Maneno yanayowakera wanawake!

Maneno yanayowakera wanawake!

Nailyne

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2010
Posts
350
Reaction score
113
Kugombana katika mahusiano au ndoa ni kawaida na sehemu ya maisha watu mnachukuliana maisha yaende sasa kuna yale maneno utakuta mwanaume anamasea mwanamke
' ndio maana malaya wewe'
'peleka huko kazi yako si kujiuza tu'
'wewe hujatualia ni mapepe tuu'
'we unazani nisinge kuoa ungeolewa wewe?'
hayo ni baadhi ya maneno ambayo nimewasikia baadhi wa wanawake wenzangu wakilalamikia wanaume zao kuwatukana hivyo,kwa kweli akina baba haipendezi kumwambia mwanamke aliyekuzalia watoto malaya hata kama amekukosea!maneno mengine huwa hayafutiki moyoni haraka na yanapunguza mapenzi kwa kiasi kikubwa sana. Tujaribu kugombana kwa kutukia akili ni sio mioyo, tujaribu kutumia kauli ambazo zitajenga uhusiano na sio kubomoa ni hayo tu.

Angalizo; wapo pia wanawake wenye midomo michafu sana kwa wanaume au wapenzi wao hili pia laweza kuwa ni tatizo kwa jinsia zote.
 
Kwenye hasira people say things they dont mean....., na mwenza sababu huwa ameumia na yeye anataka amuumize mwenzake atasema chochote cha kumuuzi mwenzie, na kutoa hayo maneno mtu ndio anavyotoa steam.... ingawa matusi si vizuri lakini wanasema ni bora kitu ukakitoa kuliko kukiacha rohoni, sababu siku kikifumuka..., thats when unasekia fulani amengatwa sikio....🙂😛eace: therefore sometimes arguments are healthy...
 
ni kweli kabisa...., tatizo ni pale ambapo hayo maneno yanaporudiwa rudiwa kila mkigombana mwenzio anakuita ma###y# hapo ndio panapoleta utata!
 
Hizo ni tabia mbaya na mtu mstaarabu inapaswa asimwite hata adui yake hayo maneno..., alafu hii nimeona kwa kina dada wengi anaweza akaanzisha ugomvi mbele ya marafiki ya mme wake au hata akamfata bar na kulianzisha... Mi naona ustaarabu kama mmekosana basi muitane chumbani mbali ya watoto na huko mpeane maneno na arguments zenu mkimaliza basi mnakumbatiana na let bygones be bygones....

..........:thinking: "if only it was this simple..."
 
Wakati mwingine ni vizuri kama umepatwa na hasira ukakaa mbali na huyo aliekuudhi kwa muda mchache kama saa moja au mbili hivi, ili kuepuka kuongea sana manake unaweza kujikuta unaongea neno ambalo hata we mwenyewe ukija kulitafakari baadae unaumia.

Pia jawabu la upole hupunguza wingi wa hasira na ghadhabu.Afadhali kunyamaza kimya wakati mwingine.
 
hilo nalo neno!
 
Mi hua nikikasirika najaribu kutokuongea na huyo mtu kwa wakati huo.
Mtu unatakiwa utulie kidogo kupunguza hasira maana ukiwa umekasirika
mtu hata akikwambia sijui pole...ohh samahani unaona kama anakuzingua tu.
Sasa kuna watu wao hiyo hawawezi kwahiyo analipuka tu right there and then!!!
 
Ugomvi si tabia ya kiungwana na matusi si hekima...hata kidogo...kwa maana hiyo hata tusi lililosemwa softly bado sili-entertain kwa kua halikuzingatia kanuni niliyoitoa hapo juu
 
Mi huwa naondoka sehemu hiyo ili nisiseme maneno nitakayoyajutia baadae.Hi lizzy hope your ok,za toka jana ? missing you besti.
 
Ugomvi si tabia ya kiungwana na matusi si hekima...hata kidogo...kwa maana hiyo hata tusi lililosemwa softly bado sili-entertain kwa kua halikuzingatia kanuni niliyoitoa hapo juu

Mkuu,
haya usemayo ni kweli kabisa...lakini hapa JF mbona hizi lugha za kukera zinatumika sana tu au ubaya ni pale zikitumika kwa wanawake tu.. Jf yanashushwa maneno ya kukera, mengine matusi ya nguoni.
Tujitahidi wanaJF kuitafakari kauli ya Horseshoe Arch tunapotoa michango yetu kwenye forums hapa JF pia.
 
Kwenye hasira people say things they dont mean....., na mwenza sababu huwa ameumia na yeye anataka amuumize mwenzake atasema chochote cha kumuuzi mwenzie, na kutoa hayo maneno mtu ndio anavyotoa steam.... ingawa matusi si vizuri lakini wanasema ni bora kitu ukakitoa kuliko kukiacha rohoni, sababu siku kikifumuka..., thats when unasekia fulani amengatwa sikio....🙂😛eace: therefore sometimes arguments are healthy...

Ni kweli kabisa VoR lakini hata kwenye ugomvi ni lazima wahusika wachague maneno yao very careful maana kumuita mkeo malaya haistahili kabisa hata wakati wa ugomvi huko ni kumdhalilisha kupita kiasi.
..
 
Jaman siyo mke tu mwanamke yeyote anahitaji kuthaminiwa kusikilizwa kuheshimiwa na kama amekosea ajibiwe kwa hekima ya ndani sana kulingana na udhaifu wake na siyo matusi na katika uzoefu wangu nimegungua kuwa ukiwa mpole na mstaarabu na hata kunyamaza kwa mwanamke mwenye makosa na vituko huwa ni adhabu kubwa sana kuliko hjizo za matusi ambazo zitakufanya udharaulike tu hata kama mkirudiana tena yanaacha majeraha mioyoni mwao
 
ila kusema ukweli hasa uswahilini wanawake wengi ndio wana maneno machafu kuliko wanaume ndio maana kila siku unakuta uswazi w/ume wanatembeza vibao baada ya kuzidiwa na maneno machafu
 
Kuna jamaa mmoja wakati anagombana na mke wake akamwambia "Hivi kati wanawake na wewe ni mwanamke" nilijiuliza maswali mengi ila majibu sikupata.
 
maneno mengine yachekesha wallah sasa kama ni mwanamme kwanini alimuoa??? na kampata tuu wakumwambia hivyo mi ningempa jibu lililo eleweka.. lol...

Hapo nilichoka kweli, ila kweli kuna mambo mengine yanafurahisha sana
 
Mi hua nikikasirika najaribu kutokuongea na huyo mtu kwa wakati huo.
Mtu unatakiwa utulie kidogo kupunguza hasira maana ukiwa umekasirika
mtu hata akikwambia sijui pole...ohh samahani unaona kama anakuzingua tu.
Sasa kuna watu wao hiyo hawawezi kwahiyo analipuka tu right there and then!!!
Hasira za kupindukia zinatokana na ulaji kwa wingi wa Red Meat. punguzeni kula nyama kama Simba.
:-*
 
ila kusema ukweli hasa uswahilini wanawake wengi ndio wana maneno machafu kuliko wanaume ndio maana kila siku unakuta uswazi w/ume wanatembeza vibao baada ya kuzidiwa na maneno machafu

sign yako nzuri
 
Back
Top Bottom