Kumbe watu hawasomi hata magazeti mleta hoja hii mada inazaidi ya mwezi kwenye magazeti yeye ndiyo kaiona mpya.
Mleta mada angeweka tarehe ya hii habari!
Mangula is right; mwelekeo ni serikali moja tu siyo serikali tatu...
Hebu watanganyika jiulizeni kwanini nyerere ilimshinda kuimeza zanzbr?kuimeza zanzbr ni ngumu ni sawa kuambiwa umeze mkuki,kaunganeni na kenya muigeuze jimbo lakini kwa zanzbr mumechelewa,hakuna sheria iliyotumika kuifuta tanganyika ni upumbavu wake mwenyewe mzee kifimbo cheza.
Kumbe watu hawasomi hata magazeti mleta hoja hii mada inazaidi ya mwezi kwenye magazeti yeye ndiyo kaiona mpya.
Mkuu huku wanafikiria ulaji tu hawaangalii factor zingine. Km sote tungekuwa na mawazo ya serikali moja hii nchi ingesonga mbele.hakuna umuhimu wa miserikali mingi, ya nn?? Dunia inaungana ss tunajigawaMangula is right; mwelekeo ni serikali moja tu siyo serikali tatu...
Mleta mada angeweka tarehe ya hii habari!
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula
MWELEKEO wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mabadiliko ya muundo mpya wa Serikali ya Muungano, ni wa kuwa na Serikali moja, yenye Rais mmoja atakayesaidiwa na mawaziri wakuu wawili wenye hadhi sawa, mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine kutoka Zanzibar, imefahamika.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, ameliambia Raia Mwema kuwa pamoja na kwamba sera ya sasa ya chama chake ni kuwa na muundo wa Muungano wenye Serikali mbili, lakini yeye binafsi ni muumini wa Serikali moja ya Muungano, yenye Rais mmoja. Mangula, katika maoni yake hayo, anasema angependa Katiba Mpya ipendekeze muundo wa Serikali ya Muungano yenye Rais mmoja, atakayesaidiwa na mawaziri wakuu wawili au viongozi wakuu wawili kulingana na jinsi Katiba itakavyoona inafaa vyeo vyao viitwe, watakaokuwa wasimamizi wakuu wa shughuli za Serikali katika pande mbili zinazounda Muungano huo, kwa maana ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, wakimsaidia Rais wa Muungano katika maeneo yao hayo.
........
- See more at: Raia Mwema - Mangula hamtaki Makamu Rais
....Unachokisema hapo ni serikali tatu tu mkuu,kuwa na Baraza dogo ilihali bado kuna mabaraza mengine mawili ya mawaziri ni upofu.Suala muhimu hapa ni kuwa serikali moja isiyotuletea gharama kubwa ktk matumizi.Hoja ya Mangula isipotoshwe labda kama nia ni kuuvunja Muungano.
This is good idea. Hii kidogo inaleta maana. Coz tutakuwa na serikali moja. This is good i support it.
I proposed this to the "Tume ya mabadiliko ya Katiba" kuwa Tanzania Bara kuwepo na Waziri Mkuu, Zanzibar nako kuwepo na Waziri Mkuu, rais abakie kuwa wa JMT.
watanzania wakati mwingine sijui tunakua na mawazo gani.Kiongozi anatuambia serikali tatu ni gharama,wakati huohuo anatuambia kuwe na muungano wa serikali moja ina mawaziri wakuu wawili, hili kwangu ni sawa na kuwa na serikali tatu.Kama wanataka muungano wa serikali moja, tuwe na rais mmoja na waziri mkuu mmoja ,halafu tuwe na majimbo.Zanzibar litakua ni jimbo.Lakini ukitaka kila sehemu itoe waziri mkuu bado manung'uniko yataendelea tu hasa kwa hao wazanzibar.CCM hapa inacheza ngoma ya kuokoa chama chao kwani nje ya muungano hakuna CCM.