Mange Kimambi na Maria Sarungi wamehusika kuhujumu maandamano

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
MANGE KIMAMBI NA MARIA SARUNGI WAMEHUSIKA KUHUJUMU MAANDAMANO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kukosa Uongozi wa Kitaalamu na Kimaadili

Watu wenye tabia ya kuropoka au kutumia lugha ya matusi mtaani na mitandaoni mara nyingi hukosa uaminifu wa kijamii.
Wafuasi wanaposhuhudia matusi, kejeli, au hasira zisizodhibitiwa, hamasa hubadilika kuwa utani au hofu.
Kwa mfano:

Mange Kimambi amekuwa akitumia lugha kali dhidi ya watu tofauti, matusi ya nguoni hii imewafanya baadhi ya wafuasi na watu kumwona kama msemaji mwenye hasira na asiye na maadili badala ya kiongozi wa mabadiliko.

Uongozi wa maandamano unahitaji hekima, nidhamu, na heshima ya hoja; si kelele za hasira na matusi.

Kiongozi ambaye anaendana na culture ya jamii husika. Kutumia matusi mitandaoni na kutukana watu bila kujali ni mkubwa au mdogo inapunguza ushawishi wa mtu kwenye mambo ya maana.

2. Kuitisha Maandamano kwa Muda Mrefu (Zaidi ya Miezi Miwili)

Haya ni makosa ya kimkakati. Hili nilieleza kwenye post za nyuma.
Maandamano ni kama moto kwenye nyasi au mabua. ukichelewesha kuwasha, moto unazima kabla hujawasha kiberiti.
Watu hupoteza:
hamasa, imani, na kipaumbele (kwani maisha yao ya kila siku yanahitaji kuendelea). Na vipaombele vinabadilika. Zaidi ya yote unampa adui (ambaye hapa ni serikali) kujipanga namna ya kuyadhibiti.

3. Kukosa Muunganiko na Viongozi wa Ndani (Ground Movement)

Maandamano yenye mafanikio huhitaji muungano wa ndani: vyama, viongozi wa kijamii, wanafunzi, wafanyabiashara, wajasiriamali n.k. Viongozi walioko nje ya nchi, na wanaharakati kama Mange, hukosa:
a) kugusa uhalisia wa hofu za wananchi.
Ukiwa nje ya nchi ukawa kiongozi wa maandamano hasa kwenye nchi kama Tanzania kisaikolojia utaonekana wewe sio mmoja wao. Ila unawasakizia wenzako.
na kuwajibika moja kwa moja iwapo vurugu au hatari ikitokea.
Matokeo yake wananchi wa ndani ya nchi hawaoni uhalisia wa uongozi huo, bali wanaona mtu aliyekimbia nchi anawaambia wapambane yeye akiwa salama.

4. Kuchonganisha Taasisi za Ulinzi (Jeshi na Polisi)

Uongozi wa maandamano unahitaji mkakati wa kisaikolojia na diplomasia. Kusema maneno yanayochonganisha jeshi, polisi, au taasisi za dola ni sawa na:

a) kuamsha tahadhari za usalama,
Hapa ni sawa na kushawishi jeshi liasi na lipindue serikali kwa kudhibiti Polisi. Hivyo serikali lazima ichukue tahadhari kubwa kukabiliana na uchonganishi huo.

b) kupunguza uhalali wa maandamano, Kupindua serikali ikiwa ni sehemu ya agenda za kuandamana kabla hata ya maandamano automatically yanapoteza uhalali.

Hata kama kungekuwa na mpango wa kuipindua serikali haikupaswa usemwe waziwazi hivi. Ingepaswa ifanyike wakati maandamano yanafanyika na yamekolea.
Kutaka kupindua serikali ni kosa la uhaini.

c) Kutoa nafasi ya serikali kutumia nguvu kwa uhalali wa kisheria.
Hivyo, badala ya maandamano kuwa sauti ya umma, yanaonekana kama uchochezi wa kuvuruga amani.

