Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula
MWELEKEO wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mabadiliko ya muundo mpya wa Serikali ya Muungano, ni wa kuwa na Serikali moja, yenye Rais mmoja atakayesaidiwa na mawaziri wakuu wawili wenye hadhi sawa, mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine kutoka Zanzibar, imefahamika.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, ameliambia
Raia Mwema kuwa pamoja na kwamba sera ya sasa ya chama chake ni kuwa na muundo wa Muungano wenye Serikali mbili,
lakini yeye binafsi ni muumini wa Serikali moja ya Muungano, yenye Rais mmoja. Mangula, katika maoni yake hayo, anasema angependa Katiba Mpya ipendekeze muundo wa Serikali ya Muungano yenye Rais mmoja, atakayesaidiwa na mawaziri wakuu wawili au viongozi wakuu wawili kulingana na jinsi Katiba itakavyoona inafaa vyeo vyao viitwe, watakaokuwa wasimamizi wakuu wa shughuli za Serikali katika pande mbili zinazounda Muungano huo, kwa maana ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, wakimsaidia Rais wa Muungano katika maeneo yao hayo.
........
- See more at:
Raia Mwema - Mangula hamtaki Makamu Rais