Mangi Mkuu Thomas Marealle katika nyaraka za Sykes

Mangi Mkuu Thomas Marealle katika nyaraka za Sykes

Fizi...
Huko tulikotoka katika mada hii ilikuwa wachangiaji wakiingia hapa kwa ghadhabu kubwa wakati mwingine wakitukana na kutoa vitisho.

Hii ni kiasi cha kama miaka 10 iliyopita.
Lakini taratibu imewadhihirikia kuwa niandikayo ni kweli.

Hivi sasa somo limeeleweka kwa hiyo wachangiaji wamegeuka kuwa wasomaji wa kimya kimya.

Nina muda mrefu sijawaona Mag 3, Nguruvi na Mwanakijiji hapa ulingoni.

Hawa walikuwa wapinzani wangu wakubwa.
Ukimya nalo ni jibu
 
Kuna vijana naamini wamehamasika kutafiti na kuandika upya historia ya uhuru wa Tanganyika na kwa kweli nawapongeza na nawatakia kila la kheri katika juhudi zao hizi.

Nimesoma makala moja ya Mangi Chief Thomas Marealle kwa bahati mbaya nimekuta kuna baadhi ya mambo mwandishi hakuyafanyaia utafiti wa kina.

Nimemwandikia baadhi ya mambo kama njia ya kumgutua na kumtia moyo:

''...katika hili bandiko la Chief Marealle kuna mambo unahitaji kuyapitia upya ili ipatikane ithibati ya ulichoandika.

Nimebahatika kumsoma Chief Marealle katika Nyaraka za Sykes barua binafsi ambazo akiandikiana na Ally Sykes.

Kwa ajili hii basi nimeweza kufahamu hata kile alichokuwa anakiamini ndani ya nafsi yake katika uongozi wa harakati za kudai uhuru.

Kuna barua moja Chief Marealle alikuwa anamuonya Ally Sykes kumtahadharisha na hali ya baadae baada ya uhuru.

Marealle alifika UNO lakini hakuwa mjumbe aliyetumwa kuwawakilisha Watanganyika.

Kuna jina moja umealiandika la mwanasheria kutoka Bermuda "Earl Seymour," naamini ulimkusudia Earle Seaton.

Earle Seaton pia nimekutananae ndani ya Nyaraka za Sykes akiwa mshauri wa TAA kuhusu "mandate territories."

Earle Seaton ana historia ya kutukuka katika harakati za uhuru wa Tanganyika hasa kwa TAA.

Abdul Sykes katika taatifa yake ya mwaka wa 1950 akiwa Katibu wa TAA kamtaja Seaton kama mtu aliyetoa msaada mkubwa kwa Constitutional Development Committee.

Abdul Sykes, Earle Seaton kama mwanasheria na Japhet Kirilo akiwa kiongozi wa Meru Citizens Union walifanya kazi pamoja kufikisha tatizo la Ardhi ya Wameru UNO 1952 na Kirilo akazungumza UNO Seaton akiwa mkalimani wake.

Yapo mengi.

Hotuba ya Mwalimu Nyerere UNO 1955 inatokana na waraka wa TAA Political Subcommittee ambao ndani ya waraka huu kuna mchango mkubwa wa Seaton.

Waraka huu ulijadiliwa mwaka wa 1954 katika kuasisi TANU na ni mapendekezo yaliyowasilishwa na TAA Political Subcommittee kwa Gavana Edward Francis Twining mwaka wa 1950.

Ningependa kukufahamisha pia kuwa Chief Marealle na Abdul Sykes walikuwa marafiki wakubwa.

Abdul akimtania Marealle akimwita, "King Tom," akimwambia Waingereza wanakataa kumwita yeye King ili asifanane na mfalme wao King George.

Mwaka wa 1951 Chief Marealle alichaguliwa kuwa Rais wa Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) Ally Sykes akiwa Katibu na Rashid Kawawa, Dr. Wilbard Mwanjisi, Michael Lugazia, Steven Mhando wakiwa katika Kamati.

Yapo mengi ningeweza kukueleza lakini nakuomba pitia upya historia ya Chief Marealle.''

View attachment 1245766
Earle Seaton na Julius Nyerere
Huyu side anaandika historia inayohusu wenziwe kiimani baaasi,yuko biased kinoma,sisomagi vitabu vya side
 
Duh ajuza FaizaFoxy, nawaona vipofu bado mnaongozana mkilishana matango pori. Hizi ngano za Mohamed Said zimechuja na nyingi ni hadithi alizosimuliwa na wazee wake kibarazani mtaa wa Gerezani akiwa mtoto.

