Mwanzoni nilikuwa nadhani wanamsingizia ila sasa kadhihirisha wazi kuwa ana kazi maalumu pale Simba. Washabiki, wapenzi na wanachama wa Simba jiandaeni kwa msimu mwingine wa kulia na kusaga meno. Kama kweli huyu mzee angekuwa Simba damu damu zile goli tano jumlisha kushika nafasi ya tatu zingekuwa sababu tosha za yeye kujiuzulu na kupisha wengine waongoze na sio kujibu kifedhulfedhuli namna hiyo.
Huyu mtu hana aibu kabisa na sijui hana mke, majirani, marafiki au watoto au zaidi hata wakwe zake wa kumshauri aachane na Simba afakafanye shughuli zake kama anazo kuliko kung'ang'ania huo uongozi ambao watu kibao wameshampinga. Hivi na ile kamati ya wakina Zungu na Tulia kule bungeni Dodoma kwa nini isitume ujumbe kwake aachie ngazi kwa maslahi mapana ya Simba?
Kama anataka kuongoza mpira si lazima ang'ang'anie Simba si aende akaifufue Pan Africa. Si anasema anazo pesa za usajili si akasajili wachezaji Pan Africa ili wapande daraja? Kwa nini anang'ang'ania asajili wachezaji hapo Simba bado hajaridhika tu na magarasa waliyoyaleta anataka aengezee mengine?