Mangungu na Tray Again ni dhaifu ndio maana wapinzani wetu wanawapenda

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
4,095
Reaction score
13,016
Kwa sisi wazoefu wa football ya nchi hii tunajua kuwa, hizi timu mahasimu wawili simba na yanga zinahitaji kuwa na viongozi katili kweli kweli.

Jiulize kwanini mahasimu wetu yanga linapokuja suala la mangungu wanamtetea kweli kweli? Jibu ni hili, dhaifu rahisi kuingilika. Jamaa ni mbobevu kwenye masuala ya kushinda uchaguzi tu.

Huyu hakuwahi kuchaguliwa na wana simba, kwa sababu wanamjua kuwa hawezi kuipambania kweli kweli simba, ndani ya uongozi wake kumekuwa na sintofahamu nyingi sana.

Baada ya mo kumteua try again kama mwenyekiti wa bodi,ndio kama aliharibu kabisa, pipa na mfuniko vilikutana, tukala tano dhidi mtani. Timu ikawa hoe hae mtani akawa anajipigia tu.

Mambo yameanza kubadilika baada ya mo kumteua magori kama mwenyekiti wa bodi, alichokifanya magori ni kuwatimua wacheza wote ambao walisajikiwa na try again, isipokuwa mpanzu tu, ambaye walikaa nae chini na kuzungumza nae kabla ya kumpa mkataba mpya.

Hapa ndio simba mpya ikaanza kuonekana, siyo haba na vikombe viwili wakabeba kwenye uongozi wa magori, tena chini ya uongozi wa magori mtani kahenyeka vibaya.
 
Magori ana fweza na haitegemei Simba. Hao akina Mangungu na Try Again Simba ndio kula yao!
 
Shida unadhani mo ndio kila kitu na yeyote anaekuwa against nae ni adui yako!

Pole sana

Usiwaze mambo yako ukiwa na mo moyoni, mchukulie nae kama ni mangungu mwingine kisha tafakari
 
Back
Top Bottom