5. Kufeli kwa MANGE zaidi ya mara mbili katika kuhamasisha maandamano. Kwenye siasa na utawala kuna msemo usemao Once a loser, Always a Loser.
Ukikubali kushindwa mara moja kwenye siasa upo kwenye nafasi ya kushindwa daima. Hiyo ni kanuni. Ndio maana kwenye siasa ukiingia lazima uwe na hesabu kali hasa kwenye pigano au pambano la kwanza kwa sababu hilo ndio limebeba msingi wako. Unaweza mtazama Raila Odinga, Edward Lowasa na wengineo.

Mange kimambi tayari anarekodi ya kushindwa kuhamasisha maandamano zaidi ya mara mbili.
Hakupaswa kwenye maandamano haya awe kinara. Yeye angetakiwa atokee pembeni.

Kuongozwa na kiongozi aliyeshindwa kwenye siasa lazima ushindwe tuu. Labda muujiza utokee lakini siasa hazitegemei mara nyingi miujiza.

6. Kukosa Mkakati wa Baada ya Maandamano.

Wengi hushindwa kujibu swali rahisi: “Baada ya maandamano, tunataka nini hasa, na tutafikaje huko?”

Mara nyingi viongozi na wanaharakati wengi wenye kelele zaidi mtandaoni hawana mpango wa kisera, mikakati, bali huongozwa na mihemko na matumaini hewa kwa kujidanganya.

Hivyo, hata kama watu wangetoka barabarani, hakuna hatua za kimfumo za kufuatilia matokeo na kutekeleza mpango wenye tija ili kulinda maslahi na haki za watu wote.

Embu fikiria maandamano yamefanikiwa. Unafikiri nini kitatokea? Ngoja nikudokeze kwa sehemu nini kitatokea
a) Mauaji na visasi kwa viongozi wa serikali.
b) Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwani viongozi nao watakuwa wanajitetea kwa kutumia pesa zao na ikiwezekana kukimbia nchi.
c) uhalifu wa kuiba kwenye mabenki, kuchoma mali za matajiri maarufu waliokuwa wanasapoti mfumo.
d) Wageni na watu jamii ya wahindu na waarabu na machotara watakuwa kwenye wakati mgumu sana. Kwani baadhi ya waandamanaji wana mtazamo kuwa wao ndio wanaiba mali za hii nchi.

e) Kutokuwa na political stability hasa kujua nani anashika nchi kwa muda. Kama ni jeshi nani atashika nafasi hiyo ukizingatia mpaka sasa jeshi lipo upande wa serikali

6. Propaganda zenye kuleta machafuko kati ya Raia na wanajeshi. Kuna propaganda mbili zimetolewa kuhusu majeshi.
a) Majeshi ya Uganda yameingia Tanzania ili kuwapiga watanzania.
b) Majeshi ya Zanzibar yapo bara ili kuwapiga Watanzania.

Propaganda hizo lengo lake ni kuwapiganidha wananchi na wanajeshi. Kwamba wananchi wa Tanzania bara siku ya maandamano ikitokea wamepigwa na polisi au wanajeshi wasishangae kwani hao askari sio watanzania wenzao.

Hivyo wapambane kufa kupona kwani wanatetea nchi yao dhidi ya uvamizi wa majeshi ya nchi nyingine.

Propaganda hii ingepaswa itolewe siku moja kabla ya maandamano ili kuchochea chuki na hasira ili Lengo la mange kimambi lifikiwe. Lakini halitafikiwa kwa sababu limetolewa wakati ambao sio sahihi ambapo serikali inaweza kuipotosha taarifa hiyo.

Lakini pia kusema kuna wanajeshi kutoka Uganda wamekuja Tanzania ni kulifanya jeshi la nchi liwe macho na kufuatilia kama ni kweli. Kama sio kweli Jeshi hata kama lingekuwa na mpango wa kuunga mkono maandamano mpango huo utafeli.

