Come out brother. You may share what u know abt him...
Remember, am taking no side.. Am just naming the devil I know things about!
Don't forget to go to kichwapanzi to see how Mange is being exposed. Apparently her brother in law is one of the biggest drug dealers in Tanzania, and somehow she failed to mention this in her many attacks on drug dealers. Double standard much!!!
jMali
Ndugu, ukitaka maelezo mengi yapo! Na kwa kuwa umeamua kutumia NUKUU za Mwalimu, nadhani ni busara kukupitisha humo humo!
Najua kwa kuwa umesoma soma na kufuatilia siasa kwa muda mrefu, bila shaka umeshakutana na maneno haya ya Mwalimu;
"Hapa hatuchagui mtu maarufu, tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa.
Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa mgombea wetu".
Unaizungumziaje hiyo chief?
"Niko tayari kurudisha kadi yangu ya chama, CCM sio baba yangu wala mama yangu. Kuna wagombea wana uchu sana wa kwenda Ikulu. Mimi nimekaa pale ikulu kwa miaka 25. Ikulu si mahali pa kupakimbilia, ni mzigo. Ukiona mtu anakimbilia ikulu ujue huyo ni wa kuogopwa kama ukoma hasa anapotumia pesa. Je amepata wapi hizo pesa na atazirudishaje?". Mwl JK Nyerere, 1995.
jMali, Suala la huyo unayemtetea sasa, halitokei kwa bahati mbaya. Ni mkakati wake wa muda mrefu wa kujisafisha na kutengeneza good impression kwa kutumia pesa aliyonayo. Tumeona mambo mengi ambayo yalikuwa hayawezekani lakini yamewezekana kwa nguvu ya pesa. Mfano mdogo tu, itazame CDM ya leo.
Wewe pengine huna hata maslahi yeyote, lakini kwa kuwa 'umetekwa' na mkumbo wa mambo yanavyoenda, unajikuta unaimba na kucheza ngoma usiyoijua. Ni halali kusema kwamba jamaa ni mchafu na ana wachafu wenzie waliopo CCM, lakini sio kukataa katu katu. Yaani unakuja kabisa hapa kwa ujasiri kusema jamaa 'anaonewa, anasingiziwa'???. Duh! Pole sana!
JF ina taarifa nyingi mno. Nakupa muda kidogo upitie huu uzi kisha urudi hapa. J. K Nyerere: 'Malecela na Lowassa hawafai urais Tanzania'
1. Kwanza hiyo nukuu yako imechakachuliwa. "CCM sio mama yangu imetokea kwenye hotuba nyingine" na hiyo ya "ukoma" imetokea kwingine. Kwa nini umechanganya? Halafu hata hizo hotuba umechagua sentensi ukaungaunga, hakusema hayo kwa mtiririko huo ulioandika. Hii inaonyesha viwango ambavyo watu wako tayari kwenda ili kumchafua Lowassa. Na hotuba zote hizo hazijamlenga Lowassa bali alikuwa anatuusia watanzania wote in general.
Sijui kwa nini mnadai inamlenga Lowassa wakati Lowassa huyu huyu akaendelea kuwa waziri kwenye serikali iliyofuata na waziri mkuu kwa wakati wa Kikwete. Ina maana CCM walimpuuza Mwalimu?
Lakini angalia, katika hotuba ya "wa kumkwepa kama ukoma". Mwalimu aliuliza "ikulu pana biashara gani mpaka mtu akope"? Ironically, tunamjua aliyegeuza Ikulu kuwa ofisi yake ya kibiashara na kukopa mamilioni toka benki alizokuwa anazibinafsisha!! Huyo huyo alijibinafsishia mgodi wa taifa yeye na wanae na wakwe zake.
Cha ajabu wewe huoni ubaya wa mtu huyu kuwa anampigia kampeni Magufuli leo hii, ila unaona ubaya wa Lowassa ambaye amehama chama hicho kibovu! Hivi kweli unadhani Magufuli ambaye tayari ameshampigia kampeni Andrew chenge na watuhumiwa wengine kama Ngeleja, ndie ataleta mabadiliko kwa chama cha CCM? CCM wenyewe wanaimba "CCM ni ile ile" wewe unataka kuipigia kura? Punguza mahaba.
