Mangula hamtaki Makamu Rais

Mangula hamtaki Makamu Rais

Naheshimu sana mawazo ya wengine na hususan ya Mzee Mangula

Msingi wa hoja wa mapendekezo ya Mzee Mngula ni UONGOZI. Mimi na umri wangu mkubwa nimefurahiwa sana na mapendekezo ya Katiba yaliyojikita karibu kila eneo. Kwangu mimi katiba ni zaidi ya uongozi.

Vitu nilivyoviona kwenye mapendekezo ya baadhi yetu sisi wananchi wakawaida wa pande zote vilijikita katika yafuatavyoa:-

1. Utaifa na Utamaduni: Pamoja na kuwa na Zanzibar kutokuwepo Tanganyika kwa jina ni kama kutuvua nguo Watanganyika. Maana asiye na asili ni mtumwa.

2. Uchumi na Ardhi: Hapa sisi wengine tunatafsiri kuwa kutokuwepo kwa umiliki wa uchumi mikononi mwa wananchi ndani ya katiba kwa kisingizio cha utaifa ni dosari na uchungu tulioshuhudia kwa watawala kuabuse na kufuja haki ya msingi ya mwananchi na uananchi.

3. Uongozi: Hapa ndipo wengine kama Mzee Mangula na chama chake wanatuchanganya. Msingi wa uongozi hata kwenye mapendekezo ya Katiba ni watu yaani wapiga kura. Maoni yake yanataka raisi sijui Waziri Mkuu, lakini sisi wengine tungetaka uongozi tunaoweza kuuwajibisha. Kwa hiyo kupanua wigo wa uraisi fursa ya kumwajibisha inakosa maana. Hivyo hivyo ya Mawaziri Wakuu. Binafsi na kwa ushuhuda tu kuimarika kwa uongozi wa kuchaguliwa kihalali kwenye mitaa (Local) ndiyo mfumo mwendelezo wa uwakilishi kwa kupanuka hadi ngazi ya juu.

4. Huduma za Kijamii: Hizi zinaamua mahitaji ya local area na kitaifa. Hapa kwetu tumeingiliwa na fikra potofu kuwa wote tutafaidika sawa kama taifa wakati kiutendaji sivyo.

5. etc Ulinzi na usalama, rasilimali

Mimi simuungi mkono mzee mwenzangu kwa sababu uongozi anaoupendekeza haujibu hoja za kumnufaisha mwananchi kwenye vitu vya msingi zaidi ya kuondoa uwajibikaji makini unaoweza kumfikia mwananchi kwa kuuwajibisha uongozi. Pia simuungi mkono kwa sababu nadhani amejikita kwenye dhana ya mtu kama kiongozi na si mfumo unaowakumbatia watu wote.

Kwa misingi ya hoja yangu siutaki muungano kabla ya Utaifa wa Tanganyika na Zanzibar kushika nafasi zake.
 
Taifa lilikuwa linahitaji kura ya maoni kuhusu muungano kabla ya kukimbilia kuunda tume ya kukusanya maoni ya katiba. Kwa kukubali uwepo wa tume, wananchi wa pande zote mbili za visiwani na bara wamenyimwa fursa muhimu ya kuamua mustakabali wao na wa vizazi vijao. Matokeo ya kura ya maoni ndiyo yangetumika kutengeneza hadidu rejea za tume na mchakato mzima. Jambo hili lingewezesha hata kupunguza gharama za zoezi zima. Ila kwa dhihaka hii dhidi ya wananchi, watawala wetu wamezidi kutuonyesha thathmini yao ya dhana nzima ya demokrasia pamoja na ile ya wananchi wa kawaida.

Mapungufu ya zoezi zima la kurasimu katiba mpya na rasimu yenyewe yamezidi kuifanya katiba ya mwaka 1977 kuonekana ni bora zaidi. Ni vyema hata taifa lisingeingizwa katika "mduara" huu !
 
Anasema mangula serikali tatu za marais wa tatu ni ghali na kutoa mfano wakistaafu kutakuwa na marais wastaafu watatu wa kutazamwa na serikali, anasahau hao prime ministers nao watakuwa hawana pia haki zao za kutazamwa na serikali wakistaafu? utasemaje ni gharama kuziendesha wakati hujajua hili litaendeshwa na yupi na lipi la kuchangia? Katika mfumo wa sasa jee hakuna malalamiko ya gharama kubebwa na upande mmoja na huku mwengine akilalamika kunyimwa haki? na jee katika mfumo huo wa prime ministers wa pande husika rais atakuwa na nguvu gani mbele ya prime ministers hasa ikiwa ni wa kuchaguliwa kwa kura za wananchi? Au atawateua yeye mwenyewe? vipi pannapotokea kuwapo kwa serikali za coalition rais atachaguwa vipi ikiwa ni mfumo wa yeye kuuwachagua prime ministers? maoni yangu ni mkataba kama tunataka kikweli kuondosha lawama ni mamlaka kamili kwa nchi husika na baadhi ya mambo kuwamo ndani ya muungano, hakuna haja ya kuwa na rais wa kuchaguliwa wa muungano, nafasi ibakie ya ceremonial tu, nguvu zikirejeshwa ndani ya bunge kwenye representation ya wananchi moja kwa moja na kukiwa na baraza la mawaziri kwa yale yatayokubaliwa, au ni serikali moja ikiwa wananchi wataridhia kwa pande zote bila ya kushurutishwa na kutishwa, ikiwa haiwezekani hayo basi na tumalizane kwa kheri na Baraka.. Sijaliona kubwa la mangula..Bora warioba kaanza katika strong stand..my veiws
 
