Mange Kimambi na Maria Sarungi wamehusika kuhujumu maandamano

Mange Kimambi na Maria Sarungi wamehusika kuhujumu maandamano

MANGE KIMAMBI NA MARIA SARUNGI WAMEHUSIKA KUHUJUMU MAANDAMANO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kukosa Uongozi wa Kitaalamu na Kimaadili

Watu wenye tabia ya kuropoka au kutumia lugha ya matusi mtaani na mitandaoni mara nyingi hukosa uaminifu wa kijamii.
Wafuasi wanaposhuhudia matusi, kejeli, au hasira zisizodhibitiwa, hamasa hubadilika kuwa utani au hofu.
Kwa mfano:

Mange Kimambi amekuwa akitumia lugha kali dhidi ya watu tofauti, matusi ya nguoni hii imewafanya baadhi ya wafuasi na watu kumwona kama msemaji mwenye hasira na asiye na maadili badala ya kiongozi wa mabadiliko.

Uongozi wa maandamano unahitaji hekima, nidhamu, na heshima ya hoja; si kelele za hasira na matusi.

Kiongozi ambaye anaendana na culture ya jamii husika. Kutumia matusi mitandaoni na kutukana watu bila kujali ni mkubwa au mdogo inapunguza ushawishi wa mtu kwenye mambo ya maana.

2. Kuitisha Maandamano kwa Muda Mrefu (Zaidi ya Miezi Miwili)

Haya ni makosa ya kimkakati. Hili nilieleza kwenye post za nyuma.
Maandamano ni kama moto kwenye nyasi au mabua. ukichelewesha kuwasha, moto unazima kabla hujawasha kiberiti.
Watu hupoteza:
hamasa,
imani,
na kipaumbele (kwani maisha yao ya kila siku yanahitaji kuendelea). Na vipaombele vinabadilika. Zaidi ya yote unampa adui (ambaye hapa ni serikali) kujipanga namna ya kuyadhibiti.

3. Kukosa Muunganiko na Viongozi wa Ndani (Ground Movement)

Maandamano yenye mafanikio huhitaji muungano wa ndani: vyama, viongozi wa kijamii, wanafunzi, wafanyabiashara, wajasiriamali n.k.
Viongozi walioko nje ya nchi, na wanaharakati kama Mange, hukosa:
a) kugusa uhalisia wa hofu za wananchi.
Ukiwa nje ya nchi ukawa kiongozi wa maandamano hasa kwenye nchi kama Tanzania kisaikolojia utaonekana wewe sio mmoja wao. Ila unawasakizia wenzako.
na kuwajibika moja kwa moja iwapo vurugu au hatari ikitokea.
Matokeo yake wananchi wa ndani ya nchi hawaoni uhalisia wa uongozi huo, bali wanaona mtu aliyekimbia nchi anawaambia wapambane yeye akiwa salama.

4. Kuchonganisha Taasisi za Ulinzi (Jeshi na Polisi)

Uongozi wa maandamano unahitaji mkakati wa kisaikolojia na diplomasia.
Kusema maneno yanayochonganisha jeshi, polisi, au taasisi za dola ni sawa na:

a) kuamsha tahadhari za usalama,
Hapa ni sawa na kushawishi jeshi liasi na lipindue serikali kwa kudhibiti Polisi. Hivyo serikali lazima ichukue tahadhari kubwa kukabiliana na uchonganishi huo.

b) kupunguza uhalali wa maandamano,
Kupindua serikali ikiwa ni sehemu ya agenda za kuandamana kabla hata ya maandamano automatically yanapoteza uhalali.
Hata kama kungekuwa na mpango wa kuipindua serikali haikupaswa usemwe waziwazi hivi. Ingepaswa ifanyike wakati maandamano yanafanyika na yamekolea.
Kutaka kupindua serikali ni kosa la uhaini.

c) Kutoa nafasi ya serikali kutumia nguvu kwa uhalali wa kisheria.
Hivyo, badala ya maandamano kuwa sauti ya umma, yanaonekana kama uchochezi wa kuvuruga amani.