Hadithi, hadithi! Kaondokea chenjagaa, kajenga nyumba kakaa, mwanangu mwana siti, kijino kama chikichi, cha kujengea kikuta na milango ya kupita! Hadithi njoo, uongo njoo, utamu kolea!

Kama unaoga mtoni akatokea chizi akakwapua nguo zako na kutimua mbio una mawili...ama umkimbize au ujisetiri. Mimi nimechagua kutomkimbiza chizi, vipi nyie wenzangu?
 
Mag3, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Yericko Nyerere, Pascal Mayalla na juzi tu Ndinani.

Wote hao wana ahadi walizoahidi. Sasa ukishusha nondo namna hizi wanaona haya kutia lao, wataonekana, kwani ahadi ni deni. Lakini kwa uhakika wanakusoma.

Hawana njia bali wakubali tu kuwa wameshindwa kutimiza ahadi zao na wajitokeze tu. Japo wakupongeze tu panapostahili.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

"Wameingia mitini".
IMG_20190925_101307_780.jpg

Katika kitabu cha Ujasusi nimeeleza kwa usahihi historia ya Tanganyika kuanzia mwanzoni mwa 1927 enzi za kuundwa kwa AA, TAA, TANU na CCM, Nimefanya hivyo kama sehemu ya kujibu upotoshaji wa mzee wangu mwanahistoria nguli anayeudanganya umma kwa miaka mingi kuwa uislamu ndio ulileta uhuru wa Tanganyika.

Upatapo muda kisome hata kama unakereka na mwandishi wake..... Soma kisha njoo tujadili ewe bibi yangu mkuu
IMG_20190925_101307_780.jpg
 
Mag3,
Hakika wengi wangependa kama historia hii niliyoandika isingekuwa kweli na watu hawa niliowarejesha kwenye historia ya Mwalimu Nyerere, TANU na uhuru wa Tanganyika baada ya kufutwa wangekuwa hawakuwapo bali ni hadithi ya mtunga hadithi hodari.

Lakini watu hawa walikuwapo na wanafahamika na mmoja wa watu hawa ni babu yangu, Salum Abdallah ambae nimeeleza historia yake kwa ushahidi wa historia yenyewe na picha.

Daisy ameeleza historia ya baba yake wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika na katika kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo cha baba yake aliandika makala ambayo mimi nimeiandikia utangulizi.

Nakuwekea kipande cha makala hiyo na utangulizi wangu kukudhihirishia kuwa haya nikwaambiayo ni kweli:

BABA YANGU ABDULWAHID SYKES KAMA NINAVYOMKUMBUKA

1572344935130.png

Aisha ‘’Daisy’’ Sykes Buruku

Utangulizi

Aisha ‘’Daisy’’ Sykes Buruku ni binti ya Abdulwahid Sykes mmoja kati ya wazalendo 17 waliounda chama cha TANU kilichopigania uhuru wa Tanganyika.

Daisy kama anavyofahamika zaidi kwa jina hili, ni msichana wa kwanza Mwafrika kusoma Shule ya Wasichana ya Aga Khan mwanzoni mwa miaka ya 1950 na msichana wa pili kuingia Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam mwishoni mwa miaka ya 1960.

Daisy amefahamiana na wazalendo wengi mmoja wapo akiwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na machifu mashuhuri kama Mangi Mkuu Thomas Marealle waliokuwa wakifika nyumbani kwa baba yake wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Katika kuadhimisha miaka 50 ya kifo cha baba yake, Daisy ameandika makala haya kukumbuka siku zile zilizojenga haiba ya baba yake na ya wazalendo walioshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kwa miaka mingi Daisy amekuwa akiishi na kufanya kazi nje ya Tanzania:

''Juma moja kabla ya kifo chake nilimuuliza baba swali ambalo jibu alilijua lakini katika hulka yake ya kawaida ya kutopenda kujikweza hakutaka achukue sifa zote kwa ule ukweli na matokeo yake.

