Mangula hamtaki Makamu Rais

Mangula hamtaki Makamu Rais

Mangula is right, serikali moja tu, zanzibar iwe na waziri mkuu na tanganyika iwe na waziri mkuu.
Ila wasiwasi wangu ni kutokea kwa huu ujinga wa kupokezana uraisi, eti kama this tme ametoka bara basi next time atoke zanzibar. Rais apatikane kutokana na sifa zake na sio anatoka upande gani wa muungano
 
Wananchi tupigie debe hili suluhisho... In fact serikali zitakuwa mbili zinazoongozwa na mawaziri wakuu lakini hawa nao wana-report kwa president mmoja!
Zanzibar wamepata, Tanganyika Wamepata! Win-Win. If you look critically jamaa ame-improve idea ya serikali tatu which is good.Ambacho hakuweka wazi ni mfumo wa bunge/ uwakilishi? Je Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na mabunge yake separate?
 
Hebu watanganyika jiulizeni kwanini nyerere ilimshinda kuimeza zanzbr?kuimeza zanzbr ni ngumu ni sawa kuambiwa umeze mkuki,kaunganeni na kenya muigeuze jimbo lakini kwa zanzbr mumechelewa,hakuna sheria iliyotumika kuifuta tanganyika ni upumbavu wake mwenyewe mzee kifimbo cheza.
 
Hili ni wazo kidogo linaweza kuelekea kulekule karibu ya mkataba, hapa rais ambaye atateuliwa ni yule atakae simamia hiki kitengo cha muungano tu, mamlaka zaid yaende kwa hawa mawaziri wakuu kwaiyo znz itakua na mamlaka yake kamili na Tanganyika itakua na mamlaka yake kamili, zanzibar iwepo ikulu ndogo ya rais wa muungano na Tanganyika vilevile, marais hawa watoke pande zote 2 kwa kila kipindi upande wake. Mamlaka yote ya kuendesha nchi yasimamiwe na waziri mkuu wa kila nchi yake na mambo yake.
 
Hebu watanganyika jiulizeni kwanini nyerere ilimshinda kuimeza zanzbr?kuimeza zanzbr ni ngumu ni sawa kuambiwa umeze mkuki,kaunganeni na kenya muigeuze jimbo lakini kwa zanzbr mumechelewa,hakuna sheria iliyotumika kuifuta tanganyika ni upumbavu wake mwenyewe mzee kifimbo cheza.


WAJUA MIMI NASHANGAA, WATU WENGI WAKO KICCM, KIFISADI, PIA KIHUNI ZAID,

JAMANI NASI WABARA TNATAKA TANGANYIKA YETu, MAWAKALA WA MASHETANI Yani CCM MSITUPELEKESHE, NYIE MKO KIMASLAI ZAIDI, MNAWAZA MADARAKA PIA UFISADI KWAN RASIM II YA KATIBA INAWATISHA
 
Wazo la Mzee Mangula imani yangu litapitishwa na wajumbe wa mabaraza; serikali tatu za nn? Kama ni muungano nchi iwe moja, kama wenzetu hawataki muungano basi tuuvunje kila mtu awe kivyake....
 
Mangula is right; mwelekeo ni serikali moja tu siyo serikali tatu...
Mkuu huku wanafikiria ulaji tu hawaangalii factor zingine. Km sote tungekuwa na mawazo ya serikali moja hii nchi ingesonga mbele.hakuna umuhimu wa miserikali mingi, ya nn?? Dunia inaungana ss tunajigawa
 
Mbona tunarogwa??????????

1. Kutengana sii dhambi!! Jana 28/06, Serbia imeanza mazungumzo kujiunga na EU baada ya kujitenga na Bosnia-Hezgivinia, na Montenegro. Croatia nayo itakuwa mwanachama wa EU tangu tar. Julai! mifano ipo to mingi!! Hawa wote walikuwa shirikisho moja la Yugoslavia!

2. Kwa nini ni lazima kwanza bara ijiunge na Visiwani ndo eti hapo tujiunge na Jumuia ya Afrika Mashariki?? Why????

3. Mbona katika mpira wa miguu- Kagame Cup (CECAFA), Mashindano ya Mabingwa Afrika.. timu za bara hazijiungi kwanza na Zanzibar katika kushiriki?? na tunapeta tu??



3. Kama sii serikali moja basi tutengane.. kututane Afrika Mashariki! Wazanzibari watakuwa huru kuja bara na bara kuja Visiwani kama Kenya wanavyokuja Tanzania kwa sasa!

4. Kwa nini tunalazimisha Muungano wa serikali mbili au tatu wakati uwazi na ukweli unaonekana??

Je tunalazimasha kwa manufaa ya nani??