5. Kufeli kwa MANGE zaidi ya mara mbili katika kuhamasisha maandamano.
Kwenye siasa na utawala kuna msemo usemao Once a loser, Always a Loser.
Ukikubali kushindwa mara moja kwenye siasa upo kwenye nafasi ya kushindwa daima. Hiyo ni kanuni. Ndio maana kwenye siasa ukiingia lazima uwe na hesabu kali hasa kwenye pigano au pambano la kwanza kwa sababu hilo ndio limebeba msingi wako. Unaweza mtazama Raila Odinga, Edward Lowasa na wengineo.
Mange kimambi tayari anarekodi ya kushindwa kuhamasisha maandamano zaidi ya mara mbili.
Hakupaswa kwenye maandamano haya awe kinara. Yeye angetakiwa atokee pembeni.
Kuongozwa na kiongozi aliyeshindwa kwenye siasa lazima ushindwe tuu. Labda muujiza utokee lakini siasa hazitegemei mara nyingi miujiza.

6. Kukosa Mkakati wa Baada ya Maandamano.

Wengi hushindwa kujibu swali rahisi:
“Baada ya maandamano, tunataka nini hasa, na tutafikaje huko?”



Mara nyingi viongozi na wanaharakati wengi wenye kelele zaidi mtandaoni hawana mpango wa kisera, mikakati, bali huongozwa na mihemko na matumaini hewa kwa kujidanganya.

Hivyo, hata kama watu wangetoka barabarani, hakuna hatua za kimfumo za kufuatilia matokeo na kutekeleza mpango wenye tija ili kulinda maslahi na haki za watu wote.

Embu fikiria maandamano yamefanikiwa. Unafikiri nini kitatokea?
Ngoja nikudokeze kwa sehemu nini kitatokea
a) Mauaji na visasi kwa viongozi wa serikali.
b) Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwani viongozi nao watakuwa wanajitetea kwa kutumia pesa zao na ikiwezekana kukimbia nchi.
c) uhalifu wa kuiba kwenye mabenki, kuchoma mali za matajiri maarufu waliokuwa wanasapoti mfumo.
d) Wageni na watu jamii ya wahindu na waarabu na machotara watakuwa kwenye wakati mgumu sana. Kwani baadhi ya waandamanaji wana mtazamo kuwa wao ndio wanaiba mali za hii nchi.

e) Kutokuwa na political stability hasa kujua nani anashika nchi kwa muda. Kama ni jeshi nani atashika nafasi hiyo ukizingatia mpaka sasa jeshi lipo upande wa serikali

6. Propaganda zenye kuleta machafuko kati ya Raia na wanajeshi.
Kuna propaganda mbili zimetolewa kuhusu majeshi.
a) Majeshi ya Uganda yameingia Tanzania ili kuwapiga watanzania.
b) Majeshi ya Zanzibar yapo bara ili kuwapiga Watanzania.

Propaganda hizo lengo lake ni kuwapiganidha wananchi na wanajeshi.
Kwamba wananchi wa Tanzania bara siku ya maandamano ikitokea wamepigwa na polisi au wanajeshi wasishangae kwani hao askari sio watanzania wenzao.
Hivyo wapambane kufa kupona kwani wanatetea nchi yao dhidi ya uvamizi wa majeshi ya nchi nyingine.

Propaganda hii ingepaswa itolewe siku moja kabla ya maandamano ili kuchochea chuki na hasira ili Lengo la mange kimambi lifikiwe. Lakini halitafikiwa kwa sababu limetolewa wakati ambao sio sahihi ambapo serikali inaweza kuipotosha taarifa hiyo.

Lakini pia kusema kuna wanajeshi kutoka Uganda wamekuja Tanzania ni kulifanya jeshi la nchi liwe macho na kufuatilia kama ni kweli. Kama sio kweli Jeshi hata kama lingekuwa na mpango wa kuunga mkono maandamano mpango huo utafeli.

Kufikia hapo sina la ziada.

Nawatakia Sabato Njema.