Kufikia hapo sina la ziada.

Nawatakia Sabato Njema.

Taikonmaster
Kwa sasa Dar es Salaam
 
Mwenzio ana maoni tofauti huku.

MANGE KIMAMBI NA MARIA SARUNGI WAMEHUSIKA KUHUJUMU MAANDAMANO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kukosa Uongozi wa Kitaalamu na Kimaadili

Watu wenye tabia ya kuropoka au kutumia lugha ya matusi mtaani na mitandaoni mara nyingi hukosa uaminifu wa kijamii.
Wafuasi wanaposhuhudia matusi, kejeli, au hasira zisizodhibitiwa, hamasa hubadilika kuwa utani au hofu.
Kwa mfano:

Mange Kimambi amekuwa akitumia lugha kali dhidi ya watu tofauti, matusi ya nguoni hii imewafanya baadhi ya wafuasi na watu kumwona kama msemaji mwenye hasira na asiye na maadili badala ya kiongozi wa mabadiliko.

Uongozi wa maandamano unahitaji hekima, nidhamu, na heshima ya hoja; si kelele za hasira na matusi.

Kiongozi ambaye anaendana na culture ya jamii husika. Kutumia matusi mitandaoni na kutukana watu bila kujali ni mkubwa au mdogo inapunguza ushawishi wa mtu kwenye mambo ya maana.

2. Kuitisha Maandamano kwa Muda Mrefu (Zaidi ya Miezi Miwili)

Haya ni makosa ya kimkakati. Hili nilieleza kwenye post za nyuma.
Maandamano ni kama moto kwenye nyasi au mabua. ukichelewesha kuwasha, moto unazima kabla hujawasha kiberiti.
Watu hupoteza:
hamasa,
imani,
na kipaumbele (kwani maisha yao ya kila siku yanahitaji kuendelea). Na vipaombele vinabadilika. Zaidi ya yote unampa adui (ambaye hapa ni serikali) kujipanga namna ya kuyadhibiti.

3. Kukosa Muunganiko na Viongozi wa Ndani (Ground Movement)

Maandamano yenye mafanikio huhitaji muungano wa ndani: vyama, viongozi wa kijamii, wanafunzi, wafanyabiashara, wajasiriamali n.k.
Viongozi walioko nje ya nchi, na wanaharakati kama Mange, hukosa:
a) kugusa uhalisia wa hofu za wananchi.
Ukiwa nje ya nchi ukawa kiongozi wa maandamano hasa kwenye nchi kama Tanzania kisaikolojia utaonekana wewe sio mmoja wao. Ila unawasakizia wenzako.
na kuwajibika moja kwa moja iwapo vurugu au hatari ikitokea.
Matokeo yake wananchi wa ndani ya nchi hawaoni uhalisia wa uongozi huo, bali wanaona mtu aliyekimbia nchi anawaambia wapambane yeye akiwa salama.

4. Kuchonganisha Taasisi za Ulinzi (Jeshi na Polisi)

Uongozi wa maandamano unahitaji mkakati wa kisaikolojia na diplomasia.
Kusema maneno yanayochonganisha jeshi, polisi, au taasisi za dola ni sawa na:

a) kuamsha tahadhari za usalama,
Hapa ni sawa na kushawishi jeshi liasi na lipindue serikali kwa kudhibiti Polisi. Hivyo serikali lazima ichukue tahadhari kubwa kukabiliana na uchonganishi huo.

b) kupunguza uhalali wa maandamano,
Kupindua serikali ikiwa ni sehemu ya agenda za kuandamana kabla hata ya maandamano automatically yanapoteza uhalali.
Hata kama kungekuwa na mpango wa kuipindua serikali haikupaswa usemwe waziwazi hivi. Ingepaswa ifanyike wakati maandamano yanafanyika na yamekolea.
Kutaka kupindua serikali ni kosa la uhaini.

c) Kutoa nafasi ya serikali kutumia nguvu kwa uhalali wa kisheria.
Hivyo, badala ya maandamano kuwa sauti ya umma, yanaonekana kama uchochezi wa kuvuruga amani.