Wakati ule nilikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki Dar- es- Salaam na mwalimu wangu wa Historia Dr. John Iliffe kwa kutambua kuwa natoka familia ya Sykes waasisi wa mwamko wa siasa katika Tanganyika na mchango wa wazee wangu katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika alinitaka niandike mafanikio ya Watanganyika wa kizazi kile pamoja na historia ya babu yangu Abdallah Kleist Sykes.

Dk. John Iliffe alinitia moyo nifanya utafiti na kuandika historia hii na nilikubali kufanya hivyo.

Nilikuwa na swali kuhusu nani khasa walikuwapo katika mkutano na kushiriki wa kuibadili TAA kuwa TANU.

Baba akashauri kuwa tuombe miadi na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere ili anipe ukweli niliokuwa nautafuta na kusadikisha mambo mengine yanayohusiana na historia hiyo.

Hivyo tukaenda Msasani kuonana na Mwalimu Jumamosi moja asubuhi.

Kama ilivyotegemewa Mwalimu alifurahi sana kutuona maana ilikuwa muda mrefu watu hawa waliokuwa marafiki wakubwa sana kupata kuonana.

Mwalimu alitoa ushirikiano mkubwa sana kwangu kupata ukweli kutoka kwake katika yale niliyotaka kujua kutoka kwake.

Hii ndiyo ilikuwa siku yao ya mwisho kuonana.''
 
Attachments

  • SALUM ABDALLAH NA KASSANGA TUMBO.jpg
    SALUM ABDALLAH NA KASSANGA TUMBO.jpg
    76.8 KB · Views: 1
Yapo mengi ningeweza kukueleza lakini ...
Mkuu Maalim Mohammed Said, kwanza asante kwa mchango huu, wewe humu umekuwa ni iconic kwa baadhi yetu, mimi nikiwemo, kila bandiko unalobandika, najikuta navutwa kama sumaku na lazima nilisome, hivyo nakuomba uendelee kutupatia hayo mengi yoyote unayoweza kutupa, ni siishia humu tuu kwenye mabandiko yako ya jf, mara moja moja hukutembelea kule kwako www.mohammedsaid.com, sijui siku hizi kumeingiliwa na kirusi gani.

Moja ya sifa ya viumbe hao wote, sio static, ni dynamic, and hence they change with time, hata wewe. as times goes by, unajikuta una change with time, kwa siku hizi kutuletea mabandiko ya ukweli mtupu, na sio mabandiko yenye urongo kama urongo niliouibua hapa.

Hivyo kwenye historia ya ukweli, tuko pamoja sana, ila kwenye maurongo, kama ukweli tunaujua, hatutanyamaza.

Hilo andiko la Mangi Mkuu, Chief Thomas Marealle, sijabahatika kulisoma, ila kuna taarifa ambazo hazina uthibitisho kuwa Mangi Mkuu aliwaambia Wakoloni wetu Waingereza kuwa Tanganyika bado haijawa tayari kujitawala, ila North Province ndio wako tayari, hivyo kuwaomba watoe uhuru kwa mafungu, North Province ndio ipewe uhuru kwanza. Taarifa hii ilipomfikia Nyerere, ali curse kuwa never on earth mtu wa huko anaweza kuwa rais wa JMT!, japo hizi ni hearsay tuu, lakini political trends, na political dynamics za siasa zetu, zina onyesha ni kweli kuna makabila fulani fulani hayatakiwa kutoa rais wa JMT, na ni kweli sasa kuna chuki fulani ya kichini chini dhidi ya makabila fulani fulani!, huwezi amini kuna mtu fulani who was high ranking member wa utawala uliopita yuko mahabusu huu ni mwaka wa 4!.

Na sasa pia tuna makabila ambayo yanafaa sana kutoa rais
P.
 
Ahsante sanaa kaka kwa kunifundisha historia hii nimejifunza mambo ambayo sikuwahi kuyasoma darasani.
Mkuu Waterloo, jf ni zaidi ya darasa, zaidi ya shule, zaidi ya chuo, ni maktaba hai, na Maalim Mohammed Sais ni zaidi ya mwalimu, zaidi ya lecture, zaidi ya Prof, na hapa ndipo tunapoonyeshwa kuna ma prof wa Ph.D and they deliver nothing!, na kuna watu, hawana hata Masters, na wana deliver wonders.
P
 
Ukimya nalo ni jibu
Nguruvi 3,
Nakuongezea usemi mwingine.
Waingereza wana msemo: ''Silence is golden because it can never be repeated.''