Taikonmaster
Kwa sasa Dar es Salaam
Mkuu nashauri kipindi hiki ukae kimya maana naona unaelekea njia mbaya sana "From Hero to Zero"
 
Kumbe ukweli haufai hata kwa waandamanaji?
Nilidhani ni serikali tuu haipendi ukweli kumbe hata upande wenu?

Unataka tujadili ushabiki(upande) au tujadili hoja nilizoweka?

Sikutegemea kama hata upande wenu hampendi kuambiwa ukweli
Ndugu yetu wewe una tatizo la ki-saikolojia, I can assure you. Wewe siyo ''analytical thinker'' kama unavyodhani. Ni kilaza mmoja anayevizia matukio ili kujikweza. Ushauri wangu kwako: ongeza elimu yako kwa kusoma maandiko ya kitaalam na muhimu zaidi jishushe na acha kurukia kila kitu.
 
Sikiliza mtibeli, hii ngoma inogile ni ombwe lilioachwa wazi na CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani/ushindani. CHADEMA ndio ingefanya uchaguzi uwe na ladha yake kwa kuwa nayo ina watu wengi wa kuipa kura. Vibe la maandamano ni kama kuchukua nafasi ya chadema japo vibe hili liko mitandaoni tu kwenye grounda halipo. Anyway, maandamano hata yasipofanyika lengo litakuwa limetimia kuipa CCM ushindani kwenye uchaguzi. Unaona kabisa CCM inajibu kwa nguvu zote maandamano badala ya kuwajibu washindani wake inayoshindana nayo.
 
Ndugu yetu wewe una tatizo la ki-saikolojia, I can assure you. Wewe siyo ''analytical thinker'' kama unavyodhani. Ni kilaza mmoja anayevizia matukio ili kujikweza. Ushauri wangu kwako: ongeza elimu yako kwa kusoma maandiko ya kitaalam na muhimu zaidi jishushe na acha kurukia kila kitu.

Hayo yote umenipa wewe mkuu.
Ushauri wa elimu nimeupokea.
 
Mkuu nashauri kipindi hiki ukae kimya maana naona unaelekea njia mbaya sana "From Hero to Zero"
Huyu hajawahi kuwa hero hata siku moja. Ni vile sisi wabongo huwa tunapenda kupamba watu kwa mambo ambayo hata hawastahili. Nadhani ana tatizo la kujiona ana akili za kuchambua mambo kumbe ni kilaza mmoja mwenye upeo mdogo kabisa.
 
Kaka sio lazima tu uandike hata kama unaondika mambo ya Kipumbavu; Humu ndani kwa sasa unaweza Fanya Nini?

Basi tumekuteua wewe uwe kiongozi wa ndani, hemu jitahidi kuwekeza kwenye Heshima kidogo ambayo unayo.

1. Gwajima yupo wapi?
2. Pole pole yupo wapi?
3. Lisu yupo wapi?
4. Heche yupo wapi?

Unaongea tu kama li mtu lisilo na akili kabisa, Haya maandamano hayawezekani, waliofanya wamejitahidi kwa nafasi zao!
Usiwe na hasira sasa.
Jitahidi uelewe tupo katika dunia ipi. Nafikiri hata lengo la maandamano ni pamoja na uhuru wa maoni. Si ndio?



Kwa Mimi mtu wa utulivu ninayepata kidogo na wanangu siitaji maandamano, ila siwalaumu wanaojitahidi kwa nafasi zao.

Wewe unayewakosoa umefanya jambo gani la maana?

Mkuu kila mtu yupo kwenye laini yake.

Kila unachozuia nisifanye (kukosoa na kuona kasoro kwenye mapambano ya haki) ndicho hichohicho waandamanaji wanakipigania.

Waandamanaji wanatekwa kwa kuikosoa serikali. Mimi ninakosoa waandamanaji, nyie hamtaki. Sasa mngekuwa na nguvu mngefanyaje?

Muwe wavumilivu ambao mnauhitaji kwa serikali
Au ndio kuondoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako wakati wewe una boriti?

Mimi kusema Mange Kimambi anahusika kwenye kuhujumu maandamano kosa liko wapi? Kimevunja haki ipi?
Nitoe tongotongo Mkuu.