5. Kufeli kwa MANGE zaidi ya mara mbili katika kuhamasisha maandamano.
Kwenye siasa na utawala kuna msemo usemao Once a loser, Always a Loser.
Ukikubali kushindwa mara moja kwenye siasa upo kwenye nafasi ya kushindwa daima. Hiyo ni kanuni. Ndio maana kwenye siasa ukiingia lazima uwe na hesabu kali hasa kwenye pigano au pambano la kwanza kwa sababu hilo ndio limebeba msingi wako. Unaweza mtazama Raila Odinga, Edward Lowasa na wengineo.
Mange kimambi tayari anarekodi ya kushindwa kuhamasisha maandamano zaidi ya mara mbili.
Hakupaswa kwenye maandamano haya awe kinara. Yeye angetakiwa atokee pembeni.
Kuongozwa na kiongozi aliyeshindwa kwenye siasa lazima ushindwe tuu. Labda muujiza utokee lakini siasa hazitegemei mara nyingi miujiza.

6. Kukosa Mkakati wa Baada ya Maandamano.

Wengi hushindwa kujibu swali rahisi:
“Baada ya maandamano, tunataka nini hasa, na tutafikaje huko?”

Mara nyingi viongozi na wanaharakati wengi wenye kelele zaidi mtandaoni hawana mpango wa kisera, mikakati, bali huongozwa na mihemko na matumaini hewa kwa kujidanganya.

Hivyo, hata kama watu wangetoka barabarani, hakuna hatua za kimfumo za kufuatilia matokeo na kutekeleza mpango wenye tija ili kulinda maslahi na haki za watu wote.

Embu fikiria maandamano yamefanikiwa. Unafikiri nini kitatokea?
Ngoja nikudokeze kwa sehemu nini kitatokea
a) Mauaji na visasi kwa viongozi wa serikali.
b) Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwani viongozi nao watakuwa wanajitetea kwa kutumia pesa zao na ikiwezekana kukimbia nchi.
c) uhalifu wa kuiba kwenye mabenki, kuchoma mali za matajiri maarufu waliokuwa wanasapoti mfumo.
d) Wageni na watu jamii ya wahindu na waarabu na machotara watakuwa kwenye wakati mgumu sana. Kwani baadhi ya waandamanaji wana mtazamo kuwa wao ndio wanaiba mali za hii nchi.

e) Kutokuwa na political stability hasa kujua nani anashika nchi kwa muda. Kama ni jeshi nani atashika nafasi hiyo ukizingatia mpaka sasa jeshi lipo upande wa serikali

6. Propaganda zenye kuleta machafuko kati ya Raia na wanajeshi.
Kuna propaganda mbili zimetolewa kuhusu majeshi.
a) Majeshi ya Uganda yameingia Tanzania ili kuwapiga watanzania.
b) Majeshi ya Zanzibar yapo bara ili kuwapiga Watanzania.

Propaganda hizo lengo lake ni kuwapiganidha wananchi na wanajeshi.
Kwamba wananchi wa Tanzania bara siku ya maandamano ikitokea wamepigwa na polisi au wanajeshi wasishangae kwani hao askari sio watanzania wenzao.
Hivyo wapambane kufa kupona kwani wanatetea nchi yao dhidi ya uvamizi wa majeshi ya nchi nyingine.

Propaganda hii ingepaswa itolewe siku moja kabla ya maandamano ili kuchochea chuki na hasira ili Lengo la mange kimambi lifikiwe. Lakini halitafikiwa kwa sababu limetolewa wakati ambao sio sahihi ambapo serikali inaweza kuipotosha taarifa hiyo.