Lakini hii kuwa ''ukimya nalo ni jibu,'' umelijua lini?
Nakuuliza kwa kuwa mimi na wewe tumefanya mjadala kwa kipindi kirefu sana.

Ukweli ni kuwa mimi nakujua wewe si mtu mjinga kwa kukosa kuutambua ukweli.

Najua kuwa hata wewe ndani ya nafsi yako unajiuliza sana kuhusu historia ya TANU kwani ushajua kuwa hiyo iliyoandikwa si historia ya kweli.

Majuzi hapa Mzee Pius Msekwa anasema ati TAA kilikuwa chama cha kushghulika na maslahi ya wafanyakazi Waafrika katika serikali ya kikoloni na kuwa Nyerere ndiye aliyewaambia viongozi wa TAA wakivunje ''chama chao,'' ili yeye aunde TANU.

Kwa ujanja kabisa Mzee Msekwa kakwepa kuyataja majina ya Abdul na Ally Sykes kwani hao ndiyo waliompokea Mwalimu nyumbani kwao na si kwa jingine ila wote waliunganishwa na kutaka kumuondoa Muingereza Tanganyika na kumaliza ukoloni.

Mwalimu hakuwatafuta wazalendo hawa ndugu kwa nia ya kujiunga na TAA kupigania maslahi ya walimu kani yeye alikuwa mwalimu wa shule.

Naamini jibu langu kwa Mzee Msekwa umeliona hapa Majlis.

Nimemjibu kuwa Mwalimu Nyerere TANU kaikuta nyumbani kwa Abdul Sykes na nimetoa ushahidi kupitia historia ya Chief Kidaha Makwaia ambae Abdul alikuwa na majadilanonae karibu miaka miwili kuazia 1950 - 1952 kuhusu kuunda TANU.

Je, Nguruvi 3 huamini historia hii?
Kati yangu na Mzee Msekwa ni nani aijuaye kwa kina historia ya TANU?

Mimi mjukuu wa Salum Abdallah niliyezaliwa na kukulia katika nyumba ya mpigania uhuru au yeye aliyeingia TANU ukubwani, mtu mzima?

1572348169466.png

Salum Abdallah anavishwa mgolole wa vita wa kuongoza mapambano dhidi ya Waingereza enzi za (Tanganyika Railways African Union) TRAU kama Mwenyekti kulia wa kwanza ni Kassanga Tumbo Katibu
 
Duh ajuza FaizaFoxy, nawaona vipofu bado mnaongozana mkilishana matango pori. Hizi ngano za Mohamed Said zimechuja na nyingi ni hadithi alizosimuliwa na wazee wake kibarazani mtaa wa Gerezani akiwa mtoto.

Hadithi, hadithi! Kaondokea chenjagaa, kajenga nyumba kakaa, mwanangu mwana siti, kijino kama chikichi, cha kujengea kikuta na milango ya kupita! Hadithi njoo, uongo njoo, utamu kolea!

Kama unaoga mtoni akatokea chizi akakwapua nguo zako na kutimua mbio una mawili...ama umkimbize au ujisetiri. Mimi nimechagua kutomkimbiza chizi, vipi nyie wenzangu?
Mag 3,
Labda huenda umenisahau:
  1. PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  5. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  6. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2019 Dar es Salaam.
  8. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  9. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  10. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  11. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  12. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  13. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  14. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  15. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  16. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  17. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  18. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  19. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  20. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
  21. Awards: Several Awards
  22. Visiting Scholar: (2011)
  23. University of Iowa, Iowa City, USA
  24. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
  25. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
  26. OTHER COUNTRIES VISITED
  27. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
Mkuu Maalim Mohammed Said, kwanza asante kwa mchango huu, wewe humu umekuwa ni iconic kwa baadhi yetu, mimi nikiwemo, kila bandiko unalobandika, najikuta navutwa kama sumaku na lazima nilisome, hivyo nakuomba uendelee kutupatia hayo mengi yoyote unayoweza kutupa, ni siishia humu tuu kwenye mabandiko yako ya jf, mara moja moja hukutembelea kule kwako www.mohammedsaid.com, sijui siku hizi kumeingiliwa na kirusi gani.

Moja ya sifa ya viumbe hao wote, sio static, ni dynamic, and hence they change with time, hata wewe. as times goes by, unajikuta una change with time, kwa siku hizi kutuletea mabandiko ya ukweli mtupu, na sio mabandiko yenye urongo kama urongo niliouibua hapa.