2. Hotuba ya "mabadiliko nje ya CCM" ilisema wazi kuwa wananchi wamechoka rushwa, je tukipima idadi ya madili yaliyopigwa baada ya Lowassa kuondoka huoni kuwa tatizo sio lowassa bali mfumo? Lowassa ni kweli alikuwa part of old system, lakini sasa amebadilika na kuwa sehemu ya new system. Mimi nitamchagua lowassa kwa hilo. Urais sio mtu mmoja ingawa mtu ni muhimu, urais ni ujumla wa chama. Sisemi Lowassa ni malaika ila compared to CCM nitachagua 'shetani' mwenye afadhali.
Uwe unaona aibu basi mzee wangu. Hata kama una mahaba, learn to accept, sio upingane nao, utakuhadhiri. Usiwe kama huyo mzee unayempigia debe aliyekataa kwamba ni mgonjwa, lakini anaumbuka kujinyea majukwaani..
Back to the topic, pamoja na kuruka ruka kama bisi mzee wangu, nimefurahi kuona hujakanusha kwamba hayo maneno sio ya Nyerere. Yawe yametolewa nyakati tofauti, lakini msg ni ile ile..
Kwa kuwa umeshatangaza msimamo kwamba utampigia kura shetani wako, basi kila la heri..
1. Nukuu hiyo imetolewa lini na wapi? Mimi nukuu zangu unaweza kuthibitisha anytime kwa kwenda kwenye archives za magazeti niliyotaja na tarehe zake, wewe hii ya kwako ilitolewa lini na kwa uthibitisho gani?
2. Tukichukulia kuwa ni kweli hayo ni maneno ya mwalimu. Mwalimu mwenyewe anafananisha tuhuma za Lowassa na tuhuma za mke wa Kaisari ambazo zilikuja kubainika kuwa sio za kweli. Mara baada ya kukatwa hiyo 1995, Lowassa aliteuliwa na chama hicho hicho cha CCM kuwa mbunge wa Monduli, aliteuliwa kuwa waziri wa Benjamini mkapa, aliteuliwa kuwa waziri mkuu na kikwete, aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje bungeni na vyeo vingine.
Je huoni kuwa CCM yenyewe ilishamsafisha na hizo tuhuma kama mke wa kaisari alivyosafishwa? Unazungumziaje hiyo? Au vyeo vyote hivi alivinunua? Mke wa kaisari aliadhibiwa mara moja tu kwa tuhuma za uongo, lakini sio kwamba everytime akitaka kuolewa hoja ya tuhuma inaibuka wakati ilishathibitika kuwa ni uongo.
Lowassa alishaadhibiwa kwa kukatwa 1995 kwa tuhuma hizi za uongo, kwa nini everytime akatwe kwa kitu kile kile ambacho kimeshathibitika kuwa ni uongo? Hakuna sehemu yoyote mtu anaweza kuthibitisha utajiri wa Lowassa ni tofauti na utajiri wa wanachama wengine wa CCM, lakini baadhi yetu tunaamini tu kuwa Lowassa ni tajiri mkubwa kwa sababu tumekuwa tukiambiwa hivyo since 1995.
Lakini please kumbuka kujibu hilo la kwanza la muda, sehemu na uthibitisho wa mwalimu kusema hayo. Maana nukuu za mwalimu ambazo ziko VERIFIED hazina ubaya wowote kwa Lowassa, isipokuwa hizi za "mwalimu alisema" ambazo mnazo nyie tu!
Anayetakiwa kuona aibu ni wewe kijana usiyejitambua, unaphotoshop mpaka maneno ya Nyerere ili kumpaka Lowassa? Ukichukua hela ya watu angalau uwe unafanya basi research kidogo tu ili kazi yako ya propaganda iwe na mashiko. Hivi kwa mtu anayetusoma malumbano yetu hapa unadhani atakubaliana na wewe?
We jamaa ubishi umesomea wapi nami nikajifunze!? Kuna videos All Over zinazoonyesha namna Mzee akiwa ana mcrash Lowassa, au ulitaka atajwe kwa jina? Huwezi kupima Time & Relevance?
Let's say kwamba maneno ya JKN yalikuwa ni usia kwa Watz wote, Lakini mbona sifa nyingi zinamwangukia huyo Mzee EL? Utajiri wake wa miaka mingi usiojulikana chanzo sio ishu kubwa kwako? Support anayoipata kutoka kwa 'marafiki' wasiojulikana haikutii wasiwasi? Pesa anazotawanya kuanzia akiwa CCM mpaka kukatwa zinatoka wapi?! Kumbuka he's branding himself as an institute..