Lakini pia kusema kuna wanajeshi kutoka Uganda wamekuja Tanzania ni kulifanya jeshi la nchi liwe macho na kufuatilia kama ni kweli. Kama sio kweli Jeshi hata kama lingekuwa na mpango wa kuunga mkono maandamano mpango huo utafeli.

Kufikia hapo sina la ziada.

Nawatakia Sabato Njema.

Taikonmaster
Kwa sasa Dar es Salaam
Wewe ndiyo Mropokaji mkuu na mnafiki, unataka uonekane upo sawa kila sehemu, you have to choose your side, praising dictators or against these oppressors. Wewe unataka uwe kote.

Nyie ndiyo wasaliti, hili bandiko lako umetumwa uwakatishe tamaa watia nia wa maandamano.

Wewe ni among hao wasaliti

Full stop
 
We mtibeli sikuhizi unavuta bange?

Swali halihusiani na mada, hoja zako zimenyooka na ndo ukweli, ila nakuuliza kama unavuta bange maana hueleweki unaandamana au hauandamani , siku zote umekua unapiga mikwara humu sahivi unaona siku zinakaribia unaanza ku withdraw

Mara useme mke wako kakukataza au ndo uoga kama yule mnyama ambae ni chakula cha mamba yaani nyumbu?
 
Watanzania 99% ni wapumbavu wanaotumika kama vibaraka wa ccm nilishasema sana kuwa hamna mapinduzi ya kisiasa yatakayoletabadiliko Tz bali mapinduzi ya kijeshi na kijamii kupitia mikono ya wananchi wenyewe na siyo chama cha upinzani au kundi la wanafiki.
 
Nje ya mada, hivi Robert ulisemaje kama serikali/mahakama isingemuachia Lissu huru by mid September? Did it work?

Kama ukichunguza, utagundua kuwa yawepo au yasiwepo hayo maandamano, the message is sent and delivered! Badala ya kunadi sera, wapo busy kutisha watanzania.
 
Wewe ndiyo Mropokaji mkuu na mnafiki, unataka uonekane upo sawa kila sehemu, you have to choose your side, praising dictators or against these oppressors. Wewe unataka uwe kote.

Nyie ndiyo wasaliti, hili bandiko lako umetumwa uwakatishe tamaa watia nia wa maandamano.

Wewe ni among hao wasaliti

Full stop

Kumbe ukweli haufai hata kwa waandamanaji?
Nilidhani ni serikali tuu haipendi ukweli kumbe hata upande wenu?

Unataka tujadili ushabiki(upande) au tujadili hoja nilizoweka?

Sikutegemea kama hata upande wenu hampendi kuambiwa ukweli
 
Kaka yanaweza yasitokee hiyo tarehe 29 ila 2030 hatufiki broo ,kinaamka hii nchi ,watu wamechoka sana tena sana!!!maana tunakoelekea siko kuzuri kabbisa yaanii wakipita kwenye uchaguzi watatushika pabaya mnoo na hali zitakua ngumu hapo ndipo kitaamka kweli kweli
 
Nje ya mada, hivi Robert ulisemaje kama serikali/mahakama isingemuachia Lissu huru by mid September? Did it work?

Haikufanya kazi
Kama ukichunguza, utagundua kuwa yawepo au yasiwepo hayo maandamano, the message is sent and delivered! Badala ya kunadi sera, wapo busy kutisha watanzania.

Hayajafanya kazi.
Lengo la maandamano
1. Kuzuia uchaguzi
2. Kufanya reforms kwenye tume ya uchaguzi na ikiwezekana katiba mpya.
3. Kupigania haki za. Watu wasitekwe.

Tangu maandamano yahamasishwe kipi kati ya hayo mambo au mengine kimebadilika mpaka useme the message was sent and delivered?
 
We jamaa huwa nakukubali sn ila khs hli la maandamano aisee umekuwa mpuuz sn mara leo upo una support maandamano, mara kesho umejtoa kwmb ww si mbuz wa kafara, keshokutwa oooh maandamano hayapo yamehujumiwa kwan ukikaa kimya unapungukiwa nn bnafs nimechoshwa na thread zako khs maandamano kama umelambshwa sukari ili ulete porojo huku jf na kichaa pascal mayala aisee mtukome.
 