Usiwe na hasira.
 
Sikiliza mtibeli, hii ngoma inogile ni ombwe lilioachwa wazi na CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani/ushindani. CHADEMA ndio ingefanya uchaguzi uwe na ladha yake kwa kuwa nayo ina watu wengi wa kuipa kura. Vibe la maandamano ni kama kuchukua nafasi ya chadema japo vibe hili liko mitandaoni tu kwenye grounda halipo. Anyway, maandamano hata yasipofanyika lengo litakuwa limetimia kuipa CCM ushindani kwenye uchaguzi. Unaona kabisa CCM inajibu kwa nguvu zote maandamano badala ya kuwajibu washindani wake inayoshindana nayo.

Mimi mambo ya hivyo sitaki.
Mambo ya ku- assume
 
Haikufanya kazi


Hayajafanya kazi.
Lengo la maandamano
1. Kuzuia uchaguzi
2. Kufanya reforms kwenye tume ya uchaguzi na ikiwezekana katiba mpya.
3. Kupigania haki za. Watu wasitekwe.

Tangu maandamano yahamasishwe kipi kati ya hayo mambo au mengine kimebadilika mpaka useme the message was sent and delivered?
Hizo ni agenda za chadema na haya maandamano sio ya chadema. Wananchi ndio hawataki kutoka, kuishinikiza serikali kupingq uovu wa kuteka na kuuwa raia. Kumbuka haya sio maandamano ya chadema, so mambo ya reforms hayapo.

Lakini pia ujue, kama wewe ulivyoipa mahakama ultimatum na haikuwa chochote, inawezekana mwingine nae akafanya kwa strategy yake na isifanikiwe.
 
Mkuu ungechukua tu gurudumu uendeleze ukiona wao wamekosea, nchi yetu wote hii sio lazima wafanye kila kitu wao na wala sio malaika wale ujue!

Play your part boss kabla hujawajaji wanajitoa muhanga mtibelii(rii)
 
Huyu hajawahi kuwa hero hata siku moja. Ni vile sisi wabongo huwa tunapenda kupamba watu kwa mambo ambayo hata hawastahili. Nadhani ana tatizo la kujiona ana akili za kuchambua mambo kumbe ni kilaza mmoja mwenye upeo mdogo kabisa.

😂😂😂
Unabishia mtazamo wa wengine dhidi yangu. 😄😄
Wenzako walishaniona hero
Wewe hukuniona Hero.
Wengine hawakuwa na mpango na mimi kabisa yaani hawana maoni yoyote juu yangu.
Yote ni mitazamo.

So take easy mkuu. Wewe kuniona najiona ninaakili pia ni suala linalohusu mtazamo wako kunihusu. Mwingine humuhumu ananiona mimi ni mnyenyekevu 🤣🤣
Huo ndio ulimwengu Mkuu.
 
Mkuu ungechukua tu gurudumu uendeleze ukiona wao wamekosea, nchi yetu wote hii sio lazima wafanye kila kitu wao na wala sio malaika wale ujue!

Play your part boss jaji mtibelii(rii)

Nipo kwenye laini yangu. Na nina play part yangu fyema kabisa.

Tatizo letu ni kuleta uchama, ushabiki na unafik(kukataa ukweli). Hilo ni tatizo
 
Nipo kwenye laini yangu. Na nina play part yangu fyema kabisa.

Tatizo letu ni kuleta uchama, ushabiki na unafik(kukataa ukweli). Hilo ni tatizo

Wabongo kwa kukosoa hatujambo, wenzako wanatumia majina yao na wanajulikana we anonymous hapa JF unajifanya fundi wa kurekebisha, kupika na kupakua, ingia tu jikoni mkuu tuone umartin luther king wako!

Kuimba kupokezana ujue...
 
Mimi namsifu Mange kwa ubunifu wa kuwapigisha kwata majeshi ya Tanzania kama vikaragosi, akikaa kwenye keyboard tu huku polisi mikundu inawawasha mama'e zao.
 
Back
Top Bottom