Kama ni kweli alikuwa anapendwa mpaka na kundi kubwa la watu wa NEC, kwanini amekatwa? Hiyo nuksi gani ya kukatwa tangu 1995???!
ACT YOUR AGE!
Kwahiyo hayo maneno ni yangu, sio ya Nyerere. Duh!
Jibu swali, kwanini mzee wenu ana gundu la kukatwa tangu 95!? Ushaambiwa kama unampenda sana, kapige naye picha!
Hahahah!
Kuna siri gani kati yake na Mzee Kingunge? Je, kati yake na Serukamba!?
Huna ushahidi kuwa Nyerere kasema hayo acha uongo. Na kama kukatwa 95 hata kikwete si alikatwa? so what? Is he the first kukatwa mara mbili ? Mbona mnamfuatafuata?
Hahaha, kijiweni kwenu we ndio wanakutegemea nini? Nimekubishia with facts, wewe unanibishia kwa empty words, hizo video za Nyerere mbona huzileti hapa? Najua huzileti kwa kuwa ni wewe peke yako ndio unayezitafsiri kuwa aliyekuwa anasemwa ni Lowassa!
Halafu mbona hujibu uadilifu wa hao wazee wako ninaowataja? Unajifanya kama huoni vile. Jibu mambo ya Mkapa, Kikwete, Kinana, Iddi Simba (UDA), Prof Kapuya, Ngeleja, Maige, Madabida, Chenge,...hawa wote na wengine wengi BADO WAPO CCM, na ndio watakaomsimamia Magufuli kwenye serikali ijayo!
Hao WAMESHAFANYA yote ambayo Mwalimu ametuonya against kwenye hotuba zake, lakini wewe bado unaona hatari kwa mtu kumchagua Lowassa atakayesimamiwa na kina Halima mdee na John Mnyika?
Wakati unatafuta hizo video zinazomuonyesha Nyerere anasema Lowassa fisadi hebu angalia mwenyewe hizi video nilizopata mimi. Unaona CCM walivyoreact baada ya Lowassa kukatwa? Mwenye akili anajua kuwa wako CCM wengi kama hawa ambao 'kula' iko CCM hivyo hawawezi kuhama lakini 'kura' iko kwa Lowassa. Kama amekatwa na wao wanamuimba kuwa wana imani naye, is it not obvious watamchagua nani Oct 25? ACT YOUR AGE!
Mzee wangu, ni vile tu nakuheshimu kwa sababu you sound too way matured. I can tell from your choice of words.. Lakini sasa nitafanyaje na umeamua kujitoa ufahamu? Ngoja nikuweke sawa.
Kwanza, videos zipo all over youtube and elsewhere. Nyerere alikemea kuomba kura kwa misingi ya udini, Huyo Mlutheri anakuja kuyafanya hayo makosa 2015. Ni mzima kweli?
Nyerere alitahadharisha kuhusu mgombea anayeng'ang'ania kwenda Ikulu, hususani kwa kutumia fedha nyingi. Tumeona wazi wazi jinsi huyo 'mgonjwa' anavyotumia mapesa mpaka ya akina Rost na the invisible kusaka Ikulu. Hii haikushtui?!
Unashangaa ya Wajumbe wa NEC kuimba tuna Imani na Lowassa, halafu unaacha kumshangaa Kikwete anavyosindikizia na makofi juu?
Angalau hao wanaoimba wameamua 'kumfurahisha mfalme' kwa kuwa wanatumikia ----- mshahara wao upande. Wewe Je?!
Umebashiri Kura watampa? Hahaha! Kura ni siri mkuu... Hapo watu 'wamefanya' kazi yao. Mbona wakina Sophia Simba na Nchimbi mpaka sasa wapo kwenye Kampeni na wakati wao ndio walionyesha kiburi cha waziwazi?! Hela tamu mzee wangu!
Simshangai Mbowe kuuza chama, ni mjanja na ameshapiga hesabu ndefu za kushinda majimbo na mkwanja juu. Anajua ilivyo ngumu kushinda Urais kwa kumtumia huyo mzee, lakini atafanyaje sasa na Mbuzi kajileta mwenyewe kwa muuza supu!?
Would you like to read this 'Fake' email Dad?!
View attachment 291522
Or you want to read this thread started on 2011?!Mbowe aiuza CHADEMA kwa Lowassa
Or you're still interested in videos za JKN?!
Nakushauri, punguza matarajio. This time around u guys have made it easier for CCM to win than how it was in 2010.. Swallow that!!!