Mangula anataka tumpe maneno yake tufungiwe, hiyo proposal yake akawafanyiw wanyakyusa wenzake walioshiba kangara kama yeye sisi Wazanzibari hatuna haja ya muungano na yoyote si mnasema tunawanyonya sasa si kila mtu kivyake?
 
..je, Mzee Mangula anapendekeza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ifutwe?
..je, hao mawaziri wakuu wa Tanganyika na Zanzibar watakuwa wanapatikana kwa utaratibu gani?
..mwisho, hao mawaziri wakuu wanaopendekezwa watakuwa na mamlaka gani?
NB:..nakumbuka kuna wakati CUF walipendekeza kuwe na gavana wa Tanganyika, na gavana wa Zanzibar.
JokaKuu, unajua ninaposikia watu wanapinga serikali 3 nashangaa.

Mangula alikuwepo katika uongozi wakati wa tume ya Kisanga, Nyalali na ile ya Warioba ya kwanza.
Hakufanya chochote kurekebisha hali, leo anakujaje kutoa maoni kuhusu kile alichoshindwa kukirekebisha akiwa madarakani?

Pili, Mangula anapendekeza SMZ ifutwe wakati wznz wanataka passport zao. Sijui hapa amekusudia nini kwasababu ni wazi kuwa hoja yake ni next to impossible.Kama wameondoa baraza la mitihani atawashaurije waondoe SMZ

Kuhusu upatikanaji wa mawaziri wakuu hilo nalo linafungamana na hoja hapo juu kuwa tatizo znz wanaloliona ni kuwa na rais mwenye bendera na wimbo wake wa taifa.

Wakati wanadai mizinga ya heshima na ilipoanza 19 hadi 21 Mangula alikuwa kiongozi hakufanya lolote, iweje leo adhani kuwa wzn watabadili mwenendo

Mamlaka ya hao mawaziri wakuu itakuwa kumsaidia rais kwa mujibu wa Mangula.
Hajaeleza watamsaidiaje rais wakati huu wa vyama vingi ambapo kuna uwezekano wa rais wa upande mmoja kuwa wa chama tofati.

Na pia hajaanisha ni kwa njia zipi huyo rais atapatikana kwa kuzingatia unfriendly political atmosphere iliyopo

Halafu anasema serikali 3 ni mzigo, ninashangaa kwasababu hata ikiwa moja ni mzigo tayari.
Hebu atuonyeshe unafuu uliopo. Inaonekana anadhani serikali 3 zitagharamiwa na Tanganyika.
Mi nadhani kila serikali itajihudmia unless aseme moja haina uwezo.

Kama moja haitakuwa na uwezo na bila shaka ni znz basi hapo hana sababu za kusema rais wa Tanganyika atakuwa super president, of course yes! mbona haangalii senate anayosema ambayo itakuwa na uwakilishi sawa.

Anasema kutakuwa na marais 9 wa kuwahudumia. What's wrong with that. Hao wanaopanga mafao si wao kwanini wasifikirie tatizo hilo. So far tunaona 5 mbona hajaona mzigo. Lakini pia kila serikali itakuwa na wajibu wa kuhudumia watu wake.

Nadhani angependekeza kuwa rais akistaafu abaki na mafao kidogo kama matibabu lakini chakula na malazi awe sawa na mstaafu mwingine. Hapo hata wakiwa 21 hakuna gharama.

Na kwanini anaamini kuwa wote hao watahudumiwa na Tanganyika? Kama sivyo kwanini awe na wasi wasi na let say SMZ kuhudumia marais wake ambao hadi sasa ni 3.

Inaonekana watu wanadhani kuwa ukiwa na gunia la kilo 120 ni jepesi sana kuliko kuligawa katika mafungu 3 ya kilo 40.

Mi nadhani suluhu hapa ni moja tu kutafuta mahali pa kushirikiana na nadhani pazuri ni EAC, SADCC, FIFA, CHANETA/CHANEZA, CECAFA, AU, UN, n.k.

Nakubaliana na nasaha zako kwa Watanganyika.
 
