Mimibaba
JF-Expert Member
- Jul 1, 2009
- 4,557
- 1,294
Naheshimu sana mawazo ya wengine na hususan ya Mzee Mangula
Msingi wa hoja wa mapendekezo ya Mzee Mngula ni UONGOZI. Mimi na umri wangu mkubwa nimefurahiwa sana na mapendekezo ya Katiba yaliyojikita karibu kila eneo. Kwangu mimi katiba ni zaidi ya uongozi.
Vitu nilivyoviona kwenye mapendekezo ya baadhi yetu sisi wananchi wakawaida wa pande zote vilijikita katika yafuatavyoa:-
1. Utaifa na Utamaduni: Pamoja na kuwa na Zanzibar kutokuwepo Tanganyika kwa jina ni kama kutuvua nguo Watanganyika. Maana asiye na asili ni mtumwa.
2. Uchumi na Ardhi: Hapa sisi wengine tunatafsiri kuwa kutokuwepo kwa umiliki wa uchumi mikononi mwa wananchi ndani ya katiba kwa kisingizio cha utaifa ni dosari na uchungu tulioshuhudia kwa watawala kuabuse na kufuja haki ya msingi ya mwananchi na uananchi.
3. Uongozi: Hapa ndipo wengine kama Mzee Mangula na chama chake wanatuchanganya. Msingi wa uongozi hata kwenye mapendekezo ya Katiba ni watu yaani wapiga kura. Maoni yake yanataka raisi sijui Waziri Mkuu, lakini sisi wengine tungetaka uongozi tunaoweza kuuwajibisha. Kwa hiyo kupanua wigo wa uraisi fursa ya kumwajibisha inakosa maana. Hivyo hivyo ya Mawaziri Wakuu. Binafsi na kwa ushuhuda tu kuimarika kwa uongozi wa kuchaguliwa kihalali kwenye mitaa (Local) ndiyo mfumo mwendelezo wa uwakilishi kwa kupanuka hadi ngazi ya juu.
4. Huduma za Kijamii: Hizi zinaamua mahitaji ya local area na kitaifa. Hapa kwetu tumeingiliwa na fikra potofu kuwa wote tutafaidika sawa kama taifa wakati kiutendaji sivyo.
5. etc Ulinzi na usalama, rasilimali
Mimi simuungi mkono mzee mwenzangu kwa sababu uongozi anaoupendekeza haujibu hoja za kumnufaisha mwananchi kwenye vitu vya msingi zaidi ya kuondoa uwajibikaji makini unaoweza kumfikia mwananchi kwa kuuwajibisha uongozi. Pia simuungi mkono kwa sababu nadhani amejikita kwenye dhana ya mtu kama kiongozi na si mfumo unaowakumbatia watu wote.
Kwa misingi ya hoja yangu siutaki muungano kabla ya Utaifa wa Tanganyika na Zanzibar kushika nafasi zake.