#TukutaneOktoba
Kwanini akatwe? Hili swali mbona unalikwepa? Sababu alizopewa Kikwete na Lowassa zinafanana? Kwanini JK ameshindwa 'kumtetea' swahiba wake?! JK ni zaidi ya umuonavyo, hili dada yangu FaizaFoxy analijua zaidi and that's what it really takes for a person to be a leader. No friendship when it comes to National Matters. Jamaa alitaka kuleta uswahiba kwenye kupeana 'Ikulu' kama urithi wa ng'ombe za kimasai.. Nyambaaf!
Yaani ningeshamshangaa sana endapo JK angeendelea kumchekea mtu aliyefanya hujuma kumharibia legacy pamoja na kumzawadia kote kule nafasi ya U-PM... Ama kweli, Wafadhilaka wapundaka!
Haahaha! Au jamaa ana nyota ya Mkasi?!
Jmali asante,,naona Mange a.k.a interest kaelewa. Ila mkuu mnakuwaga wapi mnawaachia hawa kina Polepole wanapotosha watu???
1. Aha, naona taratibu dawa inaanza kukuingia, unaanza sasa kuondoka kwenye madai yako ya kuwa mwalimu alimsema Lowassa specifically na unaanza reference kwa video kama za udini ambazo mwalimu aliongea generally. Safi kabisa. Sasa tuje kwenye huo udini wa Lowassa. Video mimi nimeiona na wewe najua unaijua. What did Lowassa say exactly ambacho wewe unaona ni udini? "niombeeni kwa kuwa mimi ni mlutheri mwenzenu"? Sasa hapo mzigo si anatupiwa Mungu? Shida iko wapi? Angesema nipigieni kura kwa kuwa mimi mlutheri mwenzenu hapo sawa, ingekuwa udini. Hivi ni mgombea gani hajaenda/hataenda kuombewa/kuswaliwa kwa imani ya dini yake kufanikisha uchaguzi wake? Lowassa ni mlutheri, yuko kanisa la walutheri, anaomba AOMBEWE kwa mungu wa kilutheri, tena aombewe sana wewe unasemaje udini hapo? Hilo mme-exaggerate kupitiliza. Hebu kataa kuwa Magufuli hatafanya (kama bado) maombi/sala kwa mujibu wa imani yake ili ashinde halafu ndio useme Lowassa mdini kwasababu kawaomba wa dini yake wamsalie!
2. kwenye matumizi ya pesa: Tunarudi pale pale, mwenzetu wewe ulilipwa na Lowassa? Ushahidi wako uko wapi kuwa Lowassa anatumia fedha zake? Najua huwa hunaga ushahidi dhidi ya Lowassa. So let me ask you this. Do you know where Magufuli's campaign money comes from? Je huoni hata kwa macho kuwa kampeni ya Magufuli ina fedha nyingi kuliko huyo Lowassa unayedai ana mapesa?
Pili, unamu associate Rostam na Lowassa, lakini sijui umesahau au unafanya makusudi kukumbuka kuwa Rostam alikuwa MWEKA HAZINA wa kampeni za JK 2005 na MWEKA HAZINA WA CCM (2007-9). Unajifanya hujui kuwa waliokuwa wafanyakazi wake kama Salva Rweyemamu (Richmond) alipewa cheo cha msemaji wa Ikulu, William Ngeleja (vodacom) akapewa uwaziri na anagombea tena kupitia chama unachokitetea...Sasa kuna shida gani kama akimpa fedha Lowassa wakati CCM wenyewe hawajawahi kuona ubaya wake?
3. Asante kwa kuniunga mkono kuhusu kina Sophia Simba, naona umekubali kuwa hela ni tamu na kwa kuwa 'kula' yao iko CCM basi wameufyata in public. Sasa sijui unataka kumconvince nani kuwa Nchimbi na Simba mioyo yao iko CCM. Magufuli mwenyewe nadhani umeshamsikia akisema anajua ndani ya timu yake kuna team Lowassa, that's the bitter truth! Swallow that!
4. Nimepost references toka magazeti mbalimbali, nimeposti videos, wewe umeposti nini cha maana zaidi ya hotuba za kuchakachua na kunielekeza youtube pasipo na link hata moja? Kupost kwako hicho ki graphic unachokiita email kinanifanya nikubali tu wewe uniite mzee pamoja na kwamba bado hata sijaoa! Clearly mi sio saizi yako!