Kaka yanaweza yasitokee hiyo tarehe 29 ila 2030 hatufiki broo ,kinaamka hii nchi ,watu wamechoka sana tena sana!!!maana tunakoelekea siko kuzuri kabbisa yaanii wakipita kwenye uchaguzi watatushika pabaya mnoo na hali zitakua ngumu hapo ndipo kitaamka kweli kweli

Ni kweli.
Nilichoandika kwa namna nyingine ni way forward kwa wakati ujao kuwa siku nyingine lazima pawepo na watu wenye maana au maadili kama Tundu lisu ambaye sasa yupo gerezani au Heche, na sio watu hali iwepo na mikakati ya maana.
Kabambe ijulikane kete ya kwanza mpaka ya mwisho ya kusogeza ili kufanikisha lengo.

Lakini mambo yakiendelea hivi. Mkuu nakuhakikishia tutaenda hivihivi hata miaka mia moja.

Huku kuna ushabiki.
Kuna uccm na uchadema wakati haki inatakiwa kupiganiwa ya watu wote.
Huko CCM sio wote wanatabia mbovu.
Na huko Chadema sio wote ni waadilifu.

Wewe unaitisha maandamano, badala upiganie haki labda haki sawa ya vyama vya siasa. Wewe unapigania ili ufute ccm unafikiri ccm watakubali?

Huko ccm kwenyewe sio kwamba wanakubaliana lakini akija adui wa nje lazima wakubaliane kumkabili. Huo ndio ugumu ambao wahamisha maaandamano au kupigania haki wanakosea kupambana na ccm badala ya kutetea haki zao.

Ni sawa na wanawake wafanye harakati kupambana na wanaume na kupindua nafasi za wanaume badala ya kupambana wapate haki zao. Hapo lazima mkwamo uwepo.
 
We jamaa huwa nakukubali sn ila khs hli la maandamano aisee umekuwa mpuuz sn mara leo upo una support maandamano, mara kesho umejtoa kwmb ww si mbuz wa kafara, keshokutwa oooh maandamano hayapo yamehujumiwa kwan ukikaa kimya unapungukiwa nn bnafs nimechoshwa na thread zako khs maandamano kama umelambshwa sukari ili ulete porojo huku jf na kichaa pascal mayala aisee mtukome.

Unataka nikae kimya wakati najua unaenda kushindwa?
Nakuambia wanaokuhujumu unaniona tena mimi mbaya?
Huoni kama unahujumiwa? Huoni hilo?
 
Congenital hypocrite

Tatizo unalolalamikia kwa hao Watesi wako ndio hilohilo ambalo uko nalo.
Hutaki ukweli!
Hutaki kuambiwa ukweli!

Alafu muda huohuo unailaumu serikali kwa kutotaka kuambiwa ukweli.

Sasa tofauti yenu ni ipi? Au kipi unapigania?
Hutaki maoni ya wengine?
Lakini unaiambia serikali iachie uhuru wa maoni. Uko sawa kweli?
 
Rangi yako halisi haijulikani, hakika unatambulika na kufananishwa na kinyonga katika harakati za ukombozi. Siku si nyingi utapitia maandishi yako na kujutia UVUGUVUGU wako.

Siku ukijua rangi yangu halisi utafanikiwa kile unachokipigania.

Kwenye vita wenzako wanaangalia uhalisia sio mihemko na matamanio yao.
Uhalisia ndio utakufanya uwe na mipango na mikakati halisi ya kufanikisha.

Turudi kwenye hoja.
Kipi nimeandika unaona hakipo sawa. Labda tunaweza kujadili bila kutanguliza mbele hisia za maumivu na kile unachotamani kitokee
 
Back
Top Bottom