5. Why?? These are fundamental issues!
 


Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula



MWELEKEO wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mabadiliko ya muundo mpya wa Serikali ya Muungano, ni wa kuwa na Serikali moja, yenye Rais mmoja atakayesaidiwa na mawaziri wakuu wawili wenye hadhi sawa, mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine kutoka Zanzibar, imefahamika.

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, ameliambia Raia Mwema kuwa pamoja na kwamba sera ya sasa ya chama chake ni kuwa na muundo wa Muungano wenye Serikali mbili, lakini yeye binafsi ni muumini wa Serikali moja ya Muungano, yenye Rais mmoja. Mangula, katika maoni yake hayo, anasema angependa Katiba Mpya ipendekeze muundo wa Serikali ya Muungano yenye Rais mmoja, atakayesaidiwa na mawaziri wakuu wawili au viongozi wakuu wawili kulingana na jinsi Katiba itakavyoona inafaa vyeo vyao viitwe, watakaokuwa wasimamizi wakuu wa shughuli za Serikali katika pande mbili zinazounda Muungano huo, kwa maana ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, wakimsaidia Rais wa Muungano katika maeneo yao hayo.
........
- See more at: Raia Mwema - Mangula hamtaki Makamu Rais

Tukiweza hili....basi muungano utakuwa na maana zaidi.
 
....Unachokisema hapo ni serikali tatu tu mkuu,kuwa na Baraza dogo ilihali bado kuna mabaraza mengine mawili ya mawaziri ni upofu.Suala muhimu hapa ni kuwa serikali moja isiyotuletea gharama kubwa ktk matumizi.Hoja ya Mangula isipotoshwe labda kama nia ni kuuvunja Muungano.

watanzania wakati mwingine sijui tunakua na mawazo gani.Kiongozi anatuambia serikali tatu ni gharama,wakati huohuo anatuambia kuwe na muungano wa serikali moja ina mawaziri wakuu wawili, hili kwangu ni sawa na kuwa na serikali tatu.Kama wanataka muungano wa serikali moja, tuwe na rais mmoja na waziri mkuu mmoja ,halafu tuwe na majimbo.Zanzibar litakua ni jimbo.Lakini ukitaka kila sehemu itoe waziri mkuu bado manung'uniko yataendelea tu hasa kwa hao wazanzibar.CCM hapa inacheza ngoma ya kuokoa chama chao kwani nje ya muungano hakuna CCM.
 
wanaolazimisha ni CCM ,kwani nje ya Muungano hakuna kitu inaitwa CCM, kuna TANU na AFRO SHIRAZ.
 
This is good idea. Hii kidogo inaleta maana. Coz tutakuwa na serikali moja. This is good i support it.

Tatizo la proposition hii ni kwamba kuna siku rais wa serkali ya muungano anaweza kutoka Zanzibar!! Hii sitaki kusikia
 
watanzania wakati mwingine sijui tunakua na mawazo gani.Kiongozi anatuambia serikali tatu ni gharama,wakati huohuo anatuambia kuwe na muungano wa serikali moja ina mawaziri wakuu wawili, hili kwangu ni sawa na kuwa na serikali tatu.Kama wanataka muungano wa serikali moja, tuwe na rais mmoja na waziri mkuu mmoja ,halafu tuwe na majimbo.Zanzibar litakua ni jimbo.Lakini ukitaka kila sehemu itoe waziri mkuu bado manung'uniko yataendelea tu hasa kwa hao wazanzibar.CCM hapa inacheza ngoma ya kuokoa chama chao kwani nje ya muungano hakuna CCM.

Kama kweli tunauhitaji na kuutaka muungano, hili ni pendekezo more realistic na lenye akili. Lina maana kuliko porojo zonazopigwa na wapuuzi. Rais wa Jamhuri na mawaziri wakuu wawili kimsingi ni serikali moja. Tofauti na tukiwa na rais wa bara, visiwani na wa muungano, na kila mmoja awe na waziri mkuu wake.

Lakini Mangula anatakiwa kueleza vizuri inakuwaje kama CUF inashinda Zanzibar ina kuwa na Waziri kiongozi, Chadema inakuwa na majority ya wabunge na kuwa na PM bara, na CCM inashinda urais? kweli kwa hili ni kama Mangula yuko bubu. Itakuwa taabu zaidi pale zanzibara CUF na CCM wanakuwa droo, itakuwa mawaziri kiongozi wawili? au?

Tatizo la Mzee wetu Mangula ni kuwa bado anafikiria party Supremacy na sio Supremacy ya Tanzania over parties. Kwake CCM ni each and everything.
 
Back
Top Bottom