Hivyo kwenye historia ya ukweli, tuko pamoja sana, ila kwenye maurongo, kama ukweli tunaujua, hatutanyamaza.

Hilo andiko la Mangi Mkuu, Chief Thomas Marealle, sijabahatika kulisoma, ila kuna taarifa ambazo hazina uthibitisho kuwa Mangi Mkuu aliwaambia Wakoloni wetu Waingereza kuwa Tanganyika bado haijawa tayari kujitawala, ila North Province ndio wako tayari, hivyo kuwaomba watoe uhuru kwa mafungu, North Province ndio ipewe uhuru kwanza. Taarifa hii ilipomfikia Nyerere, ali curse kuwa never on earth mtu wa huko anaweza kuwa rais wa JMT!, japo hizi ni hearsay tuu, lakini political trends, na political dynamics za siasa zetu, zina onyesha ni kweli kuna makabila fulani fulani hayatakiwa kutoa rais wa JMT, na ni kweli sasa kuna chuki fulani ya kichini chini dhidi ya makabila fulani fulani!, huwezi amini kuna mtu fulani who was high ranking member wa utawala uliopita yuko mahabusu huu ni mwaka wa 4!.

Na sasa pia tuna makabila ambayo yanafaa sana kutoa rais
P.
P,
''Maurongo,'' ni yapi?
Weka hapa kwa faida ya wasomaji nikujibu kwa ushahidi.
 
View attachment 1247610
Katika kitabu cha Ujasusi nimeeleza kwa usahihi historia ya Tanganyika kuanzia mwanzoni mwa 1927 enzi za kuundwa kwa AA, TAA, TANU na CCM, Nimefanya hivyo kama sehemu ya kujibu upotoshaji wa mzee wangu mwanahistoria nguli anayeudanganya umma kwa miaka mingi kuwa uislamu ndio ulileta uhuru wa Tanganyika.

Upatapo muda kisome hata kama unakereka na mwandishi wake..... Soma kisha njoo tujadili ewe bibi yangu mkuuView attachment 1247610
Yericko,
Nifahamishe ikiwa kitabu chetu hiki kimefanyiwa ''review'' ningependa kusoma.
 
P,
''Maurongo,'' ni yapi?
Weka hapa kwa faida ya wasomaji nikujibu kwa ushahidi.
Mkuu Maalim Mohammed Said, hatuna haja ya kuliharibu bandiko hili zuri la Mangi Mkuu, Chief Thomas Marealle, kwa kukumbushia yale maurongo yako ya siku za nyuma kwa sababu threads za maurongo hayo zipo.

Be at peace Maalim wetu, maurongo weka kando, sasa tuenende kwenye ukweli mtupu, tell only the truth and nothing else, but the truth and it is only the truth that will set you free from all the ill motives behind.

P.
 
Mag 3,
Labda huenda umenisahau:
  1. PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  5. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  6. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2019 Dar es Salaam.
  8. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  9. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  10. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  11. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  12. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  13. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  14. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  15. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  16. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  17. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  18. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  19. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  20. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
  21. Awards: Several Awards
  22. Visiting Scholar: (2011)
  23. University of Iowa, Iowa City, USA
  24. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
  25. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
  26. OTHER COUNTRIES VISITED
  27. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
Nadhani hizi zikiwa compiled pamoja, it's more than a Ph.D thesis, kama imeshindikana kabisa kupewa an academic Ph.D, umepewe hata doctorate ya heshima tuu kama Dr. Jakaya, ila sisi hapa jf kwa vile hatufungamani na yeyote, nitatoa motion kwa Invincible tukupe udakitari wa heshima kutoka hiki Chuo Kikuu cha JF.
P
 
Huyu side anaandika historia inayohusu wenziwe kiimani baaasi,yuko biased kinoma,sisomagi vitabu vya side
Gita...
Umesema kweli mimi nimeandika kitabu kinachohusu mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ikiwa somo hili hulipendi na hutaki kusoma kitabu hicho hakuna tatizo uamuzi ni wako hakuna wa kukushurutisha kwani wasomaji wa kitabu hiki ni wengi sana sasa kinakwenda toleo la nne na kipo huu mwaka wa 21.

1572356364501.png
 
Back
Top Bottom