unapewa cha kwako hiyo yote ni kwa faida yao kama wanaona ni hasara unaachana nao wasubiri serikali iwajengee
 
Back
Top Bottom