Maneno yaliyoandikwa kwenye geti la kuingia Chuo Kikuu cha Cape Town, yana funzo kubwa!

Hesabu eti ina matiple choice nikiuandaaga huu mtihani huwa nachekaga peke yangu.
 
*Nmeipenda hii* ```Kwenye geti la chuo kikuu cha Cape Town nchini Afrika kusini kuna maandishi yasemayo "Ukitaka kuangamiza taifa lolote duniani huhitaji kutumia silaha za nyuklia wala mabomu ya atomic. Njia nzuri ya kuangamiza taifa ni kuharibu mfumo wa elimu. Ruhusu "mbumbumbu" waonekane wamefaulu na wasonge mbele.

Matokeo yake yatajionesha baada ya muda, "mbumbumbu" hao wakishahitimu. Wagonjwa watafia mikononi mwa madaktari, majengo yataanguka mikononi mwa wahandisi, pesa zitapotelea mikononi mwa wachumi, utu utapotea mikononi mwa viongozi wa dini, na haki itapotelea mikononi mwa wanasheria.
 
Gate kuu LA kuingia Makao Makuu ya CIA kuna maandishi"You shall know the truth, and the truth shall set you free" yaani utaijua kweli na kweli itakuweka huru.Hivyo watu wanahangaika usiku na mchana na kwa gharama kubwa kutafuta ukweli, uwe wa kijiografia,wa kihistoria,wa kisiasa, wa kiuchumi nk ili uwaweke huru
 
Kwenye gate letu kuna hii: Jiwe huangushwa na Jiwe
 
Kwenye mlango wangu wa geto langu pameandikwa "Kakojoe ukalale"
 
Kwenye mlango wangu pameandikwa UYAONAYO YAACHE HUMUHUMU.
 
Kwenye geti la mjumbe wetu wa nyumba kumi pameandikwa"Barafu zipo"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…