Mkuu Mimibaba nadhani hoja zako hapo juu zinashabihiana kwa kiasi na hoja ya JokaKuu.
Ukimsoma Mangula anachoongelea zaidi ni upatikanaji wa viongozi,kugawana madaraka na gharama za kuwatunza siku za baadaye.

Mangula hajaongelea uongozi huo unapatikana kwa taratibu gani na mwananchi anashirikishwaje katika kuchagua uongozi wake. Ameacha hoja muhimu sana za manung'uniko yaliyopo kuhusu muungano kutoka kwa wananchi na amejikita kaika mgao wa madaraka na matunzo ya familia

Na muhimu sana Mangula kama walivyo viongozi wengi wanasahau kuwa nchi ni mali ya wananchi na si kikundi cha watu.

Lini wameuliza kuhusu muungano? Je, si wakati sasa wznz ambao wanaonekana kutotaka muungano kupewa nafasi ya kura ya maoni ili tujue wapi tunaelekea.

Kwasasa haijulikani kama znz wanataka muungano au la. Ukisoma habari za viongozi wao wengi zinachanganya, tuamini kuwa hawataki. Lakini ni muhimu tukawa na evidence kuwa hawataki.

Upo uwezekano wa basi lenye abiria 65 na kati yao walevi 5 wakapiga kelele sana na basi zima kuonekan lina wapiga kelele. Tunataka evidence ambayo ni referendum kwa znz. Ni utaratibu wa kawaida duniani

Kwanini znz basi wasipewe fursa na kama wataamua basi wote kwa pamoja Tanganyika na znz wananchi waulizwe wanataka iweje.

Pamoja na hayo hapa tulipofikia naungana na hoja ya JokaKuu, nadhani Watanganyika wanapaswa kuamka na kujuliza sana kama umuhimu upo na kwa faida ipi. Hili ni muhimu sana!
 
Ilikuwaje CCM mkamba muhuni nchemba wadhifa wenye majukumu makubwa hivyo! Nafasi hizo hupewa watu wenye busara zao, Na CCM inao! Hawa jamii ya NAPES wana nafasi zao jamani!
 
Naheshimu sana mawazo ya wengine na hususan ya Mzee Mangula

Msingi wa hoja wa mapendekezo ya Mzee Mngula ni UONGOZI. Mimi na umri wangu mkubwa nimefurahiwa sana na mapendekezo ya Katiba yaliyojikita karibu kila eneo. Kwangu mimi katiba ni zaidi ya uongozi.

Vitu nilivyoviona kwenye mapendekezo ya baadhi yetu sisi wananchi wakawaida wa pande zote vilijikita katika yafuatavyoa:-

1. Utaifa na Utamaduni: Pamoja na kuwa na Zanzibar kutokuwepo Tanganyika kwa jina ni kama kutuvua nguo Watanganyika. Maana asiye na asili ni mtumwa.

2. Uchumi na Ardhi: Hapa sisi wengine tunatafsiri kuwa kutokuwepo kwa umiliki wa uchumi mikononi mwa wananchi ndani ya katiba kwa kisingizio cha utaifa ni dosari na uchungu tulioshuhudia kwa watawala kuabuse na kufuja haki ya msingi ya mwananchi na uananchi.

3. Uongozi: Hapa ndipo wengine kama Mzee Mangula na chama chake wanatuchanganya. Msingi wa uongozi hata kwenye mapendekezo ya Katiba ni watu yaani wapiga kura. Maoni yake yanataka raisi sijui Waziri Mkuu, lakini sisi wengine tungetaka uongozi tunaoweza kuuwajibisha. Kwa hiyo kupanua wigo wa uraisi fursa ya kumwajibisha inakosa maana. Hivyo hivyo ya Mawaziri Wakuu. Binafsi na kwa ushuhuda tu kuimarika kwa uongozi wa kuchaguliwa kihalali kwenye mitaa (Local) ndiyo mfumo mwendelezo wa uwakilishi kwa kupanuka hadi ngazi ya juu.

4. Huduma za Kijamii: Hizi zinaamua mahitaji ya local area na kitaifa. Hapa kwetu tumeingiliwa na fikra potofu kuwa wote tutafaidika sawa kama taifa wakati kiutendaji sivyo.

5. etc Ulinzi na usalama, rasilimali

Mimi simuungi mkono mzee mwenzangu kwa sababu uongozi anaoupendekeza haujibu hoja za kumnufaisha mwananchi kwenye vitu vya msingi zaidi ya kuondoa uwajibikaji makini unaoweza kumfikia mwananchi kwa kuuwajibisha uongozi. Pia simuungi mkono kwa sababu nadhani amejikita kwenye dhana ya mtu kama kiongozi na si mfumo unaowakumbatia watu wote.

Kwa misingi ya hoja yangu siutaki muungano kabla ya Utaifa wa Tanganyika na Zanzibar kushika nafasi zake.

Mzee na wewe ni kati ya watu wenye damu mikononi inayotpkana na vitendo vya ufisadi?
 
Back